Part 2: TISS bado safari ngumu

Part 2: TISS bado safari ngumu

Usalama wa chama kwanza!
Screenshot_20190913-131328-picsay.jpeg
 
Think tanks ni wale "wazee" wastaafu...huku wanachukulia kama tunapiga yowe tu!

Uko sahihi kabisa, hilo kundi la wazee wastaafu ndio ambalo linaamua hadi nani awe rais bila kujali box la kura linasemaje.
 
Namshauri yafuatayo Mzee wetu mzalendo nambari moja Dr Magufuli.

1. Tathimini ya kina ifanyike kwa watumishi wote wa umma kama kweli wanalipwa mshahara kulingana na majukumu yao.

2. OPRAS ya makaratasi iliyopo sasa ifanyiwe maboresho na iwe ya ki electronics ambayo mtumishi ataweza kujaza majukumu yake tarajiwa kwa mwaka wa fedha husika, utekelezaji wa majukumu kwa siku, kwa mwezi,kwa robo mwaka na hadi mwaka. ( hii itasaidia kujua uhaliasia wa mipango inayopangwa).

3.OPRAS iunganishwe na mifumo ya ya bajeti ya Serikali kuu na Serikali za mitaa ( mifumo iwasiliane).

4. Faida ya kuwa na electronic OPRAS itasaidia kutrack add hoc overtime vile vile kutrack extra duties zisizokuwa na uhalisia ambazo mara nyingi utakuta mtumishi anazidai kwa justification za uongo.

5. Kumekuwepo na tabia ya baadhi ya viongozi kupewa communication allowance kila mwezi lakini hawazitumii ipasavyo badala yake maafisa na watumishi wa kada za chini wasiopewa hizo fedha hutumia fedha zao kuwasiliana ( kuratibu) na watumishi wenzao pindi wanapohitaji kujua mambo kadhaa. Kuna haja ya Serikali kuweka system ya kutrack matumizi halisi ya hizi fedha za mawasiliano Kwa wakuu wa idara.
Kwa haya unayohitaji kuna mambo mawili yafanyike:
1. Training ya nguvu ifanyike kwa watumishi
2. Recruitment ifanyike upya kwa watumishi wa serikali
 
Majuzi wakati natizama movie ya SNOWDEN nilisikitika sana niliposikia maneno "SELF TAUGHT na NO HIGH SCHOOL DIPLOMA" wakati wa interview ya kumrecruit awe CIA Analyst.
Tunapaswa kujitizama upya kama Taifa.
Huku kwetu kazi ipo...
 
Naendelea.

Baada ya kupitia upya sheria ya usalama wa taifa.

Sheria itafanyiwa marekebisho na ufahamike wazi kwamba TISS ipo kwa ajili ya kulinda demokrasia ya bunge ikiwemo haki ya wabunge kupinga uteuzi wa mkurugenzi mkuu endapo itaonekana hana sifa.

Pia TISS inalinda maslahi ya taifa kiuchumi, kiutamaduni na kisiasa pamoja na kukabiliana na vitendo cha kigaisi, ujasusi wa kimataifa na uhujumu uchumi.

Mapendekezo ya Muundo mpya wa TISS na idara zake muhimu chini yake.

Kama nilivyosema hapo awali TISS ni Usalama wa taifa yaani National Security Organization/ Agency ambayo inaongozwa na mkurugenzi mkuu.

Naibu mkurgenzi yeye atashughulikia idara zingine khasa ya nje kwenye mabalozi, upelelezi wa ndani yaani domestic Surveillance na kuhudhuria vikao vya kamati za usalama zote za wiyala na mikoa.

TISS iwe inasimamiwa shughuli zake kwa ukaribu na kamati ya bunge la JMT ya U;inzi na Usalama na iwe inaangaliwa kwa jicho kali kwenye bajeti yake, shughuli zake na hata utaratibu wake wa kuajiri watumishi wake.

Kwa kuwa kamati ya Bunge inajumuisha wabunge kutoka vyama vyote hapo tayari ushiriki wao kuikosoa TISS unakuwa umekamilika yaani "accomplished".

Ntaendelea.

Tatizo wabunge wanakosa nguvu za kuibana TISS kwakuwa unakuta wabunge wengi wameingia kwa kubaka box la kura na hao TISS wanajua. Sasa kama wabunge wengi wanaingia kwa hujuma na rais naye anaingia madarakani kwa utata, hapo unategemea kuwa na TISS imara?
 
