Zanzibar 2020 Pemba: Vyama sita vya siasa vyalaani vurugu za Alfajiri ya leo, waomba msaada wa IGP baada ya wananchi kukatwa mapanga

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
579
1,000
Mgombea Urais Zanzibar, Ameir Hassan Ameir(Demokrasia, makini): Katika barua yetu ya tarehe 15 kumuomba msajili wa vyama vya siasa pamoja na IGP, tulimuelezea kwamba, kuna baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa hapa nchini kwetu Zanzibar, wameanza tabia ya kuanza kuwashajihisha wanachama wao au wananchi kuingia katika vurugu.

Kwa bahati mbaya, Alfajiri ya leo kuna taarifa kwamba kisiwani Pemba, Kangagani, katika mtaa wa Mwatako kuna baadhi ya wamevamiwa wakati wanataka kuingia Msikitini na wakapigwa mapanga. Ninalaani vikali kitendo hiki.

Mheshimiwa IGP damu imeshaanza kumwagika katika kisiwa cha Pemba. Kupitia press hii tunakuomba mheshimiwa IGP utoe watu wako waende kisiwa cha Pemba na kuwasaka wale wote wanaohusika na kitendo hiki kwani sisi viongozi wa vyama vya siasa maelngo yetu tuendeleze kufanya campaign kwa salama na amani, mimi naamini kuna maisha baada ya siasa.

Kama hatua hazijachukuliwa, basi tungemuomba Rais Magufuli, Rais Shein waahirishe uchaguzi kwa sababu hatuwezi kuingia katika uchaguzi ambapo kuna baadhi ya watu hawana hatia tayari washahatarishwa maisha yao.

====

PEMBA: BAADA YA KUSHAMBULIWA KWA WATU MSIKITI ALFAJIRI YA LEO

Kamishina Msaidizi wa Polisi Mkoani Pemba, Juma Sadi Hamis amethibitisha kutokea kwa tukio hilo alfajiri ya leo

Amesema mhalifu aliingia msikitini wakati wa Ibada na kuwashambulia kwa panga watu watatu kisha akatokomea kusikojulikana. Waliojeruhiwa ni Khakis Makame(62), Bakar Hassan(55) na Kombo Hamad Yusuf(73).

Majeruhi wawili wa tukio hilo wamelazwa Hospitali ya Kangagani na Mmoja hali yake si nzuri hivyo amesafirishwa kwa ndege kupelekwa Hospitali ya Mnazi Mmoja Unguja

Aidha, Jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta mhusika wa tukio hilo.

 

Ndebile

JF-Expert Member
Sep 14, 2011
6,197
2,000
Hao ni "uhamsho masalia" kamata weka ndani watoka Hussein Mwinyi anamaliza awamu ya pili 2030! Twataka amani sie!
 

Mr. Zero

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
12,957
2,000
Nimewasikiliza. Ni Vibaraka wa CCM hao .... wanahalalisha mipango yao .......!!
 
  • Thanks
Reactions: Ami

white wizard

JF-Expert Member
May 18, 2011
5,288
2,000
Kama kila kitu kinaendeshwa kwa haki, mambo kama haya ni nadra sana kutokea!! Mnyonge akichoka, anaona hana cha kupoteza!!! Ila kila mala una mnyanyasa unasema atafanyaje, haya!!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom