Ninawaza ya kwamba uwamu hii ya sasa ya uongozi na hao mabeberu nikitu kimoja.
Na uongozi huu ndio kete yao ya mwisho katika kuhakikisha wanashinda/wanafanikisha mipango yao...
Ndio maana viongozi hawawajibiki hata iweje kwa makosa yote waliyoyafanya licha ya kua wananchi, na baadhi ya taasisi kutokuwaunga mkono.
Mabeberu wanahakikisha haachi madaraka hata apoteze vipi sifa za kua kiongozi, kwasababu akiachia tu nchi hata mipango yao itakuwa imefia hapo ndio maana waliforce uchaguzi, maandamano yalishauondolea sifa, na utekaji pia uliuondolea sifa, watu waaina mbalimbali wamepiga kelele lakini lakini bado upo... Jiulize kwanini? Je kwa yote yaliyotokea nchini uraisi unamaslahi gani?
Kama ni uzalendo na wanaona taifa linaendelea kuharibika likiwa mikononi mwao kwasababu watu wao hawaukubali uongozi si wangewaachia wengine wanaokubalika ili kulinda amani ya nchi tunayoihubili kila siku.
Aidha wanajua au hawajui...
Kama wanajua... inaonekana kuna watu au mtu anayewashawishi/mshawishi raisi na kumhakikisha kua mambo yako shwari na hawezi kufika pabaya kwasababu anajua buckup iliyopo nyuma yake.
Na kama hawajui/hajui basi ni kwamba wanachezewa mchezo wa ki-intellijensia... Wao/Yeye hajui kinachoendelea. Ila kuna mtu/mshauri nyuma yao/yake ambaye anapokea maagizo kutoka kwa mabeberu na anajua mpango mzima, hivyo anakua anaongoza hatua kwa hatua nini chakufanya... Na wanafanyiwa hayo pasipo wao/yeye kujua kua wanacheza na tune za mabeberu.
Na kinachoendelea kwa hao kina ICC, EU, CNN, MANGE na wengineo ni drama za ki-intellijensia na mwisho wa siku hakuna atakae fungwa... Yaani hapa mabeberu wanajipiga na kulia wenyewe.
Kama hatima ya kurupshani zote hizi ni njema kwa taifa basi sio tatizo na wala hao mabeberu sio maadui, tofauti na hapo basi ni wakuwaogopa kama ukoma.
Nasisitiza tushilikiane tufungamane na yeyote.
TUSIWE WA UPANDE WOWOTE NA TUSICHAGUE UPANDE WOWOTE BALI TUWE /TUFUNGAMANE NA UPANDE WOTE.
GRANDY STRATEGY.
Yaani kila atakaekua tayari kushirikiana na sisi basi kusiwe na sheria yoyote ya kutuzuia kufanya hivyo na kila tutakayemtaka basi vivyo hivyo asiwepo yeyote wa kutuzuia.
Nchi ipitie vizuri sheria na vipaumbele vyake kisha iboreshe Nchi iwe katika position ya katikati World Free Trade Center/zone (WFTC).