Part 2: TISS bado safari ngumu

Part 2: TISS bado safari ngumu

Idara ya usalama wa taifa, ndo idara nyeti, nzito na muhimu kuliko idara zote za serikali.
Kwa hiyo panatakiwa pawe na wafanyakazi ma genius hasa ktk idara hiyo, na wasiwe na mapenzi ya chama chochote cha siasa, bali wawe na mapenzi na nchi yao tu.
Wawe wabunifu kwa ajili ya usalama wa taifa lao, usaili wa ajira ufanyike bila kuangalia kiwango cha Elimu ya mtu (kwa baadhi ya vitengo) bali uwezo, weledi, uzalendo wa nchi na akili za mtu.
Neno usalama wa taifa ni neno pana sana, naipenda sana nchi yangu Tanzania ndo maana naamini ushauri wangu kuna siku utafanyiwa kazi vilivyo.
Usalama wa taifa ni lazima wahakikishe nchi ina uchumi mzuri, kwa sababu watu wakilala njaa na kukosa mahitaji muhimu matokeo yake nchi inaweza kuingia kwenye vurugu kubwa mno na hivyo kufanya usalama kutoweka.
Ndo maana nasema hii ni idara nyeti mno, taifa lolote lenye uchumi mbovu na maisha magumu kwa watu wake ina maana pia usalama wa taifa ni dhaifu hauwezi kulinda usalama wa nchi kwa uhakika.
Kutisha watu,na kuua wapinzani ni kuzidi kupanda mbegu za chuki na bomu ambalo mwisho wa siku ni lazima lilipuke .
Kama idara ya usalama wa taifa haina kitengo cha kufanya hujuma za kiuchumi kwa mataifa ya nje kwa faida ya nchi ina maana bado kitengo ni dhaifu na kina watu ambao hawajapikwa na kuiva hasa.
Kila napokuja nyumbani Tanzania na kuangalia mazingira ya nchi yapo duni mno, vijana wengi wakishinda vijiweni hawana kazi za kufanya, huwa najiuliza nini hatima ya nchi Kama hii?
Lowassa aliwahi kusema, ukosefu wa ajira ni bomu linalosubiria kulipuka siku moja.
Basi idara ya usalama wa taifa inatakiwa ihakikishe hilo bomu halilipuki kwa gharama yoyote, ikibidi kufanya ujambazi (ujasusi) wa kiuchumi kwa mataifa ya nje na kuleta nyumbani ili watoto wale.
Urusi ilikuwa taifa la kwanza Duniani kupeleka chombo na wanaanga kwenye mwezi .
Marekani ilipoona hivyo, ikajaa wivu na ilipojaribu kwenda, chombo chao kililipuka kwa sababu ya hitilafu kwenye engine, wakajiuliza kwa nini warusi waliweza na sisi kushindwa?
Walichofanya ni kuiba teknolojia ya Urusi ya engine hadi wakafanikiwa kwenda.
Sisi tuna wivu wa kichawi, tunapigana vita ndugu kwa ndugu, hatutaki wapinzani waingie ikulu, badala ya kupigana Vita ya kumaliza umaskini, tunamalizana sisi kwa sisi.
Halafu anasimama mtu na kusema eti tutafanikiwa, tutafanikiwa kwa lipi wakati mikono yetu ina Damu za watu zinazolia kwa Mungu zikidai kisasi?
Yaani idara ya usalama wa taifa ilishuhudia kabisa viwanda zaidi ya 400 alivyoacha Mwl Nyerere vikiuliwa, lakini idara hiyo haiko tayari kushuhudia mkosoaji wa serikali akisimama hadharani na kuikosoa serikali ,labda awe nyuma ya keyboard Kama mimi hapa

INAENDELEA
Nyuma ya keyboard pia tunafika mkuu... Kuwa makini tu.. Simamia hapo hapo ulipo ukitoka nnje ya mstari utawajibishwa pia.

Moja ya vitisho vya usalama ni upingaji wa utendaji wa wanausalama.

Tuendelee part 3 tupo pamoja mkuu
 
Haya mambo ni pasua kichwa! Ningetamani hiyo idara iwe chungu cha maarifa na suluhu za kitaifa.

