GE2025 Peter Msigwa ashindwa kura za maoni Iringa Mjini

GE2025 Peter Msigwa ashindwa kura za maoni Iringa Mjini

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Alipokwenda Mbweni na kushauriwa na johnthebaptist agombee ubunge kupitia CCM hapa Iringa mjini, Peter Msigwa alidhani CCM wanampenda kumbe wanamtega..

Matokeo ya awali yanaonesha Msigwa hayumo kati ya wagombea watatu wa juu. Taarifa toka ndani ya CCM hapa mjini inaonesha Msigwa hawezi kuongoza au kuwa wa pili.

Nitakuwa naweka matokeo ya hapa mjini kwa kadri nitakavyokuwa nayapata.

Hivi kweli Msigwa ni wa kuiita CHADEMA ni mama wa Kambo?

MATOKEO RASMI

1. FADHILI NGAJILO. 1,899

2. MOSES AMBINDWILE 1,523

3. PETER MSIGWA 477

4. JESCA MSAMBATAVANGU 408

5. NGUVU CHENGULA 181

6. ISLAM HUWEL 136

View attachment 3431505
Anaenda ACT/CHAUMA kishakuwa malaya wa kiasiasa uzuri ndio siasa haina rafiki wala adui wa kudumu.
 
Mkuu, kura za maoni za udiwani kata za mjini hapo zinasomaje?
Nadhani watu wapya wameshinda na kushindwa. Lakini sidhani kama wengi wa hao wapya ni bora kuliko wa zamani ingawa ule upya wao ndiyo utofauti wenyewe.
 
Ajabu huyu ni mtu alieshinda 2015 akakatwa kutokana na sakata la Lowassa (alikuwa kwenye hiyo team).

Karudi 2020 CCM wakasemehe maisha yaendelee akapata ushindi wa kishindo. Ndio nashangaa nini kimebadilika maana kama kuanguka sio kwa haraka hivyo hasa kwa mmbunge anaetetea jimbo kupata kura tatu kata zingine.

Wahehe sio watu kwakweli kwa jinsi walivyomgeuka mwenzao haraka hivyo.
Ndo kilichotokea kwa masele shinyanga mpaka najiuliza kashidwa vipi?
 
Haaahaa jesca kaachwa mbali

Back
Top Bottom