Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,380
- 39,333
Sijui kama wenzangu mlinotice au la.. hivi kwanini Karume apewe heshima ya Kijeshi Tanzania bara na kupokea saluti kwenye siku kuu ya Mashujaa wakati nafasi yake kwenye baraza la mawaziri wa Muungano ni kama waziri tu? Wakati Rais na Makamu wake hawapo nchini anayefuatia ni Waziri Mkuu na hakuna mahali hata pamoja panapompa Rais wa Zanzibar protokali hiyo. Waziri Mkuu yupo Dar kwanini Karume asimame kama vile ni kiongozi wa Muungano??? Hizi nazo ni kasoro za muungano wetu!!!!