Naongezea tu Ofisi zote za umma ziwe zinajiwekea target na wafanyakazi wapewe ili kiwe kipi cha ufanisi wao makazini akishindwa kufikia target afukuzwe tu
Watumishi wengi ukiachana na walimu wamekuwa wakitumia muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii wakichati na wengine wakirusha picha kwenye status za WhatsApp.
Wengine utawakuta Instagram, mara Facebook huo ni muda wa kazi .
Sasa unabaki kujiuliza hivi huyu mtumishi anafanya kazi muda gani?
Na hawa ndio ikifika may mosi wananyanyua mabango wakidai kuongezewa mishahara na kupandishwa madaraja na kudai allowance mbali mbali zikiwemo house allowance, communication allowance, electricity allowance n.k.

Namshauri yafuatayo Mzee wetu mzalendo nambari moja Dr Magufuli.

1. Tathimini ya kina ifanyike kwa watumishi wote wa umma kama kweli wanalipwa mshahara kulingana na majukumu yao.

2. OPRAS ya makaratasi iliyopo sasa ifanyiwe maboresho na iwe ya ki electronics ambayo mtumishi ataweza kujaza majukumu yake tarajiwa kwa mwaka wa fedha husika, utekelezaji wa majukumu kwa siku, kwa mwezi,kwa robo mwaka na hadi mwaka. ( hii itasaidia kujua uhaliasia wa mipango inayopangwa).

3.OPRAS iunganishwe na mifumo ya ya bajeti ya Serikali kuu na Serikali za mitaa ( mifumo iwasiliane).

4. Faida ya kuwa na electronic OPRAS itasaidia kutrack add hoc overtime vile vile kutrack extra duties zisizokuwa na uhalisia ambazo mara nyingi utakuta mtumishi anazidai kwa justification za uongo.

5. Kumekuwepo na tabia ya baadhi ya viongozi kupewa communication allowance kila mwezi lakini hawazitumii ipasavyo badala yake maafisa na watumishi wa kada za chini wasiopewa hizo fedha hutumia fedha zao kuwasiliana ( kuratibu) na watumishi wenzao pindi wanapohitaji kujua mambo kadhaa. Kuna haja ya Serikali kuweka system ya kutrack matumizi halisi ya hizi fedha za mawasiliano Kwa wakuu wa idara.

6. Na mwisho kabisa nimpongeze mh Rais wetu Dr Magufuli kwa maamuzi yake ya kishujaa aliyofanya kwa kutujengea sisi watanzania wa hali ya chini hospitali za wilaya zaidi ya 60 na vituo vya afya na zahanati nyingi ndani ya miaka 4. Tena kwa fedha za ndani. Fedha ambazo zilikuwa zikipotea kwa udanganyifu mbali mbali.

Karibu kwa machango wenu wa kujenga tu na sio matusi .
 
Pole sana ndugu yangu,

TISS haiendeshwi KWA kutumia Sheria moja tu ya Usalama wa Taifa ya mwaka 1996,zipo Sheria zingine pia, Kanuni za Sheria hizi, Katika ya nchi, NA Miongozo mbalimbali ambayo hutolewa NA Kurekebishwa Mara KWA mara.

Ingawaje Kanuni za Sheria hizi (baadhi) NA miongozo yake, haziruhusiwi kuwekwa publicly, lakini ukweli unabaki kuwa Sheria hizi hazifai, mbaya, zimepitwa NA wakati.

Kinachotakiwa sasa ni kuifumua TISS yote kabisa KWA kutunga Sera mpya ya Usalama wa Taifa, Sheria NA Kanuni mpya, pamoja na Kuunda Muundo mpya kabisa wa Utendaji ktk taasisi hii. Baadhi ya mambo machache mazuri yaliyomo kwenye Sheria zilizopo hivi sasa yachukuliwe, mambo mabaya yaachwe, pia yaongezwe mambo mengine mazuri zaidi KWA mustakabali bora wa nchi yetu, ikitiliwa mkazo suala LA UJASUSI wa Kiuchumi, KWA sababu Uchumi Mbaya ktk nchi hii ndilo tatizo kubwa zaidi tulilonalo wananchi wa Tz KWA sasa. Ufukara ndiomadui yetu mkubwa.KWA sasa Watanzania wanahitaji "Ukombozi wa Kiuchumi KWA sababu Ukombozi wa Kisiasa tayari tunao, tulishaupata yangu 1961.

