Salaam.
Wakuu kuna tetesi zimeanza kuenea kuwa leo Paul makonda anataka kufanya press Conference ili kujisafisha na tuhuma nzito zinazomkabili kuhusu kumpiga mzee wetu waziri mkuu mstaafu jaji Joseph Warioba.
Hii ni dharau kwa taifa na watu wake tuhamasishane kupitia hapa na kuwaomba wahariri wote wagomee kwenda kumsikiliza huyu bwana mdogo kama tetesi hizi zitakuwa na ukweli ndani yake.
Nawasilisha.
Kuna kitu kinaitwa "the right to be hard!", kanuni ya kwanza kabisa ya haki ni "no one is condemned unheard!", ndio maana kwenye kashfa ya Richmond, mimi ni miongoni mwa watetezi wakuu wa Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa kuwa hakuhusika direct kwa sababu hakuhojiwa na hakupewa haki ya hakusikilizwa!, hivyo hawezi kushutumiwa!.
Kwa tulio angalia vurugu zile kupitia TBC video footage, kijana alionekana wazi akimsaidia yule mjumbe mwenye ulemavu wa kutoona!, inawezekana kabisa, lengo la kijana kumfikia Jaji Warioba, lilikuwa ni kumsadia!, hivyo kwa vyombo vyote makini vya habari, vitatuma waandishi ma senior wenye uwezo wa kuhoji "the motive behind" uwepo wa kijana huyo kwenye kongamano lile!. A lame excuse kuwa "it was an open public forum" hivyo yeye kama alivyo Mtanzania mwingine yoyote, had the same rights to be there, can't just sail through, kirahisi!, kijana huyu anapaswa kusikilizwa kwa makini utetezi wake, ili pia kubaini "his motive behind!".
Fujo zile zilizotokea pale, ni matokeo tuu, kuna chanzo na hicho ndicho muhimu zaidi.
Waandishi nendeni!, tena mimi ningelikuwa bado ni mwandishi wa press, hapa ndipo haswa nilipaswa kuhudhuria hii press conference, sio ili kuripoti kitakachosemwa!, bali kuripoti kile ambacho hakikusemwa, "the motive behind, the reasons behind!" and "the causative course" ambayo ndio "the mens rea", kwenye "the actus reus" ya vuruge zile!.
Pasco.