Hebu rejea kuhusu katiba, Rais A ana ruhusu mchakato wa maboresho ya katiba, mara umeishia njiani, mara Rais B anaamuru sio suala la kipaumbele, mchakato usiendelee.

Jiulize, lilipokuwa suala la kipaumbele vigezo gani vilitumika?

Mchakato wa katiba na yaliyotokea ni mfano tu. Huwa najiuliza, nafasi ya raia kuonesha kutoridhishwa kwao iwe ni kwa njia ya kura tu?

Nini nafasi ya TISS kwa maamuzi ya vyombo vikuu yanayo fanana na kulamba sumu?

Tuendelea kukua na kujifunza, tutafikia ukomavu hatua kwa hatua.
Ujue mi naona kila kitu kinaenda sawa tu, tatizo la wabongo tunapenda kuona tunachokitaka sisi kiwe hapo ndipo tutaona TISS au idara husika ipo sawa..

Kwa mfano.
Umezungumzia kudhohofu kwa mchakato wa katiba.. Ukiwa unaamini kuwa kama mchakato wa katika ungekamilika basi ndio TISS wangekuwa wapo imara.. Ila mchakato umekwama unasema TISS wanayumba.. Bila kujali au kujiukiza umekwama kwa manufaa gani na ungeenda chap kungekuwa na madhara gani!! We unaamimin katika kile unachokitaka tu.

This is a mistake mkuu.

TISS wana kanuni, taratibu, mipango yao na miongozo yao katika kukamilisha majukumu yao.. Na katika nchi yoyote ile duniani katika harakat za kukamilisha mipango kuna mabaya lazima yatokee na kamwe huwez kukubalika na jamii nzima isipokiwa output yake ndio itaonekan.

Unachotakiwa kujua ni kwamba.

Maisha ya amani uliyo nayo mpaka sasa, nchi haina njaa, vita hakuna, na mengineyo ujue ni moja ya matokeo ya kazi ya TISS, vyombo vya usalama na raia wema.

Hii kukosoa kosoa ni siasa na uongeaji ambao watanzania tunao.

Nenda kenya, rwanda, uganda, burundi ndio utajua kuwa TISS na vyombo vyetu vya usalama vipo strong. Kenya wana idara zinazofanana na TISS zaid ya tatu na hii yoote ni mtengano wao na uchu wa madaraka...

Tuombee tu nchi ibaki kama ilivyo.. Wanasiasa wakikupandikiza ujinga kichwan ndio mwanzo wa upotevu wa amani.
 
Yaani unaangalia nguvu ya TISS kwa kujilinganisha na nchi kama Rwanda, Uganda na Burundi: Hivi wewe kweli ni mzima huko kichwani ??? Nikikuuliza kwamba hawa majirani wana hatari gani kwa Tanzania nina uhakika huwezi kunipa jawabu linaloeleweka.

Uimara wa TISS inabidi tuupime kwa kuangalia ni kwa kiwango gani wamefanikiwa kuilinda nchi dhidi ya maadui wakubwa walioko nje ya mipaka. Pia kuiletea nchi faida kubwa za kiuchumi ili kuondoa umasikini kupitia mapinduzi ya sayansi na teknolojia, uwekezaji kutoka nje na biashara za kimataifa ambavyo ni sehemu ya Sera ya mambo ya nje ya Tanzania.

Una matatizo makubwa sana bwana mdogo: Kila nikiwaza kwamba Tanzania imejaa vijana wanaofikiri kama wewe huwa nahuzunika sana.
 
Its only when a mosquito lands on your testicles, that you realize there is always a way to solve problems without using violence.
 
Umesoma andiko ukiwa na jawabu lako na mawazo yako kichwani unayoyataka na kuyaamini wewe....

Alafu ukasoma huku ukijichukulia we ndio mjuaji wa kila kitu kwa iyo huna geni la kuliskia...

Endelea hvyo tu mkuu.

Tutakuamini kwa kila jambo.. Nyie ndio watu tunaowategemea wa kupiga porojo nyuma ya keyboard.. Safi saana.

Ila kama utajiskia au utakuwa na mida soma vizur tu kipande nlichotaka warundi... Alafu utaona kama nimesema warundi wana threat kwao au kwetu.