Hivyo basi, consultations za kutosha zinahitajika ktk mchakato mzima wa kutunga hizo Sheria mpya zitakazosimamia taasisi hii nyeti kabisa ktk nchi.

Watanzania kwa sasa Tunahitaji TISS ya " UKOMBOZI WA KIUCHUMI "

Una mawazo sahihi sana, tatizo liko ni nani wanaweza kutengeneza mfumo mpya wa TISS? Ukijaribu kuangalia sheria zinatungwa na bunge, jaribu kuangalia hao wabunge wanapatikanaje, kama tuna mfumo mbaya wa kuchagua wabunge mpaka kuweza kupata wabunge wengi walio bungeni bila ridhaa ya wananchi waliowengi, ni dhahiri hata ikiundwa sheria mpya ya TISS itakuwa ni hiyo hiyo ya kulinda maslahi ya kisiasa ya chama tawala. Ili nchi hii iweze kuwa na katiba bora kwa hapa tulipofikia ni kupindua nchi tuanze upya.
 
Mi nadhani changàmoto in mfumo mzima wa uongozi wa nchi yetu.

Yaani tumechukua ule mfumo wa kwenye familia zetu ambao unasema 'baba hakosei' na kuufanya mfumo rasmi wa uendeshaji wa serikali yetu.

Leo hii rais amekuwa mungu mtu atakalosema lazima lifanyike hta km haliko sahihi.

Hebu angalia magufuli alivyoli handle suala la katiba na uangalie waingereza walivyo handle suala la brexit, vitu viwili tofauti kbsa

Uingereza ilibidi hadi waziri mkuu ajiuzulu wakati bongo magufuli alitoa tamko tu na raia wote na bunge wakawa wamenyamazimishwa
.
Nadhani issue ni kudili na mfumo halafu hizo changamoto za toss zitakaa kwenye mstari automatic.
hahahahahahahaha jomba umenifanya nicheke sana..utafananishaje nchi ya dunia ya kwanza na dunia ya tatu..hivi unajitambua kweli..au kwa sababu unaona.mnalala nao mnawaoa na kuolewa nao mnajiona mko sawa..la hasha jomba..naomba ujue kuwa hata uingereza walivyokuwa kwenye transition period kipindi kama cha kwetu sasa , nao wali behave same way..iangalie uingereza wakati.ikiwa third world.country and not first world country..tumieni walau basi chembe tu ya akili zenu
 
Tena usishangae huo mfumo ukifumuliwa ukaja mbovu kuliko ulivyo hivi sasa. Rejea kilichotokea kwenye mchakato wa katiba mpya, rais na chama chake walijimilikisha mchakato wa katiba mpya, hadi kujipa mamlala ya kubadili maoni ya wananchi tena kwa maslahi ya chama chao. Hapo ndio usalama wa Taifa walipaswa kusimama na kusema maoni ya wananchi ndio yatumike kuunda katiba mpya.
Tunarudi kule kule..
Je watunzi watakua loyal na wenye weledi wa kujali maslahi ya watu isije ikawa tukawa tunaenda gizani zaidi ya tulipo Sasa.
 
Mleta mada safi sana!
Umesaidia kurudisha mjadala mkali sana hapa JF juu ya TISS. Zamani pamewahi kuwekwa uzi hapa JF unaoitwa TISS must reform, nadhani huo mjadala lazima uendelee ili tupate Idara nzuri yenye kuweka mbele TAIFA na siyo CCM.

Mambo yaliyofanyika nchini katika miaka minne iliyopita yanasikitisha sana kwa kweli, watu kutekwa hovyo, kupotezwa hovyo, kupigwa risasi, watu wanaotumia uhuru wao wa kutoa maoni kuonekana ni wahaini, kusakwa na kupewa cha mtema kuni, kubambikizia kesi watu, kublackmail wafanyabiashara, kufwafungulia kesi watu za uhujumu uchumi kisha wakishafanya negotiations za pembeni wanaachiwa, Kuwanyima watu dhamana kwa kesi zenye dhamana ili kuwakomoa.

