Picha: Angalia jinsi daladala wanavyojiongeza na level seats

Sawa sawa kabisa, ustaarabu unaanza kurudi kwenye usafiri wa daladala, hakuna tena zile za makonda kulazimisha watu wageukiane migongo na ukiwa umekaa siti ya nyuma hadi ufike mlangoni kushuka inakuwaga mtihani
 
Sio kila kitu cha kuponda ndugu Zanguni
Gari zinazo kuja kutoka Japan Au Dubai zinakuja ziko katika mfumo huu apo chini
Wanavitoa hvyo viti ili wajaze Nyomi Maana wanao simama ni weng kuliko
.
Mnavyoponda huo Mfumo wa Vigoda Mna Maana gani ? Maana hao wamekosa Siti Special waweka vigoda shida iko wapi ?
.
Hatukatai hata hiyo Level Seat bado Maambukizi yako pale pale Lkn at least kuliko Kusimamisha ile ni Hatari zaidi, kwa tunao Panda daladala tuwanaelewa vizuri
IMG-20200404-WA0005.jpeg
IMG-20200404-WA0004.jpeg
 
Mkuu ww ndo hujatafakari vzr kuhusu kauli ya serekali kwa daladala, ni hivii... Ile seat ya nyuma huwa wanakaa watu 5. ( Haijakatazwa) sasa kuna ubaya gani hizi seati nyingine zikiunganisha katikati na watu waka kaa watano!!?

Kama ingekuwa shida ni msongamano hata seat inayokaliwa na watu wawili bado watakuwa wamebanana!

Ukiangalia nafasi inayotakiwa kuachwa kati ya mtu na mtu kwa ( kujikinga na corona) kwa gari kama coaster labda wangepanda abiria 9 tu na dereva awe wa 10.

Waendesha daladala wameji0ngeza vzr!

Sent using Jamii Forums mobile app
Chamsingi tungeongeza nauli kutoka mianne Hadi elfu moja tukaruhusu mabus makubwa Kama youtong kubeba abiria mijini,
 
U
Kilichofanywa ni kupunguza Msongamano sio kuongeza
Hivi huoni watu wanao simama wako kwenye hatari zaidi kuliko waliokaa?
Uko sawa kabisa, mie nimevaa shati jirani yangu kavaa Dera xitagusana nguo tu na akipiga chafya unakutana na mask huku haraka natoa sanitizer kujifukiza mwili
 
Corona ikichanganya bongo hakuna wa kupona.

.......Tuombe Mungu huu ugonjwa usishike kasi hapa kwetu akili zetu ndogo sana.
 
Min bus zote huwa zinakuja na seat ya kukunjua katikati ila wamiliki huwa wanazitoa ili kulq vichwa vingi kwa kusimamisha abiria so hapo hyo picha iwangu hakuna cha ajabu hapo mana zipo coaster za mkoa zina siti kati

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hilo nalo ni kosa, lengo ni kudhibiti msongomano na sio kuzuia watu kusimama. Ikiwezekana hata hiyo siti ya watu wawili akae mmoja..kwa kwenye mstari mmoja akae mwisho kushoto na mwisho kulia..

Kwa walichofanya bado tatizo litakuwepo palepale tu..
 
Usionyeshe upoyoyo wako hadharani namna hii basi. Mpaka anayesoma anaona aibu kama ndiye aliyeandika ujinga kama huu!
Sasa walivyofanya hivyo kuna tofauti gani na zile seat za kukunjua zinazokua katikati.
Mambo mengine tujadili kwa upana wake. Jiweke kwenye viatu vya hawa makondakta utajua ni kwanini wanafanya hivyo. Usibwabwaje tu humu.
 
Sasa walivyofanya hivyo kuna tofauti gani na zile seat za kukunjua zinazokua katikati.
Mambo mengine tujadili kwa upana wake. Jiweke kwenye viatu vya hawa makondakta utajua ni kwanini wanafanya hivyo. Usibwabwaje tu humu.
Kwanini unajifanya kama huna akili? Unajua ni kwanini wamesema watu wasisimame? Nia ni kupunguza mlundikano wa watu i.e. kupunguza idadi ya watu kwenye daladala ili kupunguza uwezekano wa maambukizi.
 
Back
Top Bottom