Makonda: Kuna UJINGA unaendelea wa kumtofautisha Hayati Magufuli na Rais Samia

I am Groot

JF-Expert Member
Jul 20, 2018
3,731
10,033
Makonda katika sherehe za kuipokea ndege mpya ya ATCL (BOEING 737-9 MAX) jijini Dar; amekemea tabia inayoonekana kuanza kukua na kukomaa kwa baadhi ya viongozi wa Serikali kwa ngazi mbalimbali ya kujaribu kutenganisha mafanikio yanayoendelea kutokea chini ya Rais Samia na kipindi cha awamu ya tano chini ya JPM.

Wakijaribu kuchafua huku na kusifia huku. Kitendo kicho makonda amekemea na kutaka tabia hiyo ife kuanzia leo.

Kwani hata kipindi cha kuomba kura wawili hao walizunguka kila mahali pamoja akiwemo waziri mkuu kasimu majaliwa.

Awataka waache UNAFIKI na KUJIKOMBAKOMBA.

Ndugu zangu Watanzania,

Mimi leo wala sina maneno mengi ila nataka tu kuwaambia kuwa katika siku ya leo ambapo ni siku ya mapokezi ya ndege mpya iliyonunuliwa na serikali yetu ya CCM. Mheshimiwa Paul Makonda Katibu wa itikadi, uenezi na mafunzo wa CCM Taifa .

Kwa hasira kali na kuonyesha moyo wake kujaa jazba na uchungu moyoni ametumia muda wa dakika mbili aliopewa kusalimia kuwashambulia wanasiasa aliowaita wanafiki, wajinga na wanasiasa uchwara wanaojipendekeza na kutaka kuonyesha kuwa mafanikio yaliyopatikana chini ya uongozi wa Rais Samia kuwa Hayati Dkt Magufuli hahusiki nayo.

Amesema huo ni unafiki mkubwa sana na ujinga kwa sababu Rais Samia anatekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM 2020-2025 ambayo Rais Samia na Hayati Dkt Magufuli waliinadi kwa pamoja kwa kuzunguka katika Taifa zima hivyo anachokifanya Rais Samia ndicho alichofanya Hayati Dkt Magufuli na huwezi kuwatenganisha au kuwatofautisha, hivyo Rais Samia anaendelea na kazi hiyo ya utekelezaji wa ilani ya CCM.

Ametoa marufuku na onyo kali kwa wanasiasa kuwa leo iwe ndio mwisho wa tabia hiyo ya unafiki na ujinga huo wa kumuweka kando au kuwatenganisha Hayati Dkt Magufuli na Rais Samia katika mafanikio ya Rais Samia, amesema kuwa Waziri Mkuu Mh kasimu Majaliwa ndiye yule yule waziri mkuu wao wote wawili yaani Hayati Dkt Magufuli pamoja na Rais Samia na Serikali ni moja na chama ni kile kile kimoja yaani CCM.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

VIDEO:

Tatizo linaanzia hapo Msoga kwenye ile familia ya "Fisi" Wa Taifa.
Tamaa iko mbele kuliko utu wao.
Baba anakula 80% ya mshahara wa Rais aliyepo madarakani.
Mama Mbunge,anakula mshahara mnomo na marupurupu yoote.ikiwemo hii aliyojipendekezea hivi karibuni "Mafao ya wenza wa viongozi wastaafu".
Mtoto Mbunge na waziri mwandamizi akiishi kwa matarajio ya URITHI Mkubwa huko mbeleni.

Lakini hawatosheki na sasa wanaratibu kuua Legacy ya Magufuli kwa siku zoote!
 
Wanafiki ni wakupopolewa
iu

Let the Races begin
 
Ndugu zangu Watanzania,

Mimi leo wala sina mengi ila nataka tu kuwaambia kuwa katika siku ya leo ambapo ni siku ya mapokezi ya ndege mpya iliyonunuliwa na serikali yetu ya CCM. Mheshimiwa Paul Makonda Katibu wa itikadi, uenezi na mafunzo wa CCM Taifa . Kwa hasira kali ametumia muda wa dakika mbili aliopewa kusalimia kuwashambulia wanasiasa aliowaita wanafiki,wajinga na uchwara wanaojipendekeza na kutaka kuonyesha kuwa mafanikio yaliyopatikana chini ya uongozi wa Rais Samia kuwa Hayati Dkt Magufuli hahusiki nayo.