Imefikia hatua mtu kazini hata kama ana sifa za utendaji, weledi lakini hapenyi kwenye mchujo/vetting ili aweze kuteuliwa na mamlaka za uteuzi kwa ajili ya kulitumikia Taifa kwenye ngazi inayohitaji huduma yake eti kwa sababu ana mrengo tofauti wa kisiasa tofauti na chama tawala.
Hakuna kesi ya maana juu ya Mafisadi kwenye mahakama za mafisadi

TISS imeshindwa kuona kuwa Teuzi zenye muelekeo wa bias za UDINI na UKANDA zinaweza kuvuruga harmony ya Taifa na ndiyo maana wametumia nguvu nyingi mno kuirudishia hadhi mamlaka ya Uraisi la Sivyo kipindi cha 2016 June hadi mwezi July 2019 kilikuwa ni kipindi kigumu mno kwa Taasisi ya Uraisi kama mtu ni mfuatiliaji wa mambo!. It seems Pesa nyingi, Propaganda nyingi zimetumika ili kurejesha imani ya umma kwa Taasisi hii. Hii yote ilikuwa haina haja kama TISS ingekuwa inafanya calculation chanya kwenye kila decision yenye maslahi ya usalama wa nchi hii!. TISS yenye kuhusika kikamilifu kwenye Teuzi imake sure watu wanaotueliwa kuserve hii nchi wamebalance demography ya Taifa la sivyo kukosekana kwa balance ya aina hiyo ipo siku itabackfire tu kwa mtawala!

Nchi Zilizoendelea kama marekani FBI na CIA zina nguvu kuliko Rais. Anapopata Urais wanamfundisha kazi, kanuni, taratibu, miiko ma mipaka. Wanamuambia nini anaweza kufanya nini hawezi au haruhusiwi kufanya. Wanaweza kumchunguza na kumhoji. Wao wanampa ripoti na maelekezo zaidi ya yeye anavyowapa ripoti na maelekezo. Yeye anawategemea wao zaidi kuliko wao wanavyomtegemea yeye. Kuna vingi hua wanamkatalia wanamuambia HILO HAPANA MZEE
 
Idara ya usalama wa taifa, ndo idara nyeti, nzito na muhimu kuliko idara zote za serikali.
Kwa hiyo panatakiwa pawe na wafanyakazi ma genius hasa ktk idara hiyo, na wasiwe na mapenzi ya chama chochote cha siasa, bali wawe na mapenzi na nchi yao tu.
Wawe wabunifu kwa ajili ya usalama wa taifa lao, usaili wa ajira ufanyike bila kuangalia kiwango cha Elimu ya mtu (kwa baadhi ya vitengo) bali uwezo, weledi, uzalendo wa nchi na akili za mtu.
Neno usalama wa taifa ni neno pana sana, naipenda sana nchi yangu Tanzania ndo maana naamini ushauri wangu kuna siku utafanyiwa kazi vilivyo.
Usalama wa taifa ni lazima wahakikishe nchi ina uchumi mzuri, kwa sababu watu wakilala njaa na kukosa mahitaji muhimu matokeo yake nchi inaweza kuingia kwenye vurugu kubwa mno na hivyo kufanya usalama kutoweka.
Ndo maana nasema hii ni idara nyeti mno, taifa lolote lenye uchumi mbovu na maisha magumu kwa watu wake ina maana pia usalama wa taifa ni dhaifu hauwezi kulinda usalama wa nchi kwa uhakika.
Kutisha watu,na kuua wapinzani ni kuzidi kupanda mbegu za chuki na bomu ambalo mwisho wa siku ni lazima lilipuke .
Kama idara ya usalama wa taifa haina kitengo cha kufanya hujuma za kiuchumi kwa mataifa ya nje kwa faida ya nchi ina maana bado kitengo ni dhaifu na kina watu ambao hawajapikwa na kuiva hasa.
Kila napokuja nyumbani Tanzania na kuangalia mazingira ya nchi yapo duni mno, vijana wengi wakishinda vijiweni hawana kazi za kufanya, huwa najiuliza nini hatima ya nchi Kama hii?
Lowassa aliwahi kusema, ukosefu wa ajira ni bomu linalosubiria kulipuka siku moja.
Basi idara ya usalama wa taifa inatakiwa ihakikishe hilo bomu halilipuki kwa gharama yoyote, ikibidi kufanya ujambazi (ujasusi) wa kiuchumi kwa mataifa ya nje na kuleta nyumbani ili watoto wale.
Urusi ilikuwa taifa la kwanza Duniani kupeleka chombo na wanaanga kwenye mwezi .
Marekani ilipoona hivyo, ikajaa wivu na ilipojaribu kwenda, chombo chao kililipuka kwa sababu ya hitilafu kwenye engine, wakajiuliza kwa nini warusi waliweza na sisi kushindwa?
Walichofanya ni kuiba teknolojia ya Urusi ya engine hadi wakafanikiwa kwenda.
Sisi tuna wivu wa kichawi, tunapigana vita ndugu kwa ndugu, hatutaki wapinzani waingie ikulu, badala ya kupigana Vita ya kumaliza umaskini, tunamalizana sisi kwa sisi.
Halafu anasimama mtu na kusema eti tutafanikiwa, tutafanikiwa kwa lipi wakati mikono yetu ina Damu za watu zinazolia kwa Mungu zikidai kisasi?
Yaani idara ya usalama wa taifa ilishuhudia kabisa viwanda zaidi ya 400 alivyoacha Mwl Nyerere vikiuliwa, lakini idara hiyo haiko tayari kushuhudia mkosoaji wa serikali akisimama hadharani na kuikosoa serikali ,labda awe nyuma ya keyboard Kama mimi hapa