Next time utumie zaid ubongo katika kusoma na kuelewa... Usitumie hisia na viungo vingine vya mwili.

Nahisi ni nchi yako tu pekee ndio inathreat katika ukanda wa africa.. Na we ndio unazijua izo threat... Ukitulia watajie watu pia wazifahamu.

Vipi kuhusu Bomba la Mafuta. Mbona walishindwa kubaini hatari na athari za mradi mpaka pale wazungu wanatutia hasara?. Kuna sehemu hawa TISS wanakosea na wanashindwa kuwa mbele ya matukio ya hatari kwa taifa letu, na hali ikiendelea kama hivi tutakuwa ni wa kupata hasara katika kila tukio.
Hebu tuzingatie ushauri wako "Its only when a mosquito lands on your testicles, that you realize there is always a way to solve problems without using violence."
 
Mkuu wa nchi anasema anapambana vita hatari ya Uchumi na wenye akili timamu tunaiona na kufahamu tunapambana na adui gani: Wewe ni nani hapa nchini hadi utake kutuaminisha kwamba tuko salama ??? Who are you ! Acha umalaya wa kisiasa!
 
Toka tu offkey ni kawaida ya mtu anayekurupuka... Mara mkuu wa nchi anapambana na vita ya uchumi, mara tiss hawana kazi...

Basi mkuu wa nchi yuko na wewe ndio mnapambana.

Unasema niache siasa sasa sijui kama kuna sehem umeona nimeongelea siasa...

Hulka ya nini... Tulia tu jenga hoja watu watasoma na watakuelewa... Hauna haja ya kusingizia mambo na kutoka offkey kuongea vitu tofauti.

Utakachokiandika kitatosha saana kuelezea we ni mtu wa aina gani... Hata ukipanic hakuna anayekuona zaid ya ulio nao karibu huko ulipo..

Tuliza akili tu utaelewa mleta mada anataka nin, niliyemquote mimi alisema nin na wewe unakiandika nin!!

Mihemko haina faida kwako kijana. Unajivunjia tu.

Mkuu, wanaotunga Sera ya mambo ya nje ya Tanzania pamoja na kumshauri Raisi juu ya utekelezaji wake ni hawa ndugu zetu wa TISS, wakishirikiana na wizara mbalimbali hasahasa zile za mambo ya nje na ulinzi pamoja na jeshi la wananchi. Sasa ukijiuliza swali rahisi kabisa ni kwa kiwango gani tumeweza kutekeleza sera mpya ya mambo ya nje ya Tanzania, utabakia ukisikitika.

Sera ya kwanza ya mambo ya nje ya Tanzania ilitangazwa na Mzee Nyerere miaka ya 1960's mbele ya mabalozi wa nchi za nje na ilijikita kwenye mambo yafuatayo:

Mosi, kutengeneza Tanzania huru isiyofungamana na kambi yotote ile ya vita baridi, ili kuipesha Tanzania isiingie kwenye machafuko kama yale ya Zaire, Vietnam na Korea.

Pili, kupigania uhuru wa nchi za Afrika, hasahasa zile zinaziozunguka Tanzania na kuhakikisha zinakuwa ndani ya ushawishi wa Tanzania. Mfano Msumbiji, Angola, Uganda, Namibia, Afrika Kusini, Zimbabwe, Lesotho, Zambia, Malawi na Botswana.

Tatu, kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika kukabili changamoto za amani ulimwenguni.

Nne, kupambana na ushawishi wa Kizayuni barani Afrika, pamoja na kuzuia kusambaa kwa ushawishi wa Serikali ya Kikabulu ya Afrika Kusini.

Sasa kazi za TISS zilikuwa zikizunguka kwenye mhimili huo tokea mwaka 1976 hadi 1989 baada ya kuisha kwa vita baridi na 1991 baada ya umoja wa kisovieti kuanguka. Katika malengo yote ya Sera ya mambo ya nje TISS walifanya kazi katika weledi mkubwa sana kwasababu waliweza kuyatimiza hayo malengo kwa asilimia 90%.

TISS ilituvusha salama kipindi chote cha vita baridi, japo uchumi ulikuwa mbaya lakini kama nchi tulikuwa na mwelekeo mzuri sana kama tungefanya mabadiliko ya kiuchumi vizuri, kitaalamu na taratibu hasa kipindi cha mfumo wa soko huria.

