Watanzania Udini utatumaliza. Hivi tunafaidika nini kuwahukumu wengine kwa kutumia rungu la Udini? Mi nawashauri wananchi wenzangu, tujibidishe kwenye masuala yenye maslahi kwa taifa letu. Hivi kusema Prof. Lipumba ni Muislam, au chama chake ni cha Kiislam, na Kusema Dr. Slaa ni padre, na chama chake ni cha kanisa itatusaidia nini katika ukombozi wa taifa letu? Mi naamini wana JF ni critical Thinkers, na ni Agents wa mabadiliko popote walipo. Ninapomwona mwana JF analeta udini kwenye masuala nyeti kama haya ya ukombozi, nakuwa na wasi wasi na harakati za mwana JF huyo.
Tuna changamoto nyingi zinalikabili taifa, kama Ufisadi, Migomo ya kada mbali mbali, kudorora kwa elimu, Mfumuko wa bei, Mauaji ya raia wasio na hatia, mabadiliko ya tabia nchi, mabadiliko ya katiba n.k. Haya ndo mambo ambayo kama Critical Thinkers tunatakiwa tuyajadili, na siyo kujadili udaku wa udini.
Prof. Lipumba ni mtu muhimu kwa maendeleo ya Uchumi wetu Tanzania. Dr. Slaa ni mtu muhimu kwa kukomesha ufisadi na uonevu katika Taifa letu. Wapo na wengine wengi ambao ni muhimu katika mustakabali wa nchi yetu.
Nawaomba wana JF tubadilike. Hii tabia ya kupost threads na michango yenye kuleta udini ikome kuanzia leo. Tukumbuke kuwa JF imebeba dhamana ya watanzania milion 45, na tunapojadili, tunasaidiana ktk kufungua uwezo wa wenzetu kuona mbali. Mi nakiri kuwa JF imenisaidia sana katika nyanja zote. Sasa leo kama Intellectuals tukianza kujadili mambo ya udini, tutakuwa na tofauti gani na wale wazee kule vijijini, ambao kila siku Masheikh na wachungaji wanawahubiria masuala ya udini?
TU BA DI LI KE