Nsanzagee
JF-Expert Member
- Jun 28, 2023
- 1,939
- 4,122
Wanajamvi na watanzania kwa ujumla, hasa wafanya kazi wa serikali!
Ninachokiañdika hapa, bila shaka ni hitaji la kila mfanyakazi,
Mimi nikiwa kama mkulima wa hapa nanjilinji, nimechoshwa na kukopwakopwa na wafanyakazi wa umma hasa mwishoni mwa mwaka
Mpaka naandika hivi, nimeanza kuwaonea huruma wafanya kazi wa serikali, maana kila inapofika mwisho wa mwaka, simu zinakuwa nyingi na kila mmoja akiomba mkopo kwa ajili ya kukimu mahitaji yake yanayokuwa yanalundikana kutokana na uhalisia wa mambo mwisho wa mwaka
Mshahara ni uleule, halafu unamlazimu kuugawa karibu mara nne kiasi ambacho haukidhi mahitaji hayo
Utakuta hapohapo kuna sikukuu mbili nazo ni mhimu kuzisherehekea kwa sababu ya umuhimu wake na maisha yetu yalivyo mafupi, haiwezekani kujinyima useme watoto wasile pilau!
Wakati huo huo, itabidi aweke salio lingine kwa ajili ya Ada za watoto na mahitaji yao ya lazima kuelekea shule kufunguliwa
Wakati huo huo tena, kuna kodi ya nyumba, na bila kisahau bajeti ya chakula cha mwezi huo!
Kwa sababu hiyo, ningependelea kuiomba serikali ione umhimu huo wa kila inapofika mwisho wa mwaka hasa mwezi wa December, serikali iwape wafanyakazi wake wote bonansi ya Tsh 100,000/ bila kujali vyeo na level ya elimu zao ili isaidie bajeti zinazotia ukichaa kwa mwezi huo! Hii itasaidia pia kwa wafanyakazi kuondokana na mikopo isiyo ya lazima
Tanzania ni ngombe wetu sote anayetupa maziwa, ni sisi kuamua maziwa hayo tuyanywe kwa namna gani