Miaka ya karibuni tulirekebisha sera yetu ya mambo ya nje, na kujikita kwenye diplomasia ya kiuchumi ambayo tokea kipindi cha Mkapa tulichofanikisha ni kufutiwa madeni makubwa ya nje, kufufua Jumuiya ya Afrika Mashariki, Kuimarisha SADC, kuleta uwekezaji mkubwa wa nje ambao kwa namna moja au nyingine haukuwa na maslahi makubwa kwa taifa letu.

Sasa kabla ya kuzungumzia hujuma za kiuchumi inabidi tuimulike TISS katika kutunga na kutekeleza sera za nchi ambazo ni za muda mrefu (Strategic Policies) ambazo kwa kipindi hiki ni Sera ya Elimu, Sera ya mambo ya nje, Sera ya Ulinzi na Usalama, Sera ya uwekezaji, Sera ya tafitiki kubwa za kisayansi, Sera ya Kilimo na Sera ya viwanda.Hapa tumefanikiwa kwa kiasi gani ???

Baada ya hapo nadhani ndiyo tuanze kuzungumzia hizi hujuma kama bomba, ndege na kukwama uwekezaji wa nje ambazo ni sehemu ya madhara (Symptoms) yatokanayo na kushindwa kutekeleza sera za nchi kwa kiwango kinachotakiwa.
 
Nimekuuliza wewe ni nani kusema nchi hii haina changamoto za ulinzi wakati Raisi anasema zipo ??? Hujajibu swali unalialia tu.
 
Watumishi wengi ukiachana na walimu wamekuwa wakitumia muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii wakichati na wengine wakirusha picha kwenye status za WhatsApp.
Wengine utawakuta Instagram, mara Facebook huo ni muda wa kazi .
Sasa unabaki kujiuliza hivi huyu mtumishi anafanya kazi muda gani?
Na hawa ndio ikifika may mosi wananyanyua mabango wakidai kuongezewa mishahara na kupandishwa madaraja na kudai allowance mbali mbali zikiwemo house allowance, communication allowance, electricity allowance n.k.

Namshauri yafuatayo Mzee wetu mzalendo nambari moja Dr Magufuli.

1. Tathimini ya kina ifanyike kwa watumishi wote wa umma kama kweli wanalipwa mshahara kulingana na majukumu yao.

2. OPRAS ya makaratasi iliyopo sasa ifanyiwe maboresho na iwe ya ki electronics ambayo mtumishi ataweza kujaza majukumu yake tarajiwa kwa mwaka wa fedha husika, utekelezaji wa majukumu kwa siku, kwa mwezi,kwa robo mwaka na hadi mwaka. ( hii itasaidia kujua uhaliasia wa mipango inayopangwa).

3.OPRAS iunganishwe na mifumo ya ya bajeti ya Serikali kuu na Serikali za mitaa ( mifumo iwasiliane).

4. Faida ya kuwa na electronic OPRAS itasaidia kutrack add hoc overtime vile vile kutrack extra duties zisizokuwa na uhalisia ambazo mara nyingi utakuta mtumishi anazidai kwa justification za uongo.

5. Kumekuwepo na tabia ya baadhi ya viongozi kupewa communication allowance kila mwezi lakini hawazitumii ipasavyo badala yake maafisa na watumishi wa kada za chini wasiopewa hizo fedha hutumia fedha zao kuwasiliana ( kuratibu) na watumishi wenzao pindi wanapohitaji kujua mambo kadhaa. Kuna haja ya Serikali kuweka system ya kutrack matumizi halisi ya hizi fedha za mawasiliano Kwa wakuu wa idara.

6. Na mwisho kabisa nimpongeze mh Rais wetu Dr Magufuli kwa maamuzi yake ya kishujaa aliyofanya kwa kutujengea sisi watanzania wa hali ya chini hospitali za wilaya zaidi ya 60 na vituo vya afya na zahanati nyingi ndani ya miaka 4. Tena kwa fedha za ndani. Fedha ambazo zilikuwa zikipotea kwa udanganyifu mbali mbali.

