PICHA: Mapokezi ya Prof Lipumba; Afande sele atumbuiza

Lipumba kama Lipumba namheshimu sana.Lakini kwa bahati mbaya sana yuko chama cha hovyo kabisa kuwahi kuwepo duniani.Lipumba akitaka heshima yake iendelee aachane na chama kilichojaa ubaguzi hasa wa kidini na kikanda.Karibu nyumbani Profesa.
 
Kwa taarifa nilizozipata ni kwamba Prof. Ibrahim Haruna Lipumba amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Maprofesa wa Uchumi Duniani. Kama hizi taarifa ni za kweli watanzania tujivunie kwa heshima aliotuletea mwanauchumi huyu. Pia yatupasa tumtumie atuinulie uchumi wetu unaozidi kudidimia siku hadi siku. Watanzania wenzangu tuache itikadi za siasa kwenye maslahi ya Taifa.Tusiangalie chama chake muhimu ni Elimu yake kwa maslahi ya Taifa la Tanzania.
 
LIpumba hatumiwi na watawala wa Tanzania kwa sababu watanzania wenyewe hawaamini katika sera za kibepari ambazo Lipumba amebobea. Watanzania wanapenda sana kufaidika na zao la mfumo wa kibepari lakini hawataki kabisa kuukubali mfumo wenyewe wa kibepari. kwa Ufupi watanzania kwenye mambo ya kiuchumi ni wasanii!!
 
jamani nipo hapa uwanja wa ndege kumefurika wanachama wa cuf........waliosema cuf imekufa leo sijui mtajificha wapi watu wamejaa wakimsubili mkubwa na bigwa wa uchumi duniani

Sikujua uhai wa CUF unamtegemea zaidi Prof. Lipumba!! Hivi CUF ni taasisi au ni asasi ya Prof. Lipumba. CUF haitafufuka kwa sababu ya Prof kurudi. Itakufa kwa sababu ya siasa za Kibara na Kizanzibari!!
 
Kwanza kabisa, hakupata ile nafasi kama KAFU representative
Pili ile kazi haihusiani na KAFU
Tatu tuna watanzania wengi sana wenye nafasi ZA juu sana duniani kama tungeamua kufunga airport basi tungefunga sana tu
NNe, ni dalili tosha kwamba kafu hawana hero wala anything to cheer up hadi wampokee consultant wa international agencies namna ile

Sijui sasa akirudi mama Migiro itakuaje.... maana angekua kafu wangefunga hata mwzi mzima kumsubiri

BTW, HONGERA PROF LIPUMBA.... GOOD JOB
 
WanaCUF bwana kwa Propaganda. Ooh watu wengi wamejazana Air Port! Picha hakuna! Jifunzuni kutoka kwetu Arumeru jana. Mkutano unaendelea picha zinarushwa wakati huo huo!
 
Prof. Lipumba mwenyekiti wa kamati ya Maprofesa wa uchumi Duniani. Cha kushangaza nchi anayotoka ina hali mbaya kiuchumi. Tunapata tafsiri gani hapa? 1.Tunaenzi zile methali za kiswahili za "kwenye miti hakuna wajenzi na Nabii hakubaliki kwao"? 2. Hatutaki ushauri wake kwa sababu anatoka chama cha upinzani?
 
Prof. Lipumba mwenyekiti wa kamati ya Maprofesa wa uchumi Duniani. Cha kushangaza nchi anayotoka ina hali mbaya kiuchumi. Tunapata tafsiri gani hapa? 1.Tunaenzi zile methali za kiswahili za "kwenye miti hakuna wajenzi na Nabii hakubaliki kwao"? 2. Hatutaki ushauri wake kwa sababu anatoka chama cha upinzani?

Inaonekana yeye ni mtaalamu wa Uchumi wa Developed Countries (Nchi zilizoendelea). Nchi kama yetu (Developing Country), utaalamu hana! Ndiyo maana Rais wa Uganda, Yoweri Museven alidhani angemsaidia lakini alipomchukua kwenda kuwa mshauri wake wa uchumi hakuna alichokifanya zaidi ya Uganda kuendelea kudidimia hadi leo!
 
WanaCUF bwana kwa Propaganda. Ooh watu wengi wamejazana Air Port! Picha hakuna! Jifunzuni kutoka kwetu Arumeru jana. Mkutano unaendelea picha zinarushwa wakati huo huo!

Cuf waache propaganda za kitoto, nimepita hapo airport mida ya saa 5 wala sijaona nyomi yoyote zaidi ya watu wachache tu waliojitokeza. Labda kama sasahivi ndio wamejaa uwanjani, na kama ndivyo basi waweke picha waache longolongo.
 
Uchumi ni uchumi mwana uwe wa developed au wa developing countries!
Issue ni kuwa nabii hakubaliki kwao.
 
Kwani huko alikoenda amelisaidia nini Taifa ili Tukampokee hata kichama sidhani kama hiyo safari ina msaada hadi twende Airport eti tukampokee... NONSENsE!!
 
Back
Top Bottom