Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 93,497
- 119,432
Rais Magufuli, wakati akiwa mapumzikoni huko Chato, iliripotiwa akinukuliwa kuwa akirudi Dar atatoa pay stubs za mshahara wake ili Watanzania anaowatumikia waujue.
Mpaka kufikia sasa, licha ya yeye kurudi Dar kwa zaidi ya wiki mbili sasa (niko tayari kusahihishwa maana siikumbuki vizuri tarehe aliyorudi), sijasikia wala kuona popote pale ambapo hivyo vitu alivyoahidi kuvitoa, kuwa kavitoa.
Naona hata watu walio wengi washasahau tena maana suala lenyewe hata halijadiliwi tena. Ni kama vile lishasahaulika....limekuwa upepo uliokwishapita.
Mimi hili suala siwezi kulisahau na msimamo wangu bado uko palepale. Watanzania walipa kodi wana haki ya msingi kabisa ya kujua pesa zao zinatumikaje.
Kwenye matumizi ya pesa za walipa kodi uwazi ni jambo la lazima.
Nasubiri kuziona hizo pay stubs za mshahara wa rais na asiishie hapo tu. Atuambie malipo yake yote yanayogharamiwa na walipa kodi.
Naamini yeye akifanya hivyo basi hata viongozi wengine wa umma nao wataufuata mfano wake.