Uchaguzi 2020 Uzinduzi wa Kampeni za CUF: Prof. Lipumba asema akishinda Urais atakuwa Rais wa 1 Tanzania kupewa tuzo ya Mo Ibrahim

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
4,457
2,000
Mgombea Urais kupitia CUF, Prof. Ibrahim Lipumba amezindua kampeni za chama hicho Mkoani Mtwara ambapo ameahidi kuboresha Huduma za Afya kwa wajawazito na watoto, kuimarisha Uchumi wa Baharini (Uvuvi), Elimu bora na kuimarisha Soko la Nafaka na Mazao mbalimbali

Prof. Lipumba amesema akichaguliwa yeye atakuwa Rais wa Mfano na ndio atakuwa Rais wa kwanza kutoka Tanzania kupewa Tuzo ya Mo Ibrahim. Anadai yeye ndio Profesa pekee anayetumika hadi Mataifa ya Nje kwenye Masuala ya Uchumi

Ameongeza kuwa Mwaka 2017, zao lililoongoza kwa kuuzwa nje lilikuwa korosho ambapo Tanzania iliuza Dola Mil. 530 lakini 2018 Serikali ya CCM ikafanya mambo yake, mauzo ya korosho yakapungua toka Dola Milioni 530 na kufikia Dola Milioni 110

 

VAPS

JF-Expert Member
Jul 10, 2012
5,542
2,000
Lissu alikuwa anawatetea Mabeberu yaibe madini yetu
Rais Magufuli akatupigania Watanzania
Umesikia mwenyewe aibu Mrejesho makubaliano na Barrick hizo USD300M, mafungu yake kulipwa miaka kadhaa, ambapo Hiyo ni pato la miezi3 pekee kwa uzalishaji kawaida Barrick, hakugusia zile trilliin 400 tzs?// Usd 190 B , tax bill.
 

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
25,333
2,000
..naona TBC wanaendeleza michezo ileile iliyowagombanisha na CDM.

..nadhani hawa ndugu zetu hawaelewi chaguzi na kampeni za vyama vingi vinavyofanyika.

..Nimeona hapo CUF wakitaja mapungufu ya ccm na viongozi wake sauti inakatwa.
 

Ettore Bugatti

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
4,054
2,000
..naona TBC wanaendeleza michezo ileile iliyowagombanisha na CDM.

..nadhani hawa ndugu zetu hawaelewi chaguzi na kampeni za vyama vingi vinavyofanyika.

..Nimeona hapo CUF wakitaja mapungufu ya ccm na viongozi wake sauti inakatwa.
Washaonja nyama ya 'mtu' hao..Hawawezi kuacha huo ushamba wao!

Time will tell.
 

DT125

JF-Expert Member
Oct 19, 2011
336
500
Bora hawa cuf kuliko Chadema wanaotumiwa na mabeberu kuharibu amani ya Nchi yetu
Hivi unadhani bila mabeberu vyama tawala vingetoka madarakani Afrika na Tume zao za uchaguzi zisizo huru. Ukikubalika kwa mabeberu kazi saa nne tu unamaliza.
 

Kinoamiguu

JF-Expert Member
Nov 29, 2018
6,121
2,000
Bora hawa cuf kuliko Chadema wanaotumiwa na mabeberu kuharibu amani ya Nchi yetu
Una amani gani wewe miaka 60 yya uhuru watu wanakunywa maji ya rope?
Serikali baada ya kuwainua wakulima inawapora KOROSHO Zao?
Miaka 5 jitu halijaongeza mishahara linabweka tu na kiswahili kibovu
 

Alvin Slain

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
6,378
2,000
Chadema ndio waasisi matusi majukwaani wanaleta shida

Mimi na familia yangu Siwezi kufungua t.v. niangalie mkutano wa chadema kwani matusi yamewajaa kinywani
Mambo mengine ni asili ya dunia huwezi kuyazuia.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom