Part 2: TISS bado safari ngumu

My Son drink water

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
4,932
13,283
Idara ya usalama wa taifa, ndo idara nyeti, nzito na muhimu kuliko idara zote za serikali.

Kwa hiyo panatakiwa pawe na wafanyakazi ma genius hasa ktk idara hiyo, na wasiwe na mapenzi ya chama chochote cha siasa, bali wawe na mapenzi na nchi yao tu.

Wawe wabunifu kwa ajili ya usalama wa taifa lao, usaili wa ajira ufanyike bila kuangalia kiwango cha Elimu ya mtu (kwa baadhi ya vitengo) bali uwezo, weledi, uzalendo wa nchi na akili za mtu.

Neno “Usalama wa Taifa” ni neno pana sana, naipenda sana nchi yangu Tanzania ndo maana naamini ushauri wangu kuna siku utafanyiwa kazi vilivyo.

Usalama wa taifa ni lazima wahakikishe nchi ina uchumi mzuri, kwa sababu watu wakilala njaa na kukosa mahitaji muhimu matokeo yake nchi inaweza kuingia kwenye vurugu kubwa mno na hivyo kufanya usalama kutoweka.

Ndo maana nasema hii ni idara nyeti mno, taifa lolote lenye uchumi mbovu na maisha magumu kwa watu wake ina maana pia usalama wa taifa ni dhaifu hauwezi kulinda usalama wa nchi kwa uhakika.

Kutisha watu,na kuua wapinzani ni kuzidi kupanda mbegu za chuki na bomu ambalo mwisho wa siku ni lazima lilipuke.

Kama idara ya Usalama wa Taifa haina kitengo cha kufanya hujuma za kiuchumi kwa mataifa ya nje kwa faida ya nchi ina maana bado kitengo ni dhaifu na kina watu ambao hawajapikwa na kuiva hasa.

Kila napokuja nyumbani Tanzania na kuangalia mazingira ya nchi yapo duni mno, vijana wengi wakishinda vijiweni hawana kazi za kufanya, huwa najiuliza nini hatima ya nchi Kama hii? Lowassa aliwahi kusema, ukosefu wa ajira ni bomu linalosubiria kulipuka siku moja.

Basi idara ya Usalama wa Taifa inatakiwa ihakikishe hilo bomu halilipuki kwa gharama yoyote, ikibidi kufanya ujambazi (ujasusi) wa kiuchumi kwa mataifa ya nje na kuleta nyumbani ili watoto wale.

Urusi ilikuwa taifa la kwanza Duniani kupeleka chombo na wanaanga kwenye mwezi.

Marekani ilipoona hivyo, ikajaa wivu na ilipojaribu kwenda, chombo chao kililipuka kwa sababu ya hitilafu kwenye engine, wakajiuliza kwa nini warusi waliweza na sisi kushindwa?

Walichofanya ni kuiba teknolojia ya Urusi ya engine hadi wakafanikiwa kwenda.

Sisi tuna wivu wa kichawi, tunapigana vita ndugu kwa ndugu, hatutaki wapinzani waingie ikulu, badala ya kupigana Vita ya kumaliza umaskini, tunamalizana sisi kwa sisi.

Halafu anasimama mtu na kusema eti tutafanikiwa, tutafanikiwa kwa lipi wakati mikono yetu ina Damu za watu zinazolia kwa Mungu zikidai kisasi?

Yaani idara ya Usalama wa Taifa ilishuhudia kabisa viwanda zaidi ya 400 alivyoacha Mwl Nyerere vikiuliwa, lakini idara hiyo haiko tayari kushuhudia mkosoaji wa serikali akisimama hadharani na kuikosoa serikali ,labda awe nyuma ya keyboard Kama mimi hapa

INAENDELEA

Tatizo ni wanasiasa kuingilia taasisi badala ya kuziache zifanye kazi zake kitalaamu.

Sio TISS tu ambayo ni tatizo/inalalamikiwa, bali hata vyombo kama Bunge,Mahakama na vinginevyo vingi navyo vinalalamikiwa kufanya kazi kwa kufuata matakwa ya wanasiasa badala ya weledi.
 
OK kwa hiyo unashauri tukisome vizuri kitabu cha Yerico Nyerere

Yeriko Nyerere ameyaandika hayo yote kwenye kitabu chake

Mkuu umewahi kukisoma kitabu cha ujasusi cha Yeriko

Angeruhusu ningekipandisha hapa Jukwaani ni kitabu kizuri sana

Try to read, Soma page zinazokuhusu kila kitu kipo kwenye kitabu
 
Mkuu hata kabla ya Yericko kuandika hicho kitabu mimi nalijua hilo
 
*Itafika siku watatamani kuurudisha muda nyuma ili wayafanyie kazi maoni walioyaona mabazu na muda hautakuwa upande wao....Mungu jaalia hili lisitokee kwa kuwapa usikivu viongozi wetu*
 
Watumishi wengi ukiachana na walimu wamekuwa wakitumia muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii wakichati na wengine wakirusha picha kwenye status za WhatsApp.
Wengine utawakuta Instagram, mara Facebook huo ni muda wa kazi .
Sasa unabaki kujiuliza hivi huyu mtumishi anafanya kazi muda gani?
Na hawa ndio ikifika may mosi wananyanyua mabango wakidai kuongezewa mishahara na kupandishwa madaraja na kudai allowance mbali mbali zikiwemo house allowance, communication allowance, electricity allowance n.k.

Namshauri yafuatayo Mzee wetu mzalendo nambari moja Dr Magufuli.

1. Tathimini ya kina ifanyike kwa watumishi wote wa umma kama kweli wanalipwa mshahara kulingana na majukumu yao.

2. OPRAS ya makaratasi iliyopo sasa ifanyiwe maboresho na iwe ya ki electronics ambayo mtumishi ataweza kujaza majukumu yake tarajiwa kwa mwaka wa fedha husika, utekelezaji wa majukumu kwa siku, kwa mwezi,kwa robo mwaka na hadi mwaka. ( hii itasaidia kujua uhaliasia wa mipango inayopangwa).

3.OPRAS iunganishwe na mifumo ya ya bajeti ya Serikali kuu na Serikali za mitaa ( mifumo iwasiliane).

4. Faida ya kuwa na electronic OPRAS itasaidia kutrack add hoc overtime vile vile kutrack extra duties zisizokuwa na uhalisia ambazo mara nyingi utakuta mtumishi anazidai kwa justification za uongo.

5. Kumekuwepo na tabia ya baadhi ya viongozi kupewa communication allowance kila mwezi lakini hawazitumii ipasavyo badala yake maafisa na watumishi wa kada za chini wasiopewa hizo fedha hutumia fedha zao kuwasiliana ( kuratibu) na watumishi wenzao pindi wanapohitaji kujua mambo kadhaa. Kuna haja ya Serikali kuweka system ya kutrack matumizi halisi ya hizi fedha za mawasiliano Kwa wakuu wa idara.

6. Na mwisho kabisa nimpongeze mh Rais wetu Dr Magufuli kwa maamuzi yake ya kishujaa aliyofanya kwa kutujengea sisi watanzania wa hali ya chini hospitali za wilaya zaidi ya 60 na vituo vya afya na zahanati nyingi ndani ya miaka 4. Tena kwa fedha za ndani. Fedha ambazo zilikuwa zikipotea kwa udanganyifu mbali mbali.

Karibu kwa machango wenu wa kujenga tu na sio matusi .
 
Hiyo yatakiwa iwe ni ajenda ya taifa na kwa maslahi ya taifa.

Hiyo ni pamoja na mawaziri wa ulinzi na mambo ya ndani kukutana na kujadili namna ya kuipitia upya sera ya usalama wa taifa.

Usalama wa taifa usiwe unajihusisha na masuala ya kisiasa.

Hapo ndipo penye tatizo kubwa la TISS, inatuhumiwa kujihusisha na matukio au matokeo ya kisiasa.
 
Haya yote tiss inapaswa kuyafuatilia na kuhakikisha hata shilingi ya Serikali haipotei bure,

Mtu anapolipwa mshahara bure ina maana miundombinu haitajengwa ili ifaidishe taifa Kwa ujumla kiuchumi na kijamii.

Watumishi wengi ukiachana na walimu wamekuwa wakitumia muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii wakichati na wengine wakirusha picha kwenye status za WhatsApp.
Wengine utawakuta Instagram, mara Facebook huo ni muda wa kazi .
Sasa unabaki kujiuliza hivi huyu mtumishi anafanya kazi muda gani?
Na hawa ndio ikifika may mosi wananyanyua mabango wakidai kuongezewa mishahara na kupandishwa madaraja na kudai allowance mbali mbali zikiwemo house allowance, communication allowance, electricity allowance n.k.