INAENDELEA
Watu Kama wewe wako wengi sana nchini , watu wanao chambua sekta moja moja kuwa ndio tatizo linalosababisha kuwa hapa tulipo Kama taifa. Haujakosea ,Ila ulichoandika ni sehemu tu ya tatizo ,hebu jaribu kujiuliza sisi kama taifa lenye karibu kila kitu tumefanikiwa japo nini kwa mfano? Je tumefanikiwa ikatika elimu? Afya? Au miundo mbinu ?? Jibu utakuta ni hapana hatujafanikiwa lolote si kilimo, si afya ,si elimu, siuchimbaji wa madini au japo michezo. Ni kama mwanafunzi mwenye uwezo wa kupata 90% anapata 10,12 nk
Kwa hiyo tatizo si TISS pekee. Tatizo ni kubwa zaidi ya TISS. Mfano rahisi, ukiwa na mfumo Wa elimu duni, je utapata TISS yenye weledi? Tatizo ni kubwa hata kuwepo tu Kwa sisi Kama Tanzania ni Tatizo,ongeza uasisi Wa taifa lenyewe , misingi yake, male go yetu Kama taifa nk nk....itaendelea
 
Watu Kama wewe wako wengi sana nchini , watu wanao chambua sekta moja moja kuwa ndio tatizo linalosababisha kuwa hapa tulipo Kama taifa. Haujakosea ,Ila ulichoandika ni sehemu tu ya tatizo ,hebu jaribu kujiuliza sisi kama taifa lenye karibu kila kitu tumefanikiwa japo nini kwa mfano? Je tumefanikiwa ikatika elimu? Afya? Au miundo mbinu ?? Jibu utakuta ni hapana hatujafanikiwa lolote si kilimo, si afya ,si elimu, siuchimbaji wa madini au japo michezo. Ni kama mwanafunzi mwenye uwezo wa kupata 90% anapata 10,12 nk
Kwa hiyo tatizo si TISS pekee. Tatizo ni kubwa zaidi ya TISS. Mfano rahisi, ukiwa na mfumo Wa elimu duni, je utapata TISS yenye weledi? Tatizo ni kubwa hata kuwepo tu Kwa sisi Kama Tanzania ni Tatizo,ongeza uasisi Wa taifa lenyewe , misingi yake, male go yetu Kama taifa nk nk....itaendelea

Lete suluhisho badala ya kutetea udhaifu kwa kuleta udhaifu wa maeneo na sekta nyingine.
 
Tatizo hii nchi kuna kundi la watu ni kama vile wameshajipa hatimiliki ya kuingoza na kuiendesha nchi hii watakavyo bila kujali kuwa nchii ni yetu sote na hakuna mtu mwenye haki zaidi ya mwenzake.

Nchii hii siasa ina nguvu kuliko kitu kingine, na kwa bahati sana siasa yenyewe inatumika kunufaisha kundi fulani tu la watu ambao ni wachache.

