Part 2: TISS bado safari ngumu

Part 2: TISS bado safari ngumu

Mkuu, wanaotunga Sera ya mambo ya nje ya Tanzania pamoja na kumshauri Raisi juu ya utekelezaji wake ni hawa ndugu zetu wa TISS, wakishirikiana na wizara mbalimbali hasahasa zile za mambo ya nje na ulinzi pamoja na jeshi la wananchi. Sasa ukijiuliza swali rahisi kabisa ni kwa kiwango gani tumeweza kutekeleza sera mpya ya mambo ya nje ya Tanzania, utabakia ukisikitika.

Sera ya kwanza ya mambo ya nje ya Tanzania ilitangazwa na Mzee Nyerere miaka ya 1960's mbele ya mabalozi wa nchi za nje na ilijikita kwenye mambo yafuatayo:

Mosi, kutengeneza Tanzania huru isiyofungamana na kambi yotote ile ya vita baridi, ili kuipesha Tanzania isiingie kwenye machafuko kama yale ya Zaire, Vietnam na Korea.

Pili, kupigania uhuru wa nchi za Afrika, hasahasa zile zinaziozunguka Tanzania na kuhakikisha zinakuwa ndani ya ushawishi wa Tanzania. Mfano Msumbiji, Angola, Uganda, Namibia, Afrika Kusini, Zimbabwe, Lesotho, Zambia, Malawi na Botswana.

Tatu, kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika kukabili changamoto za amani ulimwenguni.

Nne, kupambana na ushawishi wa Kizayuni barani Afrika, pamoja na kuzuia kusambaa kwa ushawishi wa Serikali ya Kikabulu ya Afrika Kusini.

Sasa kazi za TISS zilikuwa zikizunguka kwenye mhimili huo tokea mwaka 1976 hadi 1989 baada ya kuisha kwa vita baridi na 1991 baada ya umoja wa kisovieti kuanguka. Katika malengo yote ya Sera ya mambo ya nje TISS walifanya kazi katika weledi mkubwa sana kwasababu waliweza kuyatimiza hayo malengo kwa asilimia 90%.

TISS ilituvusha salama kipindi chote cha vita baridi, japo uchumi ulikuwa mbaya lakini kama nchi tulikuwa na mwelekeo mzuri sana kama tungefanya mabadiliko ya kiuchumi vizuri, kitaalamu na taratibu hasa kipindi cha mfumo wa soko huria.

Miaka ya karibuni tulirekebisha sera yetu ya mambo ya nje, na kujikita kwenye diplomasia ya kiuchumi ambayo tokea kipindi cha Mkapa tulichofanikisha ni kufutiwa madeni makubwa ya nje, kufufua Jumuiya ya Afrika Mashariki, Kuimarisha SADC, kuleta uwekezaji mkubwa wa nje ambao kwa namna moja au nyingine haukuwa na maslahi makubwa kwa taifa letu.

Sasa kabla ya kuzungumzia hujuma za kiuchumi inabidi tuimulike TISS katika kutunga na kutekeleza sera za nchi ambazo ni za muda mrefu (Strategic Policies) ambazo kwa kipindi hiki ni Sera ya Elimu, Sera ya mambo ya nje, Sera ya Ulinzi na Usalama, Sera ya uwekezaji, Sera ya tafitiki kubwa za kisayansi, Sera ya Kilimo na Sera ya viwanda.Hapa tumefanikiwa kwa kiasi gani ???

Baada ya hapo nadhani ndiyo tuanze kuzungumzia hizi hujuma kama bomba, ndege na kukwama uwekezaji wa nje ambazo ni sehemu ya madhara (Symptoms) yatokanayo na kushindwa kutekeleza sera za nchi kwa kiwango kinachotakiwa.
SAFI SANA. Aya ya pili kutoka mwisho ndio hasa tunatakiwa kufanyia kazi kama ikitokea dirisha la kubadilisha mambo. Kingine ni chanzo chake cha fedha ni muhimu sana. Watengewe budget yao kwa namna yoyote hata kama itakuwa ya siri(bila shaka) ya kutosha.
 
