Kada mwandamizi wa CHADEMA kulalamikia mialiko ya ikulu ni ishara nzuri ya kukubalika kwa Rais Samia

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,223
22,302
Huko Instagram na Twitter kumetokea malalamiko ya kada mwandamizi na mjumbe wa mkutano mkuu wa CHADEMA ndugu Yericko Nyerere kuhusu kutoalikwa kwenye hafla ya futari iliyoandaliwa ikulu na Rais Dr Samia Suluhu ambaye pia ni mwenyekiti wa chama pendwa CCM. Nimesikitika na waandaaji kumsahau ndugu Yeriko kwenye hafla hii. Ingependeza kama angealikwa.

TUJIKUMBUSHE alichoandika Yeriko;
"Utaratibu wa Rais kualika Watz katika hafla za Ikulu ni wa kibaguzi ubadilike, Rais @SuluhuSamia anaongoza Watz wa kada zote, lakini mara nyingi kada inayopewa fursa nyingi za kufika Ikulu ni kada ya Wasanii, Viongozi wa Dini na kundi jipya katika nchi la Machawa. Haikubaliki!"

Binafsi siwezi sema kuwa Yeriko ana shida sana ya kwenda kufakamia futari iliyoandaliwa na mwenyekiti wa CCM bali naona anataka tu kutumia hiyo nafasi angalau hata kupiga picha na Mama Samia kwa sababu ya kumkubali sana jinsi anavyoiongoza nchi. Ninawasihi maafisa wa Ikulu kutomsahau Yeriko pale inapotokea hafla huko. Kiukweli mama anaupiga mwingi hadi makada wakubwa wa CHADEMA kama Yeriko wanashindwa kuficha hisia zao.

20240313_135025.jpg
 
Mimi nimeanzisha thread kabisa. Hakuna mahali Yeriko amelalamikia kutoalikwa Acha uzushi. Mama yenu kualika Chawa waliokula kitimoto mara 3 mchana ni kinyume cha taratibu za Uislamu. Tumemwambia tukiamini anajua vizuri thawabu za Ramadan zinapatikanaje.
 
Mimi kama nimemuelewa ile hafla kimsingi ilitakiwa kubance kila makundi lakini imeonekana kama ni mkutano wa CCM uliofanyika ikulu nilitegemea kuwaona makada wa vyama mbali mbali na wale watu hata wasio na vina saba vya CCM waalikwe kama kweli Rais ana maanisha kweli kwenye kuliunganisha taifa..! Yericko anayo hoja!
 
Anamzungumzia rais si mwenyekiti wa CCM, aliyeandaa ni rais kwa pesa za watanzania, jifunze kutofautisha nyazifa.

Alipoingia madarakani alisema, yeye ni rais, ni mwenyekiti wa CCM na ni mama.
 
Anamzungumzia rais si mwenyekiti wa CCM, aliyeandaa ni rais kwa pesa za watanzania, jifunze kutofautisha nyazifa.

Alipoingia madarakani alisema, yeye ni rais, ni mwenyekiti wa CCM na ni mama.
Makada wa CHADEMA kuna mambo mengine mnatakiwa tu mpotezee kulinda misimamo yenu. Kulalamikia futari ni uzwazwa
 
Back
Top Bottom