Baadhi yetu wana JF tuliokutana msibani leo katika Ibada pale Kanisa katoliki Segerea, tumeamua kwamba tutapanga siku maalumu hivi karibuni na tutakutana British Council na kujadili yale yote aliyosimamia Regia na nini cha kufanya ikiwa ni namna ya JF kumuenzi marehemu. Yote tutayajulisha maana tutashirikiana na uongozi wa JF.
Mimi si mwandikaji sana, lakini leo wacha niandike machache.Machache haya ninayoweza kusema ni kuwa, Mwaka 2010 tulipoendesha shindano la "JF Woman of the Year 2010" Regia alichaguliwa na Wana JF na akashinda. Hii ni uthibitisho tosha kuwa Regia alikuwa anapendwa, anathaminiwa na anakubalika katika hoja zake. Ni Regia huyu huyu aliyethubutu kuweka pembeni ID yake ya JF ya "Gender Sensitive" na kutumia jina lake halisi Regia Mtema! Ni wachache sana wanaweza na wanaojiamini kwa hilo.
Lakini kikubwa na ambacho wengi hamjui ni kuwa, katika Mwaka wa uchaguzi 2010 JF ilijizolea umaarufu sana toka ndani na nje ya Nchi katika kutoa habari za uchaguzi mkuu. Binafsi niliendesha threads kuu kama za Uzinduzi wa Kampeni wa Chadema jangwani, Uzinduzi wa Kampeni wa CCM ambayo yote ilifanyikia jangwani. Reporting ile ilikuwa ni LIVE nikiaangalia TV, kusikiliza na hatimaye kuandika kadiri nilvyoona katika Luninga na huku napost JF. Hii ilifanya baadhi wakaniita "Mzee wa Matukio"
Wakati wa Uzinduzi wa Kampeni wa CHADEMA wote mnajua kuwa Matangazo yalikatishwa na TBC. Ni katika kipindi hiki nilianza kuhaha ni vipi sasa nitawaletea wadau matangazo live. Unajua kipindi kile kulikuwa na watu wengi sana online. Na wengi walisononeka. Niliwasiliana na Maxence (Founder wa JF) na kumuuliza kama kuna mtu yeyote anaweza akanisaidia kupost live ambaye yuko jangwani.
Maxence alinipata namba ya simu ya Regia, akaniambia yuko Jangwani na atakupa updates zote. Huo ndiyo ukawa Mwanzo wa Mimi na Regia kufahamiana. Mwanzoni nilimjua tu kama Gender Sensitive na Baadaye Regia Mtema.
Naam . . . Nilipompigia Regia akaniambia kuwa haina tabu, yeye atanipa updates kwa simu, naam, hatukukata simu, Yeye akieleza matukio na hotuba nami pia nikisikiliza kwa mbali na wakati huo huo nikipost JF. Huyo ndiye Regia ninayemfahamu ambaye alikuwa tayari wakati wowote kufanya kile anachokiamini na kukusimamia. Ulemavu wake wa mguu kweke yeye haukuwa na nafasi ya kumnyima fursa yoyote au kufanya jambo lolote alilitaka. Wakati mwingi aliwazidi hata wasio na ulemavu wowote.
Niliposikia msiba huu, niliumia. Na leo sikuwa na jinsi, ilibidi nisitishe kila kitu na kwenda kumwaga Mwanamapinduzi huyu, naamu, Kumwanga Regia.
Kwa heri Kamanda Regia, kalale pema peponi Kamanda, umefanya sehemu yako. Inatupasa na sisi tufanye sehemu yetu na kuiga na kuendeleza mazuri yote aliyoyafanya.
Regia, wewe ni kama Mshumaa uliokuwa unaleta Mwanga wa matumaini katika kiza kinene sana na sasa Mshumaa huo umepulizwa na upepo na kuzima.
Regia, yo are a Tanzanian Rose & Gold, you are like Candle in the wind.
We will miss you Regia. You were the JF icon.
Kalale pema peponi Kamanda
Amen.