Kero ya kubadili njia "Route" kwa mabasi ya usafiri (daladala) ya Buza to Kawe

Anti-Hacker

JF-Expert Member
Oct 1, 2018
804
1,231
Habari zenu wapendwa na Moderators.

Ni kitambo sana sijaaandika kitu humu jamii forums, ila leo nimeamua kuandika hii kero ambayo imenikumba mara kadhaa.

Ninaomba, hii taarifa iwafikie LATRA, SUMATRA CC, na Jeshi la Police Tanzania kitengo cha usalama barabarani, pia iwafikie umoja wa Makondakta na umoja wa wamiliki wa daladala.

Kwanza nianze kwa kutoa Anagalizo au
🇩 🇮 🇸 🇨 🇱 🇦 🇮 🇲 🇪 🇷

"Taarifa zote nitakazo toa humu ni 100% kweli, sina nia wala dhumuni baya la kuchafua Biashara wala mmiliki wa daladala ambayo nitaitumia kama mfano, pia sina lengo la kufungua mashtaka kwa mhusika wala wahusika, ila ninaomba nipate ufafanuzi na wahusika pia waweze kufuatiria hili nitakaro lisema."

Kiapo:
"Mimi Anti-Hacker, ninaapa kwa jina la Nchi ya Tanzania, kua Taarifa zote nitakazo zitoa ni sahihi na nilizopitia Mwenyewe, sijaambiwa wala kuagizwa na mtu wala kikundi chochote kile, nipo radhi kwa nitakao wakosea."

KERO.
Sijajua ni kwanini au nini Chanzo ila nimekuja kugundua kua kila ifikapo jioni haswa siku za mikutano ya mwaposa, Daladala za kutoka Kawe kwenda Buza, huua Route, au huvunja njia kwa kufupisha route..yaani badala ya daladala kwenda moja kwa moja Buza, kondacta hutamka Buguruni, Buguruni, ilala boma buguruni.
Hii inawafanya abiria wote wakose alternative au mbadara na kupanda daladala hiyo na kuishia buguruni, na wamekua wanafanga hii tabia, na wakishafika buguruni sheli, au sokoni au rozana husema ndio mwisho wao na kuamuru abiria woye washuke chini kwani wanaenda kulaza gari.

Lahasha, wakishahakikisha wameshuka husubiri kwa dakika 3-5, na kueasha gari moja kwa moja kwenda kwenye kituo cha daladala cha buguruni kuelekea tazara, gongo la mboyo, au uhasibu, temeke na meneo jirani.

Hufanya hivi na kupata abilia wapya, na hivyo kujioatia pesa zaidi kuliko mwanzo..

Hii inafanya abilia kutoka kawe kwenda buza kulipa 1000 Tzs, hadi 1100 Tzs(500 kutoka kawe to buguruni, na 500/600 kutoka buguruni hadi buza), Badara ya kulipia Tsh.750 tu ya awali kama angepata daladala ya moja kwa moja.

Mtu anaweza sema ni hela ndogo, laah hasha hapo mtu amepoteza shillingi 250 hadi 350, ambayo kama ukizani ndogo nenda Benki yoyote ile na 99750, na useme ni imepelea 250 ifike 100000..

Nimeamua kuandika hili, ili watu na jamii na viongozi wahusika wasikie, kwani mnamo tarehe 01/12/2023
Nilikutana na hiyo kharaha, ijapokua nilikutano nayo mara 5 hadi sita nyuma . Ila hii siku ilikua tofauti, kwani kuna mama mmoja aliongea kauli ambayo iliniumiza mimi kama kijana na mmoja wa majobless na mpambanaji..

Taarifa sahihi.

Ilikua tarehe 01/12/2023 mida ya saa 20:10-22, nilikua nipo maeneo ya mikocheni chama, kwa kituo cha daladala jirani na TANESCO, ndipo ilikuja daladala yenye number ya usajiri
T 540 DQH, iliyoandikwa BUZA - KAWE
via Usalama road na UHURU road,
ikiwa na mistari ya rangi ya kijani, njano na zambarau. Iliyopita katikati mwa Daladala.