Mkuu,

Kwahio hii ya 1970 ndo general

Na hii ya 1996 ni ya Usalama wa taifa.

Je, huoni kwamba kuna haja ya kuzifanyia mabadiliko sheria hizi na kuitunga sheria moja tu ya Usalama wa taifa?
Nakubaliana na wewe kufanyia mabadiliko lakini kila sheria ibaki kivyake. Moja ifanye kazi kwa watu wote wanaoweza kukutana na nyaraka, silaha, nyara, maofisa, fedha, mali au chochote chenye kuhusiana na usalama wa JMT na TISS wawe na sheria specific kwa ajili yao iliyoboreshwa kwa kiwango cha sasa na cha wakati huu na ujao.
 
Nakubaliana na wewe kufanyia mabadiliko lakini kila sheria ibaki kivyake. Moja ifanye kazi kwa watu wote wanaoweza kukutana na nyaraka, silaha, nyara, maofisa, fedha, mali au chochote chenye kuhusiana na usalama wa JMT na TISS wawe na sheria specific kwa ajili yao iliyoboreshwa kwa kiwango cha sasa na cha wakati huu na ujao.

Kabisa.
 
Vitu vingine vya muhimu ni:
1. Mseto wa watumishi wa taasisi ya ujasusi na usalama wa nchi. Iache kuegemea kwa watu waliosoma tabia za binadamu, ulinzi, sheria na uchumi pekee. Tunahitaji watu wa kada zote. Tunahitaji watu wa ICT hasa, Wahandisi, madaktari, walimu, watu wa mazingira. Namaanisha uwiano wa watumishi uangaliwe. Composition ya taasisi iwe imara. Wakifanya hivyo itakuwa wakitoa kitu kilichochambuliwa basi kinakuwa cha ukweli usio na mashaka.
2. Wakati wa recruitment: Ili uweze kuwa na uhakika wa composition nilioutaja hapo juu, basi hakuna budi kufanya recruitment kuanzia A-LEVEL, Vyuoni na Makazini. Hapo ndio unakuw na uhakika kwamba huyu mtu ataleta utaalam gani kwenye taasisi pamoja na uwezo wake katika mambo ya kiusalama na kijasusi. Tuache kuajiri kiholela.
3. Kuwasomesha na kuwaendeleza watumishi wake hasa wa ICT kwa kuwapekeka vyuo vya hali ya juu vya kimataifa i;li waweze kusaidia katika eneo la ICT. Hta wakiendelezwa katika vyuo vyetu. na wapewe eneo maalum la kukazia(specific areas of concentartion).
4. Kuepusha PSU kuifunika TAASISI wakati PSU ndio subset ya TAASISI.
 
