Hotuba mwaka mpya 2024

Bemendazole

JF-Expert Member
Nov 14, 2020
2,356
5,872
Awali ya yote napenda kutoa pole na hongera kwa kila mwananchi kwa pilika za mwaka 2023. Mengi ya kuumiza, kutaabisha, kutia faraja na furaha yalitukia miongoni mwetu. Mungu baba wa rehema alikuwa katikati yetu katika yote hayo hivyo tunapaswa kumshukuru.

Pili napenda kutoa pole kwa kila mwananchi aliyeguswa na tatizo la kukatika kwa umeme. Uchumi wetu umeendelea kukua kwa kasi hivyo kuongeza mahitaji ya umeme yanayozidi uzalishaji.

Hizi ni dalili njema kwamba uchumi wetu unakua kwa kasi. Hata hivyo 2024 tumejipanga kutokomeza changamoto zote za umeme kwa kuongeza uzalishaji na kuzidisha usambazaji.

Mwisho niwatakie wote kila la heri katika kuuhitimisha mwaka '23 na kuukaribisha mwaka '24. Serikali itakuwa pamoja nanyi katika kuimarisha usalama, afya na uzalishaji, kwa ustawi wa kila familia.

Mungu ibariki Tz na watu wake wote. Heri ya mwaka mpya wa '24.
 
Dah
Hotuba tata sana
 
Back
Top Bottom