Namshauri yafuatayo Mzee wetu mzalendo nambari moja Dr Magufuli.

1. Tathimini ya kina ifanyike kwa watumishi wote wa umma kama kweli wanalipwa mshahara kulingana na majukumu yao.

2. OPRAS ya makaratasi iliyopo sasa ifanyiwe maboresho na iwe ya ki electronics ambayo mtumishi ataweza kujaza majukumu yake tarajiwa kwa mwaka wa fedha husika, utekelezaji wa majukumu kwa siku, kwa mwezi,kwa robo mwaka na hadi mwaka. ( hii itasaidia kujua uhaliasia wa mipango inayopangwa).

3.OPRAS iunganishwe na mifumo ya ya bajeti ya Serikali kuu na Serikali za mitaa ( mifumo iwasiliane).

4. Faida ya kuwa na electronic OPRAS itasaidia kutrack add hoc overtime vile vile kutrack extra duties zisizokuwa na uhalisia ambazo mara nyingi utakuta mtumishi anazidai kwa justification za uongo.

5. Kumekuwepo na tabia ya baadhi ya viongozi kupewa communication allowance kila mwezi lakini hawazitumii ipasavyo badala yake maafisa na watumishi wa kada za chini wasiopewa hizo fedha hutumia fedha zao kuwasiliana ( kuratibu) na watumishi wenzao pindi wanapohitaji kujua mambo kadhaa. Kuna haja ya Serikali kuweka system ya kutrack matumizi halisi ya hizi fedha za mawasiliano Kwa wakuu wa idara.

6. Na mwisho kabisa nimpongeze mh Rais wetu Dr Magufuli kwa maamuzi yake ya kishujaa aliyofanya kwa kutujengea sisi watanzania wa hali ya chini hospitali za wilaya zaidi ya 60 na vituo vya afya na zahanati nyingi ndani ya miaka 4. Tena kwa fedha za ndani. Fedha ambazo zilikuwa zikipotea kwa udanganyifu mbali mbali.

Karibu kwa machango wenu wa kujenga tu na sio matusi .
 
Watumishi wengi ukiachana na walimu wamekuwa wakitumia muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii wakichati na wengine wakirusha picha kwenye status za WhatsApp.
Wengine utawakuta Instagram, mara Facebook huo ni muda wa kazi .
Sasa unabaki kujiuliza hivi huyu mtumishi anafanya kazi muda gani?
Na hawa ndio ikifika may mosi wananyanyua mabango wakidai kuongezewa mishahara na kupandishwa madaraja na kudai allowance mbali mbali zikiwemo house allowance, communication allowance, electricity allowance n.k.

Namshauri yafuatayo Mzee wetu mzalendo nambari moja Dr Magufuli.

1. Tathimini ya kina ifanyike kwa watumishi wote wa umma kama kweli wanalipwa mshahara kulingana na majukumu yao.

2. OPRAS ya makaratasi iliyopo sasa ifanyiwe maboresho na iwe ya ki electronics ambayo mtumishi ataweza kujaza majukumu yake tarajiwa kwa mwaka wa fedha husika, utekelezaji wa majukumu kwa siku, kwa mwezi,kwa robo mwaka na hadi mwaka. ( hii itasaidia kujua uhaliasia wa mipango inayopangwa).

3.OPRAS iunganishwe na mifumo ya ya bajeti ya Serikali kuu na Serikali za mitaa ( mifumo iwasiliane).

4. Faida ya kuwa na electronic OPRAS itasaidia kutrack add hoc overtime vile vile kutrack extra duties zisizokuwa na uhalisia ambazo mara nyingi utakuta mtumishi anazidai kwa justification za uongo.

5. Kumekuwepo na tabia ya baadhi ya viongozi kupewa communication allowance kila mwezi lakini hawazitumii ipasavyo badala yake maafisa na watumishi wa kada za chini wasiopewa hizo fedha hutumia fedha zao kuwasiliana ( kuratibu) na watumishi wenzao pindi wanapohitaji kujua mambo kadhaa. Kuna haja ya Serikali kuweka system ya kutrack matumizi halisi ya hizi fedha za mawasiliano Kwa wakuu wa idara.