Idara ya usalama wa taifa, ndo idara nyeti, nzito na muhimu kuliko idara zote za serikali.
Kwa hiyo panatakiwa pawe na wafanyakazi ma genius hasa ktk idara hiyo, na wasiwe na mapenzi ya chama chochote cha siasa, bali wawe na mapenzi na nchi yao tu.
Wawe wabunifu kwa ajili ya usalama wa taifa lao, usaili wa ajira ufanyike bila kuangalia kiwango cha Elimu ya mtu (kwa baadhi ya vitengo) bali uwezo, weledi, uzalendo wa nchi na akili za mtu.
Neno usalama wa taifa ni neno pana sana, naipenda sana nchi yangu Tanzania ndo maana naamini ushauri wangu kuna siku utafanyiwa kazi vilivyo.
Usalama wa taifa ni lazima wahakikishe nchi ina uchumi mzuri, kwa sababu watu wakilala njaa na kukosa mahitaji muhimu matokeo yake nchi inaweza kuingia kwenye vurugu kubwa mno na hivyo kufanya usalama kutoweka.
Ndo maana nasema hii ni idara nyeti mno, taifa lolote lenye uchumi mbovu na maisha magumu kwa watu wake ina maana pia usalama wa taifa ni dhaifu hauwezi kulinda usalama wa nchi kwa uhakika.
Kutisha watu,na kuua wapinzani ni kuzidi kupanda mbegu za chuki na bomu ambalo mwisho wa siku ni lazima lilipuke .
Kama idara ya usalama wa taifa haina kitengo cha kufanya hujuma za kiuchumi kwa mataifa ya nje kwa faida ya nchi ina maana bado kitengo ni dhaifu na kina watu ambao hawajapikwa na kuiva hasa.
Kila napokuja nyumbani Tanzania na kuangalia mazingira ya nchi yapo duni mno, vijana wengi wakishinda vijiweni hawana kazi za kufanya, huwa najiuliza nini hatima ya nchi Kama hii?
Lowassa aliwahi kusema, ukosefu wa ajira ni bomu linalosubiria kulipuka siku moja.
Basi idara ya usalama wa taifa inatakiwa ihakikishe hilo bomu halilipuki kwa gharama yoyote, ikibidi kufanya ujambazi (ujasusi) wa kiuchumi kwa mataifa ya nje na kuleta nyumbani ili watoto wale.
Urusi ilikuwa taifa la kwanza Duniani kupeleka chombo na wanaanga kwenye mwezi .
Marekani ilipoona hivyo, ikajaa wivu na ilipojaribu kwenda, chombo chao kililipuka kwa sababu ya hitilafu kwenye engine, wakajiuliza kwa nini warusi waliweza na sisi kushindwa?
Walichofanya ni kuiba teknolojia ya Urusi ya engine hadi wakafanikiwa kwenda.
Sisi tuna wivu wa kichawi, tunapigana vita ndugu kwa ndugu, hatutaki wapinzani waingie ikulu, badala ya kupigana Vita ya kumaliza umaskini, tunamalizana sisi kwa sisi.
Halafu anasimama mtu na kusema eti tutafanikiwa, tutafanikiwa kwa lipi wakati mikono yetu ina Damu za watu zinazolia kwa Mungu zikidai kisasi?
Yaani idara ya usalama wa taifa ilishuhudia kabisa viwanda zaidi ya 400 alivyoacha Mwl Nyerere vikiuliwa, lakini idara hiyo haiko tayari kushuhudia mkosoaji wa serikali akisimama hadharani na kuikosoa serikali ,labda awe nyuma ya keyboard Kama mimi hapa

INAENDELEA
Mada imekaa kiushambenga na hazina ukweli sehemu nyingine.

Urusi haikuwa ya kwanza kupeleka binadamu mwezini bsli ilikuwa ya kwanza kupeleka binadamu angani.
Mtu mwanaanga huyo aliitwa Yuri Gagarin, na ilifanyika mwanzoni mwa miaka ya 60.

Binadamu wa kwanza mwezini ni Neil Armstrong na alitua huko katika chombo Apollo 11 mwaka 1969.

Kwa taarifa yako ulichosema juu ya idara ni hisia zako tu ambazo haziko researched.
 
