Rais Samia: Februari na Machi, 2024, Mgao wa umeme utaisha Nchini

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa salaam za mwaka mpya leo tarehe 31 Desemba, 2023.


Rais Samia Suluhu Hassan, amesema changamoto ya upungufu wa umeme unaosababisha mgawo nchini utaisha baada ya mradi wa bwawa la Julius Nyerere utakapoanza kufanya kazi.

Aidha Rais Samia amesema, Februari mwaka 2024 watawasha mtambo wa kwanza kisha Machi kuongeza mtambo wa pili, mitambo hiyo itatoa umeme Megawati 470 hivyo utafidia upungufu wa Megawati 300 uliopo sasa.

“Habari njema ni kwamba, panapo majaliwa, mwezi Februari 2024 tutawasha rasmi mtambo wa kwanza na mwezi Machi tutawasha mtambo wa pili. Mitambo hii miwili itatupatia jumla ya Megawati 470 na hivyo kufidia upungufu wa sasa ambao ni Megawati 300 tu. Hatua hii itakwenda sambamba na kuwasha mtambo wa Rusumo utakaoongeza Megawati 27.”

“Ni imani yangu na Serikali kwa ujumla kuwa, hatua hizi zitaleta ufumbuzi wa kudumu kwa suala la mgao wa umeme nchini. Aidha, Serikali inaendelea kuwekeza kwenye vyanzo vingine vya umeme kama vile gesi, jua, na upepo, ili kuongeza uhakika wa umeme,”amesema na kuongeza Rais Samia.

RELI YA SGR
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa maagizo kwa wanaohusika na mradi wa reli ya kisasa (SGR) kuhakikisha inapofika Julai 2024 safari za kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma zinaanza.

“Nimekuwa nikisikia mabadiliko ya tarehe za kuanza kwa safari za treni, na kwa kweli, wananchi wamechoshwa na vijisababu, wanataka kuona reli ikifanya kazi. Sasa, naelekeza, ifikapo mwisho wa Julai 2024, safari kati ya Dar es Salaam hadi Dodoma zianze,”amesema Rais Samia.

AMANI, ULINZI NA USALAMA
Mipaka yote ya nchi yetu iko salama, na Muungano wetu unazidi kuimarika. Aidha, vikosi vyetu vya ulinzi na usalama vipo imara. Sote tulishuhudia namna vikosi vyetu vilivyojitoa katika uokoaji na kurejesha hali ya kawaida pale tulipopatwa na maafa. Nitumie fursa hii kuvipongeza kwa ujasiri na uzalendo wao.

MAPITIO YA KIUCHUMI
Katika kuuhami uchumi wetu, tulitekeleza sera madhubuti za fedha ili kuhakikisha utulivu wa bei, kuchochea ukuaji na kudumisha uthabiti wa sekta ya fedha.

Aidha, ukuaji wa Uchumi na Pato la Taifa kwa mwaka 2023 ulikadiriwa kuongezeka kwa 5.2% ikilinganishwa na 4.7% mwaka 2022.

Tumeendelea kudhibiti mfumuko wa bei, ambao katika kipindi cha Januari hadi Novemba 2023 ulipungua hadi wastani wa 3.9%, ikilinganishwa na wastani wa 4.3% kipindi kama hicho mwaka jana, 2022.

SEKTA YA KILIMO
Tumeongeza bajeti ya kilimo kutoka Shilingi Bilioni 751 mwaka jana hadi Shilingi Bilioni 970 mwaka huu, sawa na ongezeko la 29%. Shabaha yetu ni kuchochea kiwango cha ukuaji wa sekta ya kilimo kufikia 10% kwa mwaka, ifikapo mwaka 2030.

Uzalishaji wa mazao ya chakula umeongezeka kutoka tani 17,148,290 msimu wa 2021/2022 hadi tani 20,402,014 msimu wa mwaka 2022/2023, hivyo kufikisha 124% ya kiwango cha utoshelevu chakula nchini.

Serikali imetoa shilingi bilioni 116 kwa NFRA na CPB ili kuchochea soko, ambapo katika awamu ya kwanza NFRA imenunua jumla ya tani 200,293 za mazao. Vilevile, tumeanzisha mnada mpya wa zao la chai.

Hadi Novemba, 2023 tani 204,818.16 za mbolea zilikuwa zimesambazwa kwa wakulima katika mikoa yote ya Tanzania Bara, ikiwemo ruzuku ya serikali yenye thamani ya shilingi Bilioni 67.82.

Serikali imeendelea na jitihada za kuwaingiza vijana na wanawake kwenye uzalishaji, ikiwemo kwa kutenga jumla ya ekari 201,241.6. Aidha, imeanzisha programu ya kilimo cha kisasa iitwayo Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT) ili kuongeza uzalishaji, kuchochea viwanda vya usindikaji na kutengeneza ajira kwa vijana.

SEKTA YA MADINI
Tumeendelea kutoa kipaumbele kwa sekta ya madini, ambapo mwaka huu 2023 tumeshuhudia ongezeko la 6.43% la thamani ya madini yaliyozalishwa.

Pia kumekuwa na ongezeko la 5.8% ya madini yaliyouzwa nje ya nchi hadi kufikia Dola za Marekani bilioni 3.15.

SEKTA YA UTALII
Kipindi cha Januari hadi Oktoba mwaka huu tume-pokea watalii 1,471,567, ikilin-ganishwa na watalii 1,175,930 walioingia kipindi kama hicho mwaka jana.

Kipindi cha Januari hadi Oktoba mwaka huu tume-pokea watalii 1,471,567, ikilin-ganishwa na watalii 1,175,930 walioingia kipindi kama hicho mwaka jana.
 
Point zipo bwana ni vile tu ulikua mzingativu wa pointless ndio maana umekosa .
 
ẞidhani kama tatizo la uchache wa umeme linaeleweka sawasawa

Lakini hakuna Lisilowezekana na Mungu wa Mbinguni
 
Kama mugao utaisha itakuwa jambo la kheri ,lakini si kwa Tanzania ninayoijua mimi
 
Back
Top Bottom