6. Na mwisho kabisa nimpongeze mh Rais wetu Dr Magufuli kwa maamuzi yake ya kishujaa aliyofanya kwa kutujengea sisi watanzania wa hali ya chini hospitali za wilaya zaidi ya 60 na vituo vya afya na zahanati nyingi ndani ya miaka 4. Tena kwa fedha za ndani. Fedha ambazo zilikuwa zikipotea kwa udanganyifu mbali mbali.

Karibu kwa machango wenu wa kujenga tu na sio matusi .
Hio ari yenyewe ya kufanya kazi wanaitoa wapi bana kwa hali hii?? Si bora wachat tu waondoe stress.
 
Kazi wanapeana ndani ya CCM tena kiundugu, wao kwao lakini bado wanapendeleana ndiyo itakuwa watanzania wote
 
Wiki hii TISS imetrend, boss mpya, wa zamani etc

Kwani TISS ina kazi gani hasa na nini tofauti yake na polisi na wanajeshi wanaolinda usalama wetu raia.
 
Mi nadhani changàmoto in mfumo mzima wa uongozi wa nchi yetu.

Yaani tumechukua ule mfumo wa kwenye familia zetu ambao unasema 'baba hakosei' na kuufanya mfumo rasmi wa uendeshaji wa serikali yetu.

Leo hii rais amekuwa mungu mtu atakalosema lazima lifanyike hta km haliko sahihi.

Hebu angalia magufuli alivyoli handle suala la katiba na uangalie waingereza walivyo handle suala la brexit, vitu viwili tofauti kbsa

Uingereza ilibidi hadi waziri mkuu ajiuzulu wakati bongo magufuli alitoa tamko tu na raia wote na bunge wakawa wamenyamazimishwa
.
Nadhani issue ni kudili na mfumo halafu hizo changamoto za toss zitakaa kwenye mstari automatic.
 
Watumishi wengi ukiachana na walimu wamekuwa wakitumia muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii wakichati na wengine wakirusha picha kwenye status za WhatsApp.
Wengine utawakuta Instagram, mara Facebook huo ni muda wa kazi .
Sasa unabaki kujiuliza hivi huyu mtumishi anafanya kazi muda gani?
Na hawa ndio ikifika may mosi wananyanyua mabango wakidai kuongezewa mishahara na kupandishwa madaraja na kudai allowance mbali mbali zikiwemo house allowance, communication allowance, electricity allowance n.k.

Namshauri yafuatayo Mzee wetu mzalendo nambari moja Dr Magufuli.

1. Tathimini ya kina ifanyike kwa watumishi wote wa umma kama kweli wanalipwa mshahara kulingana na majukumu yao.

2. OPRAS ya makaratasi iliyopo sasa ifanyiwe maboresho na iwe ya ki electronics ambayo mtumishi ataweza kujaza majukumu yake tarajiwa kwa mwaka wa fedha husika, utekelezaji wa majukumu kwa siku, kwa mwezi,kwa robo mwaka na hadi mwaka. ( hii itasaidia kujua uhaliasia wa mipango inayopangwa).

3.OPRAS iunganishwe na mifumo ya ya bajeti ya Serikali kuu na Serikali za mitaa ( mifumo iwasiliane).

4. Faida ya kuwa na electronic OPRAS itasaidia kutrack add hoc overtime vile vile kutrack extra duties zisizokuwa na uhalisia ambazo mara nyingi utakuta mtumishi anazidai kwa justification za uongo.

5. Kumekuwepo na tabia ya baadhi ya viongozi kupewa communication allowance kila mwezi lakini hawazitumii ipasavyo badala yake maafisa na watumishi wa kada za chini wasiopewa hizo fedha hutumia fedha zao kuwasiliana ( kuratibu) na watumishi wenzao pindi wanapohitaji kujua mambo kadhaa. Kuna haja ya Serikali kuweka system ya kutrack matumizi halisi ya hizi fedha za mawasiliano Kwa wakuu wa idara.

6. Na mwisho kabisa nimpongeze mh Rais wetu Dr Magufuli kwa maamuzi yake ya kishujaa aliyofanya kwa kutujengea sisi watanzania wa hali ya chini hospitali za wilaya zaidi ya 60 na vituo vya afya na zahanati nyingi ndani ya miaka 4. Tena kwa fedha za ndani. Fedha ambazo zilikuwa zikipotea kwa udanganyifu mbali mbali.

Karibu kwa machango wenu wa kujenga tu na sio matusi .
Ina maana Mkuu hujajua tatizo lilipo mpaka kupendekeza yote haya?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom