Pay stubs za mshahara wa Rais

Pay stubs za mshahara wa Rais

Rais Magufuli, wakati akiwa mapumzikoni huko Chato, iliripotiwa akinukuliwa kuwa akirudi Dar atatoa pay stubs za mshahara wake ili Watanzania anaowatumikia waujue.

Mpaka kufikia sasa, licha ya yeye kurudi Dar kwa zaidi ya wiki mbili sasa (niko tayari kusahihishwa maana siikumbuki vizuri tarehe aliyorudi), sijasikia wala kuona popote pale ambapo hivyo vitu alivyoahidi kuvitoa, kuwa kavitoa.

Naona hata watu walio wengi washasahau tena maana suala lenyewe hata halijadiliwi tena. Ni kama vile lishasahaulika....limekuwa upepo uliokwishapita.

Mimi hili suala siwezi kulisahau na msimamo wangu bado uko palepale. Watanzania walipa kodi wana haki ya msingi kabisa ya kujua pesa zao zinatumikaje.

Kwenye matumizi ya pesa za walipa kodi uwazi ni jambo la lazima.

Nasubiri kuziona hizo pay stubs za mshahara wa rais na asiishie hapo tu. Atuambie malipo yake yote yanayogharamiwa na walipa kodi.

Naamini yeye akifanya hivyo basi hata viongozi wengine wa umma nao wataufuata mfano wake.

mkuu...watanzania tuko vichwa ganii meeeen...tushasahauuu...ni rahisi sana kuitawala Tanzania

hakikisha tu unafanya matukio na majamboz
 
Ngoja nikaone diary yangu....eti ilikuwa moja aprili?
Hivi mtu anayejinasibu kuwa mstaarabu na msemakweli anapoahidi kuwa nikimaliza likizo huku Chato nitaweka hadharani rekodi za malipo yangu ya mshahara ili walipa kodi wajue halafu anarudi Dar anakaa zaidi ya wiki mbili akipiga kimya cha kutisha na badala yake anapiga kelele za kuhimiza watu waendelee kulipa kodi na akiona kuna uwezekano wananchi wakakumbuka ahadi yake anatafuta jipu la Kutumbua au anaibua tukio la kuvamia benki ili apate headline watu wasahau kuhusu hilo utamuelewaje au tutamuitaje?

Wengine hatusahau.Tutaendelea kumkumbusha aweke hadharani malipo yake yote na marupurupu.Afanye sarakasi zote lakini bado hili tutamkumbusha

Haya mambo ya kujifanya umesahau kutimiza ulichoahidi kinaweza kuleta tafsiri isiyoandikika na kupelekea watu kuvunja sheria ya mitandao bure

Hivi anatofauti gani na Mama ana Kilango aliyedaiwa kutumbuliwa kwa kumdanganya mwajiri wake? Mbona sisi ametupigia kimya kuhusu mshahara wake na marupurupu wakati sisi ni waajiri wake na alitupa aidha taarifa au ahadi za uongo?

Hebu tumkumbushe bila ugomvi tuone atatoa sababu gani au atatunga jipu la kutumbua ili kupotezea hii habari?

Hivi kati ya kupiga pushup na kuweka tu hadharani Pay tubs zake ni ipi lipi lenye kutumia nguvu nyingi na kazi nzito zaidi? Au kuna marekebisho(uchafuzi) unafanyika katika hizo record za malipo?

Kataa ukimya huu,hauna afya.Ni ukimya wenye kuchochea hasira na migogoro isiyo ya lazima.

Ni heri aseme ilikuwa April Fools tu yaishe

Aluta Continua,Victory Ascerta....

Ben Saanane
 
Yaani wewe una chuki sana na Magufuli,ila ndo RAIS WA TANZANIA,nothing you can do,kwani mtu akiwa Raisi ndo ubinadamu unamtoka ama?sasa akienda bank mwenyewe kuna tatizo?kwani anavunja sheria za nchi?kuna sheria inayomkataza Rais asipige simu kwenye vituo vya habari?

Hakuna sheria inayomzuia hata akiamua kununua mihogo Coco beach
ana uhuru huo....

hatuwezi wote kuwa na mitazamo sawa...

Sisi wengine tunapenda kumuona Rais wa nchi kwenye headline kwa ya msingi..
akifanya tunayoyaona sio tuna uhuru wa kusema.
ndio maana ya nchi huru....

Hata Mwinyi alianzisha utamaduni wa kuonana na wananchi Lumbumba
wengine waliona ni la maana,wengine waliona ni kioja...
 
Wamarekani wanaujua mshahara wa Obama?
Siyo tu wana ujua bali wanauona live kila April 15 anapo file income tax yake na kuonyesha kalipwa ngapi,kakatwa kodi bei gani na katoa ngapi kwa NGO

Mwaka jana Obama alipata mshahara wa $ 400,000 lkn karibia zote aligawa kwa NGO,ingia online ona mwenyewe
 
Ungeweka wa kwako km mfano kwanza au hata ungeutaja kwakua Rais aliutaja wa kwake.
 
Magufuli ni mtu wa 'stunts'...

Mara kapiga simu kwenye TV..

mara apige simu tena ataleta pay slip

mara aende bank mwenyewe.....mradi kila siku ana 'new stunts'....

kila siku yupo kwenye headline...asipofukuza huyu kaibukia huku....
A moron at best. Tafuta cha kufanya to make use of your valuable time. You lost the election months ago.
 
Haya, tuendelee kusubiri tuone kama ahadi itatimizwa....
 
Kwakua JPM keshaweka wazi labda kama wewe si mtumishi wa umma.

Kaweka wazi kwa maneno tu na hakuna kingine zaidi ya hapo.

Na kusema kweli hajaweka wazi malipo yote anayolipwa na walipa kodi.

Kwa nini tunafichwa matumizi ya kodi zetu?

Halafu mimi raia binafsi. Silipwi mshahara na pesa za walipa kodi.
 
Kaweka wazi kwa maneno tu na hakuna kingine zaidi ya hapo.

Na kusema kweli hajaweka wazi malipo yote anayolipwa na walipa kodi.

Kwa nini tunafichwa matumizi ya kodi zetu?
Issue ilikua ni mshahara na si Vinginevyo, hayo mengine yamejitokeza baada ya yeye kutaja mshahara wake jambo halikutarajiwa kwakua halijawahi kufanywa na watangulizi wake. Hata hivyo tungejikita zaidi kumsaidia JPM kupambana na mafisadi na majanga mengine ili tupate maendeleo. Marupurupu ya Rais si janga la kitaifa kama hayo mengine.
 
Suala la malipo ya viongozi limejikita katika hoja ya uwazi.

Kuwaelimisha watu kuhusu hilo nako ni kulisaidia taifa kwa sababu inavyoonekana watu wengi hata hawajui kuwa wao ndo waajiri wa hao viongozi.

Huwezi kupambana na ufisadi bila kuwa na uwazi. Utakuwa unajidanganya tu.

Na usiri ni ndo mazingira mazuri sana ya kuzalisha ufisadi na mafisadi.

Nitajie nchi mmoja tu iliyo na utawala bora ambayo mishahara na malipo mengine ya viongozi wake ni siri kubwa.
 
Suala la malipo ya viongozi limejikita katika hoja ya uwazi.

Huwezi kupambana na ufisadi bila kuwa na uwazi. Utakuwa unajidanganya tu.

Na usiri ni ndo mazingira mazuri sana ya kuzalisha ufisadi na mafisadi.

Nitajie nchi mmoja tu iliyo na utawala bora ambayo mishahara na malipo mengine ya viongozi wake ni siri kubwa.
Kuna tume ya maadili ya uongozi na kuna TAKUKURU kama kuna sheria inayotamka kua Viongozi wataje mishahara yao hadharani mm naunga mkono hoja kinyume cha hapo alichofanya JPM ni kitendo cha kishujaa.
 
Taasisi ya Urais siku hizi! Mmmh! Kila mtu anajibwatukia tu..
Kwa mfano hata ukijua hizo stubs, wewe zinakusaidia nini? Will it change anything? How?

You always find a weak point to cling on so that you can remain relevant.. The Boss calls it 'stunt'!
Itatusaidia nini?kama analipwa kiasi kikubwa inabidi iundwe tume maalumu ya kurekebisha mishahara ya viongozi wote wa umma iendane na hali halisi ya uchumi wetu.
 
Rais Magufuli, wakati akiwa mapumzikoni huko Chato, iliripotiwa akinukuliwa kuwa akirudi Dar atatoa pay stubs za mshahara wake ili Watanzania anaowatumikia waujue.

Mpaka kufikia sasa, licha ya yeye kurudi Dar kwa zaidi ya wiki mbili sasa (niko tayari kusahihishwa maana siikumbuki vizuri tarehe aliyorudi), sijasikia wala kuona popote pale ambapo hivyo vitu alivyoahidi kuvitoa, kuwa kavitoa.

Naona hata watu walio wengi washasahau tena maana suala lenyewe hata halijadiliwi tena. Ni kama vile lishasahaulika....limekuwa upepo uliokwishapita.

Mimi hili suala siwezi kulisahau na msimamo wangu bado uko palepale. Watanzania walipa kodi wana haki ya msingi kabisa ya kujua pesa zao zinatumikaje.

Kwenye matumizi ya pesa za walipa kodi uwazi ni jambo la lazima.

Nasubiri kuziona hizo pay stubs za mshahara wa rais na asiishie hapo tu. Atuambie malipo yake yote yanayogharamiwa na walipa kodi.

Naamini yeye akifanya hivyo basi hata viongozi wengine wa umma nao wataufuata mfano wake.
.....hivi na wewe umenasa mtego wa kujadili hili mkuu, unaweza kuletewa pay stubs mpaka za laki moja sasa badala ya milioni, nn kinashindikana kwa mfano!!! Tupige kazi tuachane na hii maneno!!!!!
 
Back
Top Bottom