Yaani kama ni alama Mkuu umepata 99.99%..tatizo siyo TISS au CCM hayo ni matokeo tu ya tatizo kubwa tulilo nalo wote kama watanzania, mfumo wetu wa elimu ulifail kitambo sana, mfumo ambao uliwekwa ili kila anayepata elimu anaelimika na elimu inambadilisha zile tabia na mazoea yasiyo na tija yanakufa, anakuwa mtu mpya..tabia za ubinafsi, chuki kwa wengine, wivu, ushirikina, kujiona bora kuliko wengine, kiburi na dharau nk Tanzania ina watu wachache sana walioelimika, wengi wamekusanya vyeti tu..maarifa ZERO! bahati mbaya sana watu wa aina hii ndiyo wapo TISS, kugeuza hali hii inahitaji nguvu ya wananchi kupitia sanduku la kura ili wpatikane wawakilishi walioelimika waanze kuweka misingi upya hasa kwenye maeneo strategic kama wizara ya Elimu, wizara ya fedha, TISS nk elimu yetu ndio chimbuko la yote haya, nilitarajia waziri wa elimu alete mabadiliko ya msingi kwenye elimu yetu badala ya kukimbizana na ishu ambazo mtu yeyote hata mwenye elimu ya darasa la saba anaweza kuzifanya..kwa mfano bado ni sahihi kuchagua maeneo ya fani kama sheria, elimu, uhandisi, mambo ya jamii nk kwa ngazi ya chuo kikuu kwa kutizama ufaulu wa kidato cha sita..nadhani ufaulu wa kwenye makaratasi ni kitu kidogo sana kupima uwezo wa mtu husika kwenye jambo fulani, wengine walishaacha mfumo huu, kwa nini kuchagua mtu kwa matokeo ambayo si yako..mfano mwingine, hao TISS kila anapokuja Rais mpya nilitarajia wao wasaidie kuweka mazingira mazuri kimuundo hasa kwenye kubuni wizara kulingana na mabadiliko yanayoathiri utendaji wa wizara zetu, sikutarajia wakati Rais huyu anaanza kuwe na wizara ya VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI kama wizara moja, ukipima mambo hayo 3 kila moja linaweza kuwa wizara peke yake..lakini kwa vile wahusika wanafanya kwa mazoea na pengine hawataki kufikiri zaidi ya wanachokijua na kukiona tunaishia kuja kulaumu Mwijage, mara Kakunda, hata huyu kijana aliyepo hamna analofanya, tatizo si yeye, tatizo ni waliounda hiyo wizara, msimamizi anataka wizara ifanye anayotarajia, waliomsaidia kuiunda wizara walipishana na vision yake kwa wizara hii..unadhani tutatoka hapo, thubutu! Tutatue tatizo la msingi kwanza ELIMU, tufanye elimu yet itubadilishe, itufanye tuwe na kiu ya kujifunza mambo mapya, kusoma vitabu, kufahamu matatizo yetu na kuleta majibu nk not business as usual au nikipata kazi basi ndio nimefika, dont need more! nabaki kuwa KEEPER hadi nistaafu, hilo siyo lengo la ELIMU!
[/QUOTE
Lete suluhisho badala ya kutetea udhaifu kwa kuleta udhaifu wa maeneo na sekta nyingine.
Suluhisho lipo na hata nikilileta hapa jukwaani litafanya nini smartass?
 
Haya tunayoongea wala hayataweza kutokea mpaka tutakapotiana Adabu ndio wataamka usingizi na watafanya mambo kwa maslai ya Taifa sio ya Chama. Ila kwa sasa wapo kwenye Mode ya "Sikio La Kufa"
 
Naona uko kwenye theory za economic Hitman.Hizo hazitumiei na vinchi vidogo Kama vyetu zonatumiwa na mataifa makubwa yenye nguvu kubwa Sana ya kiuchumi dhidi ya nchi ndogo zisizo na.nguvu kwa kutumia vitu Kama vikwazo vya kiuchumi,masharti ya mikopo na misaada,Kutumia nguvu ya soko na Bei SI unajua beo za vya kwetu hatupangi Bei Ila vya kwao Bei wanaipanga wao.Unapngea vitu vya kusoma kwenye Novel.Tanzania Ina ubavu gani wa kuhujumu mfano uchumi wa marekani? Marekani inaweza ndio.maana Iran wanalia,Korea kaskazini wanalia nk unaongea kwa kujiamini Lakini Sio Siri kichwani uko mweupe una confidence za ujasiri wa kuonyesha ujinga

Tanzania haiwezi kuhujumu uchumi wa USA, CHINA nk lakini Tanzania inaweza kutumia maendeleo ya China na USA kama prime mover ya uchumi wake. Hapa ndipo matumizi ya akili yanatakiwa ili mbinu zitengenezwe na utekelezaji ufuate.
 