Karibu kwa machango wenu wa kujenga tu na sio matusi .
Mkuu walikutema kwenye interview?hasira Kali hizi
 
Mkuu, wanaotunga Sera ya mambo ya nje ya Tanzania pamoja na kumshauri Raisi juu ya utekelezaji wake ni hawa ndugu zetu wa TISS, wakishirikiana na wizara mbalimbali hasahasa zile za mambo ya nje na ulinzi pamoja na jeshi la wananchi. Sasa ukijiuliza swali rahisi kabisa ni kwa kiwango gani tumeweza kutekeleza sera mpya ya mambo ya nje ya Tanzania, utabakia ukisikitika.

Sera ya kwanza ya mambo ya nje ya Tanzania ilitangazwa na Mzee Nyerere miaka ya 1960's mbele ya mabalozi wa nchi za nje na ilijikita kwenye mambo yafuatayo:

Mosi, kutengeneza Tanzania huru isiyofungamana na kambi yotote ile ya vita baridi, ili kuipesha Tanzania isiingie kwenye machafuko kama yale ya Zaire, Vietnam na Korea.

Pili, kupigania uhuru wa nchi za Afrika, hasahasa zile zinaziozunguka Tanzania na kuhakikisha zinakuwa ndani ya ushawishi wa Tanzania. Mfano Msumbiji, Angola, Uganda, Namibia, Afrika Kusini, Zimbabwe, Lesotho, Zambia, Malawi na Botswana.

Tatu, kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika kukabili changamoto za amani ulimwenguni.

Nne, kupambana na ushawishi wa Kizayuni barani Afrika, pamoja na kuzuia kusambaa kwa ushawishi wa Serikali ya Kikabulu ya Afrika Kusini.

Sasa kazi za TISS zilikuwa zikizunguka kwenye mhimili huo tokea mwaka 1976 hadi 1989 baada ya kuisha kwa vita baridi na 1991 baada ya umoja wa kisovieti kuanguka. Katika malengo yote ya Sera ya mambo ya nje TISS walifanya kazi katika weledi mkubwa sana kwasababu waliweza kuyatimiza hayo malengo kwa asilimia 90%.

TISS ilituvusha salama kipindi chote cha vita baridi, japo uchumi ulikuwa mbaya lakini kama nchi tulikuwa na mwelekeo mzuri sana kama tungefanya mabadiliko ya kiuchumi vizuri, kitaalamu na taratibu hasa kipindi cha mfumo wa soko huria.

Miaka ya karibuni tulirekebisha sera yetu ya mambo ya nje, na kujikita kwenye diplomasia ya kiuchumi ambayo tokea kipindi cha Mkapa tulichofanikisha ni kufutiwa madeni makubwa ya nje, kufufua Jumuiya ya Afrika Mashariki, Kuimarisha SADC, kuleta uwekezaji mkubwa wa nje ambao kwa namna moja au nyingine haukuwa na maslahi makubwa kwa taifa letu.

Sasa kabla ya kuzungumzia hujuma za kiuchumi inabidi tuimulike TISS katika kutunga na kutekeleza sera za nchi ambazo ni za muda mrefu (Strategic Policies) ambazo kwa kipindi hiki ni Sera ya Elimu, Sera ya mambo ya nje, Sera ya Ulinzi na Usalama, Sera ya uwekezaji, Sera ya tafitiki kubwa za kisayansi, Sera ya Kilimo na Sera ya viwanda.Hapa tumefanikiwa kwa kiasi gani ???

Baada ya hapo nadhani ndiyo tuanze kuzungumzia hizi hujuma kama bomba, ndege na kukwama uwekezaji wa nje ambazo ni sehemu ya madhara (Symptoms) yatokanayo na kushindwa kutekeleza sera za nchi kwa kiwango kinachotakiwa.
Hakika. Kuna sehemu bado hatujaweza kujiimarisha. Na wanaotaka kutuvusha wamekwama aidha kwa kutofahamu au kwa kupotoshwa uelekeo sahihi wa sera yetu ya mambo ya nje. Inavyoonekana nasi tumekosa vigezo sahihi vya kubainisha makosa pindi tupovuka mipaka yetu. Je ni nani atakayetusahihisha? Je wahusika wako tayari kuyasoma na kuyafanyia kazi maoni yanayotolewa au ndio yanapotezewa kama vile hawayaoni.
 
