Picha: Mwingine familia ya Nyerere ajiunga CHADEMA

Picha: Mwingine familia ya Nyerere ajiunga CHADEMA

Mnatumia jina la Nyerere eti familia ya Nyerere.....kumbe mtoto wa Joseph Nyerere! Joseph Nyerere kwa Nchi hii ana umaarufu gani kama sio kulima viazi pale butiama? Familia ya Nyerere kwa kuamanisha Mwl Julius Nyerere ni akina Madara,makongoro,rose na wengine na sio hao machola wengine mnaotaka kuwapaisha kwa jina la baba yao mlima Viazi Joseph Nyerere! Acheni propaganda za kishamba

Kwa wanaojuwa historia...Jina la Joseph Nyerere sio la kubeza...Zaidi ya kuwa independent na kutenga jina lake kama Joseph..
Alishiriki harakati za mwanzo za TANU na kina Bibi titi..
Alikuwa Mwanzilishi wa TANU - Youth League
Waziri wa Mwanzo wa Vijana etc...

Nadhani Mwalimu angekuwa mtu wa kuibeba familia yake ....basi Joseph angeweza kujulikana Zaidi ..

Pia familia ya mwalimu wana nchi tunawasifu kwa kutoa Uhuru wa Mawazo binafsi....mnakumbuka mwalimu alijibu nini Pale Capt Makongoro alivojiunga NCCR...! Wengi walifikiri angemkana....lakini anasema alimruhusu na kumpa Baraka ...hii tena inaashiria ni Watu wanaopenda kujenga majina Yao Kama wao bila kutegemea la mwalimu....mnaona namna watoto wa viongozi wanavyosafiria nyota za baba Zao.

Pia wana chi tuna Amini mwalimu alikuwa mtu wa Extended family Kama Africa tunavyoamini...ukishafanikiwa hata watoto wa mpwa wako watajiita watoto wako na hakuna neno..hata kidogo sisi ni Waafrika
 
Huyo Francis baba yake ni Joseph Nyerere,sasa wana mleta hapa JF kwa akili ya kuamini kama nae ni mtoto wa Mwl Julius Nyerere! Ni ulimbukeni tu wa kujifanya familia ya Julius Nyerere mmoja wapo kahamia Chadema
Kwenye tasnia ya habari, big names makes big news!, kwenye siasa big names makes big political impact!, Jina la Nyerere sio tuu ndio the biggest name of all times kwenye politics za Tanzania!, linabeba the biggest political goodwill ya ukombozi wa nchi hii na the legacy ya CCM!.

Jina hili la Nyerere kwa Tanzania, ni kama Karumes kwa Zanzibar, Kenyattas kwa Kenya, Kenedies na Bushes kwa US, Gandhis kwa India etc, jina tuu peke yake linakupa political mileage ya kutosha!.

Kitendo tuu cha kutaja Mwanafamilia mwingine wa Nyerere ajiunga Chadema, its ment to send a strong meseg kwa wale waumini wa CCM kuwa ndicho chama cha Nyerere alichotuiachia, hivyo wataendelea kukichagua CCM milele kwa sababu tuu ya Nyerere, hata kiboronge vipi!, hivyo kama wanafamilia wa Nyerere wanaendelea kuhamia Chadema, then kumbe sasa CCM sio chama cha Nyerere tena, na labda kama angelikuwa hai saa hizi, angelishaachana na CCM zamani na kujiunga na Chadema!, hivyo hii ni kuwaeleza wale wote wanaoendelea kuikumbatia CCM pamoja na madudu yake yote kwa heshima tuu ya Nyerere, sasa ni wakati wa kuinga mkono Chadema, kwa sababu kina Nyerere sasa wanajiunga Chadema!.

Politics strategies is about making moves that will bring most impact, more members and establish more trust ahead of 2015!. Its a "good move!".
Pasco.
 
Pauleta Nyerere anatajwa Kama mtoto wa mwisho ambae mwalimu na mama maria walimu adopt....So ni mdogo wenu wa mwisho?

Bado unaamini kwenye CCM( TANU) ya Arusha au Zanzibar ?....
Ndiyo,Pauleta ni legally adopted.
CCM wapo rank and file ambao bado wanaamni katika maadili mema ya uongozi.
 
Hivi,yule bibi MARIA naye anasubili nn asijiunge na CDM,,?maana hata babu angekua hai naye angeshatujoin kitaaamboooooo


Weweee!! Hauoni Magamba wanavyojipendekeza kwake? Mama,kwa sasa anapendeza kuliko hata alipokuwepo Teacher!!
 
Mkuu Watanzania wengi wangapi? Mwaka 2010 Watanzania tulikuwa wangapi kwa makadirio? na ni Watanzania wangapi tulipiga kura? Je ni Watanzania wangapi waliopia kura CCM? Mwisho ni Watanzania wangapi ambao wahakupiga kura? Na unadhani ni kwa nini hawakupiga kura?

Labda kuna watu hawakwenda kupiga kura kwa kuogopa fujo za Chadema. Lakini sijafuatilia hiyo stori ya watu kutojitokeza kupiga kura.
 
Kila mmoja ana uhuru wa kuamini anachofikiri ni sahihi kukiamini.Tuheshimu maamuzi ya watu/marafiki zetu yanayopingana na fikra zetu. Jina la ukoo halina hati miliki ya mtu mmoja,si kampuni wala alama ya biashara.Hoja ni muhimu kunishawishi kufuata mawazo yako;si matusi na kejeli.:bange:
 
Babako hakuwa mchumia tumbo, wewe unaanza kuwa mchumia tumbo uzeeni utaweza?...Sitaki jibu lako ila ninauhakika dhamira inakusuta sana...wee endelea kutoza ada kwa waokuja kuhiji kaburi la baba...