CCM hawako tayari hata siku moja kuziachia taasisi nyeti zijitegemee na kuwa neutral side maana hii ni hatari kwa uwepo wake, Ukizifanya taasisi nyeti zote ziwe neutral na ziwepo kwa maslahi ya umma basi nusu na robo ya viongozi wa chama na serikali wanaweza kuwa jela au kufa na CCM yenyewe inaweza kuzikwa rasmi.

Miezi ya karibuni kuna kesi ya Rushwa inayohusisha mawaziri wa Kenya katika serikali ya Kenyata, ukifuatilia hii kesi na action zake utagundua Tanzania bado tunavitu tunahitaji kujifunza.
 
Kuna watu mna post tamu sana yani hata kama huna elimu yyt ni macho tu unaelewa basi na wengine wanaohusika na chochote katika hilo wakaelewe lengo ni kujenga na si kubomoa kama hatuwezi kuwafikia kwa chochote basi tuandike chochote vitafika tu
 
Teknolijia kubadilika huwa Siri kubwa hata CiA hawawezi jua Ni bussiness.Watu hujifungia ndani kimya kuzigundua kwa kuogopa mtu mwingine asijebwawahi wakakosa biashara.Wakishagundua huingia sokoni ghafla kwa kushtukiza Kama mchina alivyowashtukiza nchi za magharibi na marekani kwa kuiteka Afrika kwa kuuza bidhaa za Bei nafuu na mjapan alivyoua soko la magari ya nchi za Ulaya Afrika.Nchi za Afrika magari yao yalikuwa ya kifaranza ,kiingereza na kijerumani na kiitaliano Kama landrover,Benz,Renault ,pegeout,Leyland ,Fiat nk. ofisi zote za serikali na watu binafsi na kila Kona Hayo ndio yalikuwa yametawala.Lakini Pamoja na wao kuwa na mashirika ya kijasusi yanayosifika duniani yakishindwa kujua mjapan kakifungia kiteknoljia anafanya Nini..Mjapan ghafla bin vuu akaingia sokoni akawavurumishia mbali watengeneza magari wa ufaransa,uingereza na Ujerumani watoke Afrika.Hadi Leo wako hoi.Soko la Afrika limechukuliwa na wachina na wajapan.Mnaandika vitu vya kufikirika mnavyosoma kwenye novel na kuangalia kwenye Movie.CIA wapi,mashirika ya kijasusi ya uingereza yapo na ya ujerumani yapo Lakini soko la bidhaa zao Afrika mchina na mjapan wamebeba hawana Cha kufanya.Usicheze na teknlojia.Ikichange Ni ghafla na KU catch up nayo Sio kazi rahisi.Ukijaribu by the time una catch up unakuta wameshagundua kingine unaachwa barabarani
Umeandika gazeti kuuubwa hamna point ya maana. Sasa ulitaka hiyo teknolojia wawekewe wazi? Sasa kazi yao ingekua nini? Unaelewa maana intelijensia wewe?

Kama huna point kaa kimya sio unaandika ujinga!
 
Tanzania kuna watu wananifanya washauri elekezi kwa fani ambazo hawazijui
Watu wengi wanao comment wanatumia hisia zaidi,hawajui Tiss inafanyaje kazi
Tunaweza kuwa hatujui ila kukamatwa ndege na wao wamekaa tu inafanya tuone hawafanyi kazi zao vizuri. Yani watanzania wanauawa kule sauzi wao wapo tu... Viwanda vinakufa wao wamekaa tu...
 
Umeandika gazeti kuuubwa hamna point ya maana. Sasa ulitaka hiyo teknolojia wawekewe wazi? Sasa kazi yao ingekua nini? Unaelewa maana intelijensia wewe?

