MESTOD
JF-Expert Member
- Nov 12, 2010
- 4,798
- 2,010
Hukumbuki wangenga walisema palipo na miti mingi hakuna wajenzi? Kama umewahi kumwona Fundi uashi ana nyumba yake nzuri ujue sio fundi mzuri sana. Vile vile Mafundi seremala wengi hawana fernichers nzuri majumbani mwao. Umeshamwona fundi mshona nguo anavaa nguo bomba? Ukimwona basi huyo ni msimamizi tu sio fundi cherehani. Je, Umeona wapi Askofu watoto wake wakawa na tabia nzuri sana? Ulizia kama utakuta watoto wengi wa walimu wana akili sana. Only the exceptions which however, are very few!!!!
Tanzania imelaaniwa laana ambayo kina Mwakasege wanapigia kelele kila siku ili kuikemea ishindwe na kulegea ktk JINA KUBWA KABISA la YESU KRISTO, lakini laana hiyo haitoki kirahisi sababu wanaowazunguka katika maombi hayo nao wametingwa na dhambi kibao hata zinawasuta wakati wa maombi na hatimaye maombi yanazuiwa kufika JUU mbele ya Muumba, Kanchi katajiri sana lakini kananuka umaskini sababu wapo watu wanatambika sana kujilimbikizia utajiri kwa kuweka misukule kwenye ofisi zao, vitega uchumi vyao, uongozi wao......hata wengine huua watoto wao ili watajirike upesi lakini hawadumu sana, wenzao wanaobaki wala hawaoni hayo maana shetani anawasahaulisha. Hii ni vita ya kiroho. Bila kujali dini gani ni lazima watanzania wote tuamke, tutubu na kutakasika na ndipo tumwombe Mungu atuonee huruma. Hatupigani lakini nchi zinazopigana zinapaa kiuchumi. Sisi tunawaita wageni waje wale, wanye waondoke na kila wanachokitaka kutoka kwetu, nasi wanaturushia sumni kama vile makonda wanavyowafanyia wapigadebe, halafu tunafuraaaaaahi ajabu. Kama sio laana ni nini hiyo. Unaweza kuiona vizuri Tanzania ukitoka nje kidogo tu, itazame kutoka kule ndo utajua laaana hapa ndio amri ya kila siku tunaitumikia.
Aaghrrrr!!!
Message sent and delivered, I am not sure it is read. kila munu abena kwabo. Tusali sana sio mchezo, tena kwa kumaanisha.
Umeongea vema.
Laana ya nchi hii ina mizizi mirefu sana.
Kama Mungu alivosema ktk kitabu cha mwanzo,
Tusipotubu sasa, atapatiliza maovu yetu hadi kizazi cha tatu na cha nne.
Ee Mwenyezi Mungu,
Uturehemu na Laana ya nchi yetu.