Mkuu haya yanayotokea sasa hivi yana mzizi mrefu sana. Tena haya ni madhara tu, tatizo lenyewe lipo na wote tunalifahamu lakini tunaogopa kuliangalia na kujifanya kuwa halipo.
 
Unashindwa kuona jibu na bado unajiita mtu mwenye akili...

Labda maana ya neno changamoto hauijui.. Sasa km hakuna changamoto vyombo vya ulinzi vimeundwa vya nin!?

Changamoto zipo lakini zinakabiliwa kwa usahihi kabisa na ndio maana mpka sasa umetulia unaandika unachokiwaza, na ratiba ya kesho unayo alafu kesho kutwa unakuja kuandika mavi....

Then unajiita msomi mwenye akili.. Sa sijui umekisomea nin ambacho kinashndwa kukuongoza.

Hujengi hoja . we ni mtu wa kupanic na kutafuta sympath.... Andika unachokijua na sio kusikia au kukisoma magezetini.

Hii Nchi ni zaidi ya maneno unayoyasikia.

Nimekuuliza wewe ni nani kusema nchi hii haina changamoto za ulinzi wakati Raisi anasema zipo ??? Hujajibu swali unalialia tu.
 
Kwanza ukiniletea andiko au ushahid hata wa video...

Raisi JPM anaongea kwa mdomo wake kuwa nchi haina ulinzi...

Nichezee Ban siku 14.

Usipotoshe umma... Iyo kauli haitolew na viongoz wa juu... Yuule ni amiri jeshi mkuu.

Kauli za kipimbi km hizi huongelewa na watu km nyie mnaoleta ujuaji mwingi... Vitabu vingi.... Unapitia pitia makala za yericko unakuja kupingana na hali halisi unayoiona kwa macho, na unajiita mwenye akili.

Aaah aaah a dah

Kuna movement inaitwa HAMU ulushawah kuziskia!?

Kuna opereshen za kijeshi za ndan ya nchi zaid ya 4 ushawah kuziskia!?

Kuna seke seke za wakimbili mtabila, nyarugusu n.k ulishawah kuziskia?

Kuna uvamivi wa raia wa kigeni katika nchi kwa malengo mabaya na wanashughulikiwa ushawah kuyaskia?

Izo zoote zinafanywa we upo kwenu unakula ugali huku una type unasoma vitabu... Ukija unasema jamaa hawana wanachokifanya.. Mara ussr mara sijui nyerere...

We jamaa bhana.
 
Kwanza ukiniletea andiko au ushahid hata wa video...

Raisi JPM anaongea kwa mdomo wake kuwa nchi haina ulinzi...

Nichezee Ban siku 14.

Usipotoshe umma... Iyo kauli haitolew na viongoz wa juu... Yuule ni amiri jeshi mkuu.

Kauli za kipimbi km hizi huongelewa na watu km nyie mnaoleta ujuaji mwingi... Vitabu vingi.... Unapitia pitia makala za yericko unakuja kupingana na hali halisi unayoiona kwa macho, na unajiita mwenye akili.

Aaah aaah a dah
Sawa.
 
Serikali ya awamu ya tatu iliifanyia mabadiliko sheria hii mwaka 1996.
Mkuu Richard hii sheria ipo na inatumika. Haijabadilishwa. Hii ni general. Ni ya wote, ni tofauti na ile ya TISS, 1996. Hii inatumika. Watu wote wanaoweza kukutana na nyaraka za serikali kama vile wasimamia michakato ya sensa, wakuu wa taasisi, wanaofanya kazi taasisi nyeti kama vile NECTA, wasimamizi wa mitihani ya kitaifa, wasahihishaji wa mitihani ya kitaifa, n.k. huapa kwa kutumia sheria hii. Ipo na inatumika.
 
Mkuu,

Kwahio hii ya 1970 ndo general

Na hii ya 1996 ni ya Usalama wa taifa.

Je, huoni kwamba kuna haja ya kuzifanyia mabadiliko sheria hizi na kuitunga sheria moja tu ya Usalama wa taifa?
 
Back
Top Bottom