Idara ya usalama wa taifa, ndo idara nyeti, nzito na muhimu kuliko idara zote za serikali.
Kwa hiyo panatakiwa pawe na wafanyakazi ma genius hasa ktk idara hiyo, na wasiwe na mapenzi ya chama chochote cha siasa, bali wawe na mapenzi na nchi yao tu.
Wawe wabunifu kwa ajili ya usalama wa taifa lao, usaili wa ajira ufanyike bila kuangalia kiwango cha Elimu ya mtu (kwa baadhi ya vitengo) bali uwezo, weledi, uzalendo wa nchi na akili za mtu.
Neno usalama wa taifa ni neno pana sana, naipenda sana nchi yangu Tanzania ndo maana naamini ushauri wangu kuna siku utafanyiwa kazi vilivyo.
Usalama wa taifa ni lazima wahakikishe nchi ina uchumi mzuri, kwa sababu watu wakilala njaa na kukosa mahitaji muhimu matokeo yake nchi inaweza kuingia kwenye vurugu kubwa mno na hivyo kufanya usalama kutoweka.
Ndo maana nasema hii ni idara nyeti mno, taifa lolote lenye uchumi mbovu na maisha magumu kwa watu wake ina maana pia usalama wa taifa ni dhaifu hauwezi kulinda usalama wa nchi kwa uhakika.
Kutisha watu,na kuua wapinzani ni kuzidi kupanda mbegu za chuki na bomu ambalo mwisho wa siku ni lazima lilipuke .
Kama idara ya usalama wa taifa haina kitengo cha kufanya hujuma za kiuchumi kwa mataifa ya nje kwa faida ya nchi ina maana bado kitengo ni dhaifu na kina watu ambao hawajapikwa na kuiva hasa.
Kila napokuja nyumbani Tanzania na kuangalia mazingira ya nchi yapo duni mno, vijana wengi wakishinda vijiweni hawana kazi za kufanya, huwa najiuliza nini hatima ya nchi Kama hii?
Lowassa aliwahi kusema, ukosefu wa ajira ni bomu linalosubiria kulipuka siku moja.
Basi idara ya usalama wa taifa inatakiwa ihakikishe hilo bomu halilipuki kwa gharama yoyote, ikibidi kufanya ujambazi (ujasusi) wa kiuchumi kwa mataifa ya nje na kuleta nyumbani ili watoto wale.
Urusi ilikuwa taifa la kwanza Duniani kupeleka chombo na wanaanga kwenye mwezi .
Marekani ilipoona hivyo, ikajaa wivu na ilipojaribu kwenda, chombo chao kililipuka kwa sababu ya hitilafu kwenye engine, wakajiuliza kwa nini warusi waliweza na sisi kushindwa?
Walichofanya ni kuiba teknolojia ya Urusi ya engine hadi wakafanikiwa kwenda.
Sisi tuna wivu wa kichawi, tunapigana vita ndugu kwa ndugu, hatutaki wapinzani waingie ikulu, badala ya kupigana Vita ya kumaliza umaskini, tunamalizana sisi kwa sisi.
Halafu anasimama mtu na kusema eti tutafanikiwa, tutafanikiwa kwa lipi wakati mikono yetu ina Damu za watu zinazolia kwa Mungu zikidai kisasi?
Yaani idara ya usalama wa taifa ilishuhudia kabisa viwanda zaidi ya 400 alivyoacha Mwl Nyerere vikiuliwa, lakini idara hiyo haiko tayari kushuhudia mkosoaji wa serikali akisimama hadharani na kuikosoa serikali ,labda awe nyuma ya keyboard Kama mimi hapa
INAENDELEA