Pasipoti ya Tanzania yawa ya 69 kwa Ubora duniani na Watanzania sasa wanaweza Kusafiri nchi 73 bila Viza

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,689
109,119
Kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati inazidiwa na Kenya tu ambayo sasa Pasipoti yao imepanda Ubora na kuwa ya 66.

Nchi ya Singapore ndiyo inaongoza kwa kuwa na Pasipoti Bora na Wananchi wake kuweza Kusafiri bila Viza katika nchi 192 kati ya nchi zote 227 zilizoko duniani.

Katika Ripoti ya Taasisi ya Henley Passport Index mwaka jana ( 2022 ) Tanzania ilikuwa nafasi ya 76 kwa Ubora wa Pasipoti yake.

Nchi za Ujerumani, Italy na Hispania zinashika nafasi ya Pili huku nchi za Japan, France na Sweden zikishika nafasi ya Tatu kwa kuwa na Pasipoti Bora duniani.

GENTAMYCINE ambaye hata sina Pasipoti yenyewe kama ilivyo kwa adriz na Bila bila bado najua mpaka sasa kati ya Watanzania Milioni 61 tuliohesabiwa mwaka jana wenye Kumiliki Pasipoti Mpya za Kielektroniki ni Laki Sita na kadhaa tu.

Pongezi Kwenu UHAMIAJI Tanzania hasa kwa Commissioner General of Immigration ( CGI ) Dk. Anna Makakala kwa Kazi nzuri na Tukuka juu ya Uimara na Uzuri wa Pasipoti.

Kwa yule tu anayetaka Kusoma zaidi Taarifa hii na una uhakika kuwa Kiingereza chako si cha Mashaka Mashaka na ni cha uhakika ( unakijua vyema ) nenda The CITIZEN Online ukaisome kwa utuo zaidi baada ya Kuandikwa vyema kwa Kiingereza cha uhakika na Mwandishi mahiri wa Taarifa za Biashara Mwanadada / Mwanamama Josephine Christopher wa MCL.
 
Kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati inazidiwa na Kenya tu ambayo sasa Pasipoti yao imepanda Ubora na kuwa ya 66.

Nchi ya Singapore ndiyo inaongoza kwa kuwa na Pasipoti Bora na Wananchi wake kuweza Kusafiri bila Viza katika nchi 192 kati ya nchi zote 227 zilizoko duniani.

Katika Ripoti ya Taasisi ya Henley Passport Index mwaka jana ( 2022 ) Tanzania ilikuwa nafasi ya 76 kwa Ubora wa Pasipoti yake.

Taarifa za Biashara Mwanadada / Mwanamama Josephine Christopher wa MCL.
Wenye passport ni laki sita? Hata asilimia kumi bado? Safari bado ni ndefu mno!
 
Mtu mwenye akili atauliza swali hili, ' ubora wa passport hupimwa Kwa vitu gani?'
 
Mtu mwenye akili atauliza swali hili, ' ubora wa passport hupimwa Kwa vitu gani?'
Kaiulize Taasisi ya Henley Passport Index, Watu wa IATA, Immigration na Foreign Affairs watakuwa na Jibu zuri kwa Nut kama Wewe.
 
Back
Top Bottom