RIP Mwalimu ulipigania nchi hii lakini wale maadui uliokuwa unapambana nao kwa dhaati wameongezeka sasa wamefika wa 4! UFISADI, UJINGA, UMASIKINI NA MARADHI...

'Dhamira inakusuta'.ndivyo alivysema mama mmoja katika uchaguzi uliopita alipohojiwa on TV;'nikitaka kuwapigia kura wapinzani,moyo wangu unanisuta' Yule mama amewafanya wengi kuipigia kura CCM kuliko kampeni yote aliyofanya JK.
 
What joseph nyerere?? Makongoro nyerere mtoto wa baba wa taifa wa kuzaa(acha hao akina vicent na josephambao ni watoto wa kaka yake)alijiunga nccr-mageuzi mwaka 1995 baba wa taifa mwl.jk nyerere akiwa hai,na akashinda ubunge wa jimbo la arusha mjini,it wasn't an issue ya kuumiza mtu kichwa,na ndio maana makongoro aliporejea ccm,it wasn't an issue too.
 
Watoto wa Nyerere wanajulikana hii tabia ya ktumia majina ya wa tu kwa umaarufu haifai,Esther na Lilian Wasra nao walijifanya kama watoto wa Wasra kumbe ni geresha,sasa Mzee Joseph Nyerere nae ni nani katika nchi hii hadi mtoto wake apewe coverage kisa kujiunga na Chadema! Au mnatumia Jina la Nyerere kujifanya kama ni watoto wa Mwl Nyerere!

Umezaliwa mwaka 1992 utafahamu wapi historia ya nchi yetu?
 
Labda kuna watu hawakwenda kupiga kura kwa kuogopa fujo za Chadema. Lakini sijafuatilia hiyo stori ya watu kutojitokeza kupiga kura.
kwa kweli uombe radhi kwa kauli hii maana umemwaibisha baba wa taifa.navyomfahamu mzee wako angekuwa hai leo angekuwa Chadema. CCM hii siyo ile aliyoiasisi, siyo chama cha wakulima na wafanyakazi bali genge la wahujumu nchi,nchi ambayo baba yako na baba yangu walijitolea mhanga kuijenga kwa hata gharama ya maisha yao. Poti omba radhi
 
'Dhamira inakusuta'.ndivyo alivysema mama mmoja katika uchaguzi uliopita alipohojiwa on TV;'nikitaka kuwapigia kura wapinzani,moyo wangu unanisuta' Yule mama amewafanya wengi kuipigia kura CCM kuliko kampeni yote aliyofanya JK.

Kuna kila dalili kwamba wewe na makongoro mlisaliti dhamira ya babenu. Hamtafanikiwa na mkitaka kufanikiwa wanyang'anyeni chama mbwa mwitu hawa.
 
kwa kweli uombe radhi kwa kauli hii maana umemwaibisha baba wa taifa.navyomfahamu mzee wako angekuwa hai leo angekuwa Chadema. CCM hii siyo ile aliyoiasisi, siyo chama cha wakulima na wafanyakazi bali genge la wahujumu nchi,nchi ambayo baba yako na baba yangu walijitolea mhanga kuijenga kwa hata gharama ya maisha yao. Poti omba radhi

Aombe radhi ya nini kwani lazima kila mtu kuwa Chadema.

Uwezi kujua anafuata maagizo ya mzee wake ambaye ndiyo muasisi wa CCM.

Radhi za wazee ni mbaya.
 
Labda kuna watu hawakwenda kupiga kura kwa kuogopa fujo za Chadema. Lakini sijafuatilia hiyo stori ya watu kutojitokeza kupiga kura.

Unadhani Chadema wangelikuwa na fujo m.k.wele angelikuwa rais leo pamoja na wizi wote alofanya 2010?
Hujui unalosema maskini.
 
Nimependa haya maneno wewe kweli ndiyo mtoto wa Julius Nyerere rais wetu wa kwanza.

CC.. Yericko Nyerere, Kimbunga, chama, zomba,

Mkuu Ritz
Maneno ya Andrew Nyerere mujarab umesahau kum cc Molemo na Matola; ila mkuu naona Chadema wanabaguana sana kamanda wangu Mwita Maranya hajapata publicity hata moja; pamoja na jitihada kubwa anayofanya hii haniingii akilini hata kidogo yaani mtu anajituma kwa kadri ya uwezo wake;hatambuliwi wala kumsikia kwenye magazeti; wameingia kina Esther Wassira magazeti yote habari ya Chadema ilikuwa hiyo; leo kaingia Nyerere kina Lissu wote wapo si ajabu zaidi ya majina hawa watu hawana mchango wowote wa maana; jamaa inaonekana wazi wana utaratibu wa kubaguana kwa majina; mkuu inabidi tuliangalie hilo sio jambo dogo!

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Butola, comments nyingine ni za hatari sana!, angalia zisije zikaingiliana na zikatutibulia ule mchakato wetu wa Mwenye Heri kuelekea kwenye Utakatifu!.
P.

Kwani comment inaongeza,kupunguza au kubadili kitu penye ukweli...!!??
 
Back
Top Bottom