Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,989
Akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya DART Mkuu wa kitengo Cha Mawasiliano na Uhusiano Kwa Umma DART William Gatambi amesema upanuzi wa kituo Cha mabasi yaendayo haraka kivukoni,Ujenzi unaotarajiwa kuanza mwezi huu wa 10
Amesema kuanzia tarehe 21 mwezi huu daladala hazitaruhusiwa kukitumika kituo hicho na badala yake daladala zilizokuwa zinatoa huduma kwenye kituo Cha Kivukoni zitatumia vituo mbadala vitatu ikiwemo pembezoni mwa Wizara ya Ardhi,PPF Tower na Posta ya zamani
Amesema kuwa waendesha bajaji wao wataendelea kufika eneo la Kivukoni kwa sababu wao hupaki bajaji zao kandokando ya barabara hivyo haziwezi kuathiri zoezi hilo la ujenzi.
Afisa Mfawidhi mamlaka ya Udhibiti wa usafiri Ardhini LATRA Mkoa wa Dar es salaam Rahim Kondo amewataka Wamiliki na watoa huduma kuzingatia ruti katika vituo mbadala vilivyoelekezwa kinyume chake watakumbana na mkono wa sheria hivyo ni muhimu wakazingatia tangazo ililotolewa ili kuepuka usumbufu watakaokumbana nao endapo watakaidi agizo hilo
Hatua ya Upanuzi wa kituo hicho Cha mabasi yaendayo haraka Cha kivukon mara kitakapokalimika kitakuwa nanuwezo wa kupokea mabasi hayo kutoka kwenye ruti za mbagala, Gongolamboto na Tegeta
Ifahamike kuwa kituo Cha mbadala pembeni mwa Wizara ya Ardhi kitahudumia daladala za Kigogo Sokoni,Buyuni Chanika,Machinga Complex na Tabata Chang’ombe Aidha kituo Cha PPF Tower kitahudumia daladala za Tegeta na Gongolamboto na kituo Cha posta ya zamani kitahudumia daladala za Kivule,Kisemvule,Tegeta,Kinyerezi na Mbande.
Vituo vingine ni pamoja na eneo karibu na Benki ya NBC (Posta ya Zamani) kwa wanaoelekea Kisemvule, Kivule Sokoni, Mbande Kisewe, kupitia Barabara ya Kilwa, Nyerere na Uhuru.
Na Kituo cha Mwisho ni eneo lililopo kwenye Mtaa wa Ohio kwa wanaoelekea Gongolamboto na Tegeta Nyuki kupitia Barabara ya Nyerere, Uhuru na Ali Hassan Mwinyi.