Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 10,129
- 35,152
Kuna mtindo mchafu umeingia kwenye taasisi nyingi za umma wa kuwakopesha pesa watumishi wake kwa kutumia pesa za ndani za uendeshaji wa mashirika hayo kiasi ambacho kimepelekea kukwamisha ufanisi wa uendeshaji wake. Mfano halisi ni mfuko wa Bima ya afya ya taifa (NHIF). Upo ushahidi wa wazi kuwa mikopo hiyo mingi haiwezi kulipika au itapitiliza muda wake wa kuweza kulipika.
Sasa kwa kuwa Pesa za umma ni mali ya umma, na watumishi wa umma ni watu tu waliopewa dhamana ya kuzisimamia hizo pesa, sio sawa na sio sahihi kwa watumishi hao hao tena kuanza kuzitumia kwa maslahi yao binafsi ikiwemo kujikopesha (tena bila riba) pesa hizo hizo kiasi cha kuzorotesha ufanisi wa mifuko hiyo.
Upande wa pili, taasisi za umma hazina utaalamu wa kutosha wa kuendesha zoezi la mikopo kama zilivyo taasisi za mabenki, hivyo busara ilikuwa ni kwa watumishi wa umma kwenda wenyewe kukopa kwenye mabenki.
Mwisho, taasisi za umma sio taasisi za mikopo, na sio jukumu lake la kimsingi kufanya zoezi la kuendesha mikopo.