Kama huna point kaa kimya sio unaandika ujinga!
sawa mfano TISS wamegundua kuwa mwakani viwanda vilivyopo vya serikali teknolojia inabadilika na bidhaa zilizopo Sasa hazitakuwa na soko popote duniani Lakini gharama za kubadili teknolijia kuondoa teknolojia iliyopo na serikali kununua teknolojia mpya itagharimu serikali bajeti ya nchi ya miaka 50.Wanashauri teknolojia ibadilishwe chap chap hiyo pesa ipo? Unaongea kibwege mjinga wewe Kama bajeti haipo Ina maana viwanda lazima vife
 
Ujue mi naona kila kitu kinaenda sawa tu, tatizo la wabongo tunapenda kuona tunachokitaka sisi kiwe hapo ndipo tutaona TISS au idara husika ipo sawa..

Kwa mfano.
Umezungumzia kudhohofu kwa mchakato wa katiba.. Ukiwa unaamini kuwa kama mchakato wa katika ungekamilika basi ndio TISS wangekuwa wapo imara.. Ila mchakato umekwama unasema TISS wanayumba.. Bila kujali au kujiukiza umekwama kwa manufaa gani na ungeenda chap kungekuwa na madhara gani!! We unaamimin katika kile unachokitaka tu.

This is a mistake mkuu.

TISS wana kanuni, taratibu, mipango yao na miongozo yao katika kukamilisha majukumu yao.. Na katika nchi yoyote ile duniani katika harakat za kukamilisha mipango kuna mabaya lazima yatokee na kamwe huwez kukubalika na jamii nzima isipokiwa output yake ndio itaonekan.


Unachotakiwa kujua ni kwamba.

Maisha ya amani uliyo nayo mpaka sasa, nchi haina njaa, vita hakuna, na mengineyo ujue ni moja ya matokeo ya kazi ya TISS, vyombo vya usalama na raia wema.

Hii kukosoa kosoa ni siasa na uongeaji ambao watanzania tunao.

Nenda kenya, rwanda, uganda, burundi ndio utajua kuwa TISS na vyombo vyetu vya usalama vipo strong. Kenya wana idara zinazofanana na TISS zaid ya tatu na hii yoote ni mtengano wao na uchu wa madaraka...

Tuombee tu nchi ibaki kama ilivyo.. Wanasiasa wakikupandikiza ujinga kichwan ndio mwanzo wa upotevu wa amani.
Nakubaliana na wewe 100% mkuu👏👏

Nimefuatilia uzi wake jamaa kuanzia no.1,2 hadi 3 sijaona akielezea MAFANIKIO ya TISS zaidi ya kusema mabaya tu, ina maana hawa TISS hawana mazuri?
 
Tunaweza kuwa hatujui ila kukamatwa ndege na wao wamekaa tu inafanya tuone hawafanyi kazi zao vizuri. Yani watanzania wanauawa kule sauzi wao wapo tu... Viwanda vinakufa wao wamekaa tu...
Unajuaje kama wamekaa tu?
Kwani wanaripoti kwako?
 
Kuna mtu humu kanijibu, amani tuliyo nayo ni kwasababu ya TISS, na kwamba tunadanganywa na wana siasa. Nina jitoa, sihoji, sichangii na sisemi tena chochote kuhusu taasisi hii.
 
sawa mfano TISS wamegundua kuwa mwakani viwanda vilivyopo vya serikali teknolojia inabadilika na bidhaa zilizopo Sasa hazitakuwa na soko popote duniani Lakini gharama za kubadili teknolijia kuondoa teknolojia iliyopo na serikali kununua teknolojia mpya itagharimu serikali bajeti ya nchi ya miaka 50.Wanashauri teknolojia ibadilishwe chap chap hiyo pesa ipo? Unaongea kibwege mjinga wewe Kama bajeti haipo Ina maana viwanda lazima vife
Mkuu si kwamba nakudharau ila mbona kama uwezo wako wa kujenga na kuchambua hoja umeshuka sana? nini tatizo? siasa nyingi? ushabiki wa ccm au nini?

Kwa uwezo wako sikutarajia uwe na mawazo madogo kama haya. No offence intended but you need to change for good!!

Kila la heri.
 
Back
Top Bottom