Historia ya Y2K na Msisimko wa Mwisho wa Dunia wa Mwaka 2000

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,861
Wakati umefika mwaka 1999, Wanasayansi wakaibuka na kudai kwamba mwaka 2000 ungekuwa mwisho wa dunia. Baadhi ya wachungaji wakaungana na wanasayansi hao na kuendelea kusema kwamba mwaka huo Yesu angerudi kwa mara ya pili.

Dunia nzima ilikuwa na wasiwasi, kila mmoja aliona kabisa alikuwa akienda kufa. Wale waliokuwa wakienda kanisani, wakaenda zaidi na wale wa msikitini wakaanza kuswali sala tano kwa kuamini kweli mwaka huo ungekuwa mwisho wa dunia hii.

Watu wa kompyuta wakasema kwamba kompyuta zote duniani zisingefanya kazi tena, yaani kila kitu kwenye dunia hii kingekufa kwa sababu mwaka huo ndiyo ungekuwa mwisho wa dunia hii.

Yaani Disemba ya tarehe 31 saa 2359 ndiyo ungekuwa mwisho wa kuvuta pumzi ya dunia hii. Kumbe Mungu akawa anatucheki tu.
Sasa kuna wajanja wengine nao wakaanzia virusi vya vilivyoitwa Y2K. Hivi vingekuwa vinaharibu kompyuta zote kwa sababu kompyuta za kipindi hicho ziliwekewa mfumo wa ufanyaji kazi wa 19, sasa wakati mwaka ulikuwa unakwenda kubadilika wa 00, kungekuwa na matatizo makubwa kwenye mfumo huo.

Hapa ngoja nikuelezee kidogo uelewe. Wakati kompyuta zimeanzishwa miaka ya 1960, mainjinia hao waliotengeza waliziwekea mfumo wa kutumia 19, waliamini kama mwaka ungebadilika na kuwa 2000, basi zisingeweza kufanya kazi kwa mfumo mpya wa 00.

Hii iliwatia hofu watu wengi kwa sababu kama kweli kompyuta zingebadilisha mfumo basi hilo lilimaanisha hata zile za benki zingepoteza kila kitu na mambo kuanza upya.

Kama kompyuta hizo zingepoteza taarifa, ilikuwa na maana kwamba hata zile pesa zako benki nazo zingepotea.

Sasa dunia nzima ikawa kimya, watu walisikilizia kuona nini kingetokea. Wanasayansi wakazidi kuchochea kwamba dunia ilifika mwisho na kila mtu angekufa.

Wakati huo, hata akinadada nao wakaanzisha mavazi yao yaliyoitwa Y2K (Unaweza kuona hapo kwenye picha).
1710665453728.jpg


Kila mtu alikuwa anazungumzia Y2K, kila kona Y2K lakini mwaka 2000 ulipoingia, hakukuwa na ishu ya Yesu kurudi wala mwisho wa dunia. Mikesha ya mwaka huo kanisani ilijaza watu wengi kwa kuwa waliaminishwa kwamba mwisho wa dunia umefika kumbe hakuna lolote lile.

Wanasayansi wanaweza kufanya kitu chochote kile kukubrainwash, kama waliweza kuwabrainwash mpaka wachungaji, who the hell are you?

Miaka 24 imepita, bado tunaendelea kudunda.
 
Huoni watoto wa Z GENERATION 😁😁
Kuanzia 2000's ndio kifo chenyewe🤣🤣
 
Hapo Ndiyo Kibwetere Wa Uganda Alipowaning'iniza Waumini Kwa Moto Mkali
Halafu Yeye Akapanda Ndege Kwenda Ughaibuni Mpaka Kesho Hajakamatwa
 
Hapo Ndiyo Kibwetere Wa Uganda Alipowaning'iniza Waumini Kwa Moto Mkali
Halafu Yeye Akapanda Ndege Kwenda Ughaibuni Mpaka Kesho Hajakamatwa
Kibwetere ni kama Adof Hitler wa vita kuu ya pili.

Aliangamia kwa moto wa gas ya Petrol aliouasisi mwemyewe.

Angelikimbia, sasa hivi dunia ni kijiji, ni lazima angelifahamika tu alikokwenda kujiswenka!
 
Hahahahahaha nakumbuka na Hadija kopa alitunga wimbo "Y2K ndo yeyee"
Nakumbuka siku ya mwaka mpya nlikua Dodoma tulikaa tunaitafari saa sita usiku itakavyokuwa, kumbe upuuzi mtupu na Joseph Kibwetere akawatia wenzie kibiriti Uganda huko na mali zao akawachukulia
 
Back
Top Bottom