Amesema huo ni unafiki mkubwa sana kwa sababu Rais Samia anatekeleza ilani ya uchaguzi ya 2020-2025.ambayo Rais Samia na Hayati Dkt Magufuli waliinadi kwa pamoja.hivyo anaendelea na kazi hiyo.ametoa marufuku na onyo kali kwa wanasiasa kuwa leo iwe mwisho wa tabia hiyo ya unafiki na ujinga .amesema kuwa Waziri Mh kasimu majaliwa ndiye yule yule waziri mkuu wao wote wawili yaani Hayati Dkt Magufuli pamoja na Rais Samia.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
Kwani Makonda anatumikia mabwana wangapi?

Kwani si Kuna miradi inayoitwa ya Magufuli na miradi ya awamu ya 6 au?
 
Tatizo linaanzia hapo Msoga kwenye ile familia ya "Fisi"
Wa Taifa.
Tamaa iko mbele kuliko utu wao.
Baba anakula 80% ya mshahara wa Rais aliyepo madarakani.
Mama Mbunge,anakula mshahara mnomo na marupurupu yoote.ikiwemo hii aliyojipendekezea hivi karibuni "Mafao ya wenza wa viongozi wastaafu".
Mtoto Mbunge na waziri mwandamizi akiishi kwa matarajio ya URITHI Mkubwa huko mbeleni.

Lakini hawatosheki na sasa wanaratibu kuua Legacy ya Magufuli kwa siku zoote!
Kuna miradi kedekede ambayo Magufuli hahusiki.

Sasa huyo Makonda anajua hii ni awamu ya ngapi? Anatumikia mabwana wangapi?

Samia fukuza huyu Makonda
 
Ni kweli wana ccm ni wanafiki ILA SAMIA hawezi kuwa hata ⅛ ya MAGUFULI.

Aliyoyafanya mwamba hayawezi hata kuwa benchmark kwa waliopo, labda kama mmedhamiria kuwafelisha.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Mimi leo wala sina maneno mengi ila nataka tu kuwaambia kuwa katika siku ya leo ambapo ni siku ya mapokezi ya ndege mpya iliyonunuliwa na serikali yetu ya CCM. Mheshimiwa Paul Makonda Katibu wa itikadi, uenezi na mafunzo wa CCM Taifa .

Kwa hasira kali na kuonyesha moyo wake kujaa jazba na uchungu moyoni ametumia muda wa dakika mbili aliopewa kusalimia kuwashambulia wanasiasa aliowaita wanafiki,wajinga na wanasiasa uchwara wanaojipendekeza na kutaka kuonyesha kuwa mafanikio yaliyopatikana chini ya uongozi wa Rais Samia kuwa Hayati Dkt Magufuli hahusiki nayo.

Amesema huo ni unafiki mkubwa sana na ujinga kwa sababu Rais Samia anatekeleza ilani ya uchaguzi ya 2020-2025.ambayo Rais Samia na Hayati Dkt Magufuli waliinadi kwa pamoja.hivyo anachokifanya Rais Samia na Katika kuendelea na kazi hiyo ya utekelezaji wa ilani ya CCM.

Ametoa marufuku na onyo kali kwa wanasiasa kuwa leo iwe ndio mwisho wa tabia hiyo ya unafiki na ujinga huo wa kumuweka kando Hayati Dkt Magufuli katika mafanikio ya Rais Samia. amesema kuwa Waziri Mkuu Mh kasimu Majaliwa ndiye yule yule waziri mkuu wao wote wawili yaani Hayati Dkt Magufuli pamoja na Rais Samia.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
Tunaposema huko CCM hakuko shwari muwe mnatuewa.
 
Back
Top Bottom