Picha: Angalia jinsi daladala wanavyojiongeza na level seats

Katika harakati hizi za kukabiliana na gonjwa la Corona tulionywa na mamlaka ya nchi juu ya kujilinda ikiwa ni pamoja na kukaa mbali kati ya mtu na mtu (social distance).

Pia mamlaka kama SUMATRA walitoa angalizo Kwenye vyombo vyote vya usafiri abiria wote wakae Kwenye viti na asiwepo mtu wa kusimama na kushikilia bomba lakini cha kushangaza na kusikitisha bado kuna baadhi ya waendesha daladala wameendelea kukaidi.

Daladala nyingi za Buza - Chamazi, Kongowe na Vikindu wamebuni njia rahisi ya kuchonga mabenchi madogo yenye urefu wa futi 1.5 ambapo huwekwa Kati ili kufidia abiria waliokuwa wanasimama kabla ya kupigwa marufuku.

Watu wa Usalama Barabarani waangalie hili TATIZO Kwenye daladala maana makondakta wameshajiongeza Kwa kufanya jeuri tena

View attachment 1408618View attachment 1408619
Safi sasa ule umbali wa mita moja sijui hapo ukoje jamani.
 
Back
Top Bottom