Na kundi hilo la watu wenye nguvu kisiasa wamekuwa wakizitumia taasisi zote kwa ajili ya manufaa yao hata zile zisizostahili kuingiliwa na siasa hata kidogo.

TISS ilipaswa kuwa taasisi huru kabisa kama zilivyo MOSSAD,KGB,CIA,ISI n.k

Leo hii CIA wana uwezo wa kumnyima Raisi Trump taarifa muhimu za kiusalama na Trump asifanye chochote sababu ni taasisi ambayo iko huru inayojitegemea hakuna mtu ambaye yuko juu ya taasisi hiyo iko kwa ajili ya kuhakikisha taifa liko salama. Na ina jukumu hata la kumchunguza Trump mwenyewe

Kwetu sisi hapa ni kinyume chake, taasisi tunayoiona ndio ya kulinda usalama wa taifa letu haiko huru, kuna watu ambao wanai control kupitia nguvu ya kisiasa waliyonayo na inafuata maagizo yao.

Kitendo cha TISS kuwa chini ya raisi(mwana siasa) ni sawa tu kusema usalama wa taifa letu huko chini ya raisi maana yeye ndio anaye teuwa viongozi wa taasisi hiyo, na ni rahisi sana kuitumia taasisi hiyo kwa maslahi yake binafsi. Na siku akitokea mjanja akamzidi akili(japo kwa stori za hapa na pale tayari mjanja huyu yupo) akamrubuni raisi wetu usalama wa taifa letu utakuwa hatarini sana.

TISS haina tena credibility kutoka na matokeo kadhaa ya kinyama ambayo imekuwa ikihusishwa nayo na hili limewezekana baada ya kuwepo kwa mwanya wa kuingiliwa kisiasa.

TISS ni jipu kubwa mno na Mwarobaini pekee ni kutunga sheria mpyaa zinahusu hii taasisi kwanzia uundwaji wake mpaka utekelezaji. Na hizo sheria yapaswa ziende sawia na mabadiliko ya katiba.
 
Haya tumeyajadili sana tangu enzi ya kikwete tukiwa nbele ba yericko ambYe yeye aliamua kuyaamishia kwenye kitabu.

Idara haiwez kubadilikA km unavyofikir wewe,

Idara ili ibadilike inahitaji mtu mmpja kwanza wa kubeba wazo km n raisi au mwingine ambaye atahakikisha anatengeneza vision itakayotekelezwa hata km yeye hayupo n kubwa huwa n budget n anaitoa nani hivyo jasusi humhudumia anayemlipa,
Kisha badili sheria mbovu iliyopo ya 1996 shida n marais hawaoni muda wa kutosha kuijenga taasisi hii.

Km rais hataamua kuibadili haitobadilika na km ss tutahitaji
ibadilike pesa yake isitoke kwa rais ili DG MWENYEWE HAItengeneze taasisi kupitia wasaidiz ba waandamiz chini ya msukumo wa baraza au bunge au kamati yake.
Iwe independently km CAG hapa tz lkn tulinde kwa nguvu uteuz wa DG kuanzia sifa hadi muda wa madaraka.


Km mtaelewa tuipindue nchi tuimarishe hili ili my son uweze kunywa maji ukiwa tz
 
hahahahahahahaha jomba umenifanya nicheke sana..utafananishaje nchi ya dunia ya kwanza na dunia ya tatu..hivi unajitambua kweli..au kwa sababu unaona.mnalala nao mnawaoa na kuolewa nao mnajiona mko sawa..la hasha jomba..naomba ujue kuwa hata uingereza walivyokuwa kwenye transition period kipindi kama cha kwetu sasa , nao wali behave same way..iangalie uingereza wakati.ikiwa third world.country and not first world country..tumieni walau basi chembe tu ya akili zenu
acha visingizio ...ghana ni third world country km tulivyo sie, lakini hawana system km za kwetu za kumfanya rais mungu mtu.
 
Richard kwakuwa ww una namba ya Diwani Athumani, mwambie aje huku jf kuna mjadala wa ofisi yake mpya, aje apate mitazamo ya wadau.

Hapana mii sina namba ya Diwani Athumani.

Ila nafikiri atakuwa anapita humu.
 
Back
Top Bottom