Nilipanda daladala na kuendelea na safari kama kawaida, nilisimama mpaka tulipofika magomeni, ambako nilioata nafasi ya kukaa kwenye siti usawa wa mlango upande wa dereva.

Mda wite sikua maanani na kondakta wala abiria yeyote zaidi nakumbuka nilimuona kondakta akiwa anatoa sarafu nyingi kwenye mfuko wa nyuma wa suruali hake na kuweka kwenye mfuko wa blue(hizi mbadala wa plastiki)

Heka heka.

Baada ya kufika Buguruni rozana, kondakta ndipo alianza heka heka za kusema anaishia Buguruni na kufunga au kwenda kukaza gari .

Na tulivyofika buguruni sokoni alisema tushuke wote, mimi kwakua nilikua nimelala na najua hii tabia niliweka mgomo kidogo, na mbele yangu alikua mama mmoja ambaye alionekana kachanganyikiwa baada ya kuambia hivyo..

Niligoma na yule mama aliomba sana , lakini kondakta ambaye sasa nilikua nishaanza kumuwekea maanani, na kijana mwingine ambaye alikua amekaa mbele pembeni ya dereve pamoja na dereva walisisitiza kua tushuke kwani wanaishia hapo.

Mimi nilimfata kondakta na kumwambia najua wanaendekea na safari lakini kondacta, alikataa na kuanza kusema anafunga vioi vya gari ili akalaze gari..

Yule mama aliwaomba kwakua mkononi alikua kabakia na 1300 tu, kwani hiyo 1000 angetumia mbele kwenye bodaboda ya kwenda kwake akifika buza.

Nakumbuka niliwaomba sana, walikataa kabisa na kusema wanaishia hapo( ikimbukwe hii tabia nishakutana nayo mra 5 nyuma, na mara zote hua watu wakishuka wengi tukiobakia hua tuanendelea mpaka kwenye kituo cha daladala cha buguruni kuelekea temeke, gongolamboto, temeke na mbagala.

Nakumbuka mda nashuka ilikua saa 09:32.

Na niliamua kuifutalia ile daladala, na kuona wtafanyaje,
Kama kawaida yao, walisubiri na kuangakia hatupo, na kuanza kuja kwenye kituo .

Na baada ya kufika kituoninkama kawaida wakaanza kutangaza wanaelekea buza kanisani kupitia maghorofani, mwembe yanga.

Nakumbuka Kondakta alikua amevaa Tshirt Nyekundu , imeandikwa Standard Charter CHAFU CHAFU.

DEREVA: alikua kavaa jersey yaan united ya red and white color mixer na alikua amevaa kofia.

Na nfani ya daladala kulikus kunapigwa nyimbo za singeli tu.

Safari ya kutoka buguruni, tumetoka saa 9:39.

Bakhera(Tazara) tulipita saa 09:44,

Veterinari tulipiga saa 09:46 kwenye late seconds.

Mwembe yanga saa 09:50-52

Na Mtaa wa Tandika kitanda tulifika saa 09:59.

Niliamua kufutilia muda wa kila kituo ili kama kuna kitu kitakua au kufutilia basi, waangalie usahihi wa mda wangu.

Pia, ninaomba Ndugu wahusika walitazame hili kwa jicho la kioekee maana linatuumiza na kuongeza gharama za maisha, hebu fikiria kama mimi kijana nitkua nasafiri kila siku kutoka kawe jioni kuja buza/temeke tandika itanibidi niunganishe gari mara mbili na kuka loss ya 250, ambayo hata latra hawafaham , kwa week nitakua nimepoteza 1750, kwa mwezi ni 7000.

Ambayo ingeweza nisaidiankwa matumizi yangu mengine ya kimaendeleo, inawezekana inaonekana ni ndogo, ila kama itatukuta watu 10, ni 70000.

Nitaomba samahani kwa popote nilipokosea kwenye kuandika ("typing").

Ila ninaomba Sana , Wahusika wafutilie hii tabia ya makondakta kuua Route.

Asanteni
 
Me naona wako sawa kutoka kawe mpaka buza unalipa 500 ama 600 ni pesa ndogo sana kuna zaidi ya km 20 na mafoleni yote ayo ingefaa mlipe 2000
 
Back
Top Bottom