Picha: Ibada ya kumuaga Regia Mtema iliyofanyika Tabata

Duh...RIP Regia.
Hizi picha za ndani ya jeneza zingetolewa. Sioni sababu ya kuweka picha kama hizi hata kidogo.
 
R.I.P Regia Kifo chake kimekuwa ni pigo kuu kwa taifa letu na hata hapa Jamii forums Michango yake kwetu sisi Wa Tanzania ilikuwa ni muhimu sana R.I.P Regia umetuacha na majonzi Makuu na ni pengo kuu halitozibika kwa haraka, Mwenyeezi Mungu akusamehe makosa yako na akupeleke peponi ameen.
 
Pumzika dada, mpiganaji wa haki zangu, mfano thabiti hasa kwa vijana, kiongozi shupavu, mwana demokrasia wa kweli, kwaheri dada!
 
Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi amen Ingawa tuko mbali lakini tuko nanyi katika sala
 
=The Finest;3147332]Wakuu hizi ndio picha nilizoweza kupiga kwenye Ibada ya kumuombea Regia Mtema iliyofanyika Kanisa Katoliki Tabata

jeneza.jpg


mapadre-askofu.jpg

Asante kwa taswiras ulizotuwekea, next time jaribu kuweka kidogo na introduction ya kutujuza ibada iliongozwa na nani na mengine macheche yaliyojilia. Thanks.
 
Nitamiss mawazo yote ya Regia, Nitamiss post zote za Regia, na mbaya zaidi nitammiss Regia.

Ingawa sikuweza kushiriki mazishi na huenda sitaweza kushiriki mkutano wa British Council kutokana na timing ambayo inaweza kukorofishana na mambo mengine ambayo yananisonga siku hiyo, nitafuatilia kwa makini maendeleo ya maombolezo na nitashiriki maombolezo hayo kikamilifu hapa pangoni kwangu. Hata hivyo iwapo litazuka wazo lolote la kuweka memorial structure ya aina yoyote kumkumbuka Regia, niko tayari kushiriki kikamilifu kufanikisha wazo hilo; kwa mfano kujenga mnara kwenye kaburi lake au kujenga mnara pale alipopotezea uhai wake au wazo lolote la namna hiyo.

Regia alikuwa kijana wa shoka sana ambaye tumempoteza mapema mno: matunda mazuri huwa hayadumu tawini kwa muda mrefu.
 
Ahsante mkuu kwa picha, ninafarijika sana kuona wana jf tunavyokuwa kitu kimoja.., ulale mahari pema peponi dada yangu mpendwa regia mtema.
 
This is yet another painful and worst experience of how road accidents claim people's lives.
Mungu ibariki Tanzania.
 
Asante saana Finest kwa kutufikisha ambako tulikosa. Poleni na shughuli zoote. Pamoja saana.
 
Asante kwa taswiras ulizotuwekea, next time jaribu kuweka kidogo na introduction ya kutujuza ibada iliongozwa na nani na mengine macheche yaliyojilia. Thanks.


Huyo wa katikati ni Askofu msaidizi wa jimbo kuu la DSM Mhashamu Baba Askofu Sartarius Libena ambaye sasa ameteuliwa kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo jipya Katoliki la Ifakara (huyu ndiye aliyeoongoza Misa ya Mazishi). Kushoto kwake ni Msinyori Deogratius Mbiku (Alikuwa Paroko wa Parokia ya Chuo Kikuu-Dar). Huyo wa upande wa kulia bila shaka ni Paroko wa Parokia ya Segerea.
 
Back
Top Bottom