Hii daladala inalazimisha wanafunzi wawe na Tsh. 200 kamili, zaidi ya hiyo hawarudishiwi chenji

Isaya wa njombe

Senior Member
Apr 2, 2023
181
325
Habari za asubuhi,

Kiukweli leo asubuhi tar 20/3/2024 nilitoka Mabibo kuelekea Muhimbili kwa usafiri wa daladala, tulipofika hapa Kigogo Roundabout ya Ilala na Magomeni, kuna mwanafunzi alishuka ni mdogo miaka kama 6 au 7 alimpa kondaka nadhani miaka 500/=. Kumbe makondakta wanataka uingie ukiwa na miambili kamili. Yule kondakta akamwambia huwa tunawaambia muwe na chenji kamili akagoma kumrudishia

Kelele kale katoto ni kabinti kamemlilia konda, jamaa akaingia kwenye gari dereva naye haraka amewasha gari na kuondoka. Tulipiga kelele na kumlaumu kondakta asimamishe akate nauli zetu ikawa hakuna namna

Binafsi ingelikuwa ni mtu mzima kwangu haikuwa shida sana ila kwa mwanafunzi tena Binti mdogo nadhani darasa la kwanza nimeumia sana

Gari ni ya Mabibo to Muhimbili na nimepga picha namba ya gari hapo chini na nipo tayari kwa ushahidi kama watagoma.

Daladala.png
 
Ila kuna watu wana roho za kikatili. Ukute maskini ya Mungu ndio nauli yake ya kurudia nyumbani.

Wazazi tunapaswa kuzingatia umbali wa shule tunazapoleka watoto wetu tukizingatia umri wa mtoto na changamoto za usafiri.
Binti wa miaka 6 kugombania madadala sio sahihi kabisa.
 
Kuumia kwako ni upumbavu kama ulishindwa kuchukua hatua papo hapo....na hiyo ndio shida ya watanzania......wao kazi Yao kuandika tu nimeumia........

Ina maana wewe umeshindwa kusimama kidete kumuamuru huyo konda kurudisha chenchi ya huyo binti.......

Sasa malalamiko haya yanamsaidia nini huyo mtoto.......

Mimi binafsi siwezi kuona mtu anaonewa nikaangalia achilia mbali malaika kama huyo.....
 
Kuna mazingira mengine ni ngumu kuchukua hatua kwa kuzingatia mambo kadhaa;

1. Inapaswa ujiweze kiubavu pale mambo yakienda kombo katika process ya kudai haki. Hakuna fedheha mbaya kama kudundwa ukiwa unatetea.

2. Kwa desturi ya wabongo usishangae ukalaumiwa wewe na abiria wenzio pale mzozo utakapoanza na gari kuchelewa kuondoka. Watanzania tuna itikadi ya kusema kama haliniathiri basi halinihusu.

3. Kunaweza kutokea upotevu wa pesa katika vurumai ukaishia kupata deni njaa.

Inawezekana alichofanya mtoa mada kisiwe na msaada wa moja kwa moja kwa binti husika lakini endapo mamlaka husika itachukua hatua (japo nina shaka kubwa juu ya hili) itakuwa funzo kwa wenye tabia kama za huyo konda hivyo kunusuru watoto wengine dhidi ya dhulma na manyanyaso.
 
Hawa makondakta Ni wajinga Sana siku hizi umekuwa kama utaratibu mwanafunzi asipokuwa na chenji kamili mtoto Ni ataambiwa maneno yote mabaya na konda minkuna mmoja dogo alikuwa na shilingi mia tano akaanza kumtukana ilibidi niingilie Kati ukawa ugomvi wa Mimi na kondakta nikampa makavu yake mwisho abiria nao wakaliunga ikabidi awe mpole .yaani akili zao utafikiri wao hawana watoto na hawatazaa
 
Kuumia kwako ni upumbavu kama ulishindwa kuchukua hatua papo hapo....na hiyo ndio shida ya watanzania......wao kazi Yao kuandika tu nimeumia........

Ina maana wewe umeshindwa kusimama kidete kumuamuru huyo konda kurudisha chenchi ya huyo binti.......

Sasa malalamiko haya yanamsaidia nini huyo mtoto.......

Mimi binafsi siwezi kuona mtu anaonewa nikaangalia achilia mbali malaika kama huyo.....
Safi sana mkuu umejibia hoja hii vema,watanzania hasa hawa middle class ni waoga wa kutake action,waoga wa push back na mashujaa wa kulalama humu,why wewe mtoa hoja hukusimama kidete kupinga unyanyasaji huu wa mtoto huyu,why hukujitolea na kumwambia konda kurudisha ile 500 tsh.halafu wewe umpe konda?,konda mmoja anasumbua wanaume zaidi ya 10 waliokuwemo kwenye daladala hiyo,sasa umetuwekea picha ya daladala ili iweje?
 
Kuna mazingira mengine ni ngumu kuchukua hatua kwa kuzingatia mambo kadhaa;

1. Inapaswa ujiweze kiubavu pale mambo yakienda kombo katika process ya kudai haki. Hakuna fedheha mbaya kama kudundwa ukiwa unatetea.

2. Kwa desturi ya wabongo usishangae ukalaumiwa wewe na abiria wenzio pale mzozo utakapoanza na gari kuchelewa kuondoka. Watanzania tuna itikadi ya kusema kama haliniathiri basi halinihusu.

3. Kunaweza kutokea upotevu wa pesa katika vurumai ukaishia kupata deni njaa.

Inawezekana alichofanya mtoa mada kisiwe na msaada wa moja kwa moja kwa binti husika lakini endapo mamlaka husika itachukua hatua (japo nina shaka kubwa juu ya hili) itakuwa funzo kwa watoto wengine kuwa wahanga wa jambo kama hili.
Nimekuelewa lakini kwa uzoefu wangu kwenye matukio hayo ni kuwa konda na dereva wake wasingekubali mzozo mkubwa Kwa ajili ya 500/=

Nilishawahi kupambana na tukio kama hilo kwenye daladala za mwenge na nikashinda......yeye ilikuwa 10,000/= mida ya asubuhi........mara nyingi huwa wanatingisha kiberiti.......

Wewe usimvae mwili simama kwenye agenda yako tu huku ukipaza sauti kupata zaidi attention za watu.....ni jambo jepesi sana kama ukiamua
 
Safi sana mkuu umejibia hoja hii vema,watanzania hasa hawa middle class ni waoga wa kutake action,waoga wa push back na mashujaa wa kulalama humu,why wewe mtoa hoja hukusimama kidete kupinga unyanyasaji huu wa mtoto huyu,why hukujitolea na kumwambia konda kurudisha ile 500 tsh.halafu wewe umpe konda?,konda mmoja anasumbua wanaume zaidi ya 10 waliokuwemo kwenye daladala hiyo,sasa umetuwekea picha ya daladala ili iweje?
Watanzania ni mabingwa kuongea, kuandika, kulalamika na kunungunika lakini sio kuchukua hatua........
 
Back
Top Bottom