Part 2: TISS bado safari ngumu

Part 2: TISS bado safari ngumu

Unajuaje kama wamekaa tu?
Kwani wanaripoti kwako?
Ndege kukamatwa,

Dhababu kukamwatwa ikiwa Kenya na kuletwa Tz.

Watanzania kuuawa sauzi,

Mauaji yaliyokua yakitokea hapa tz.

Utekaji wa watu...

Watu kupotea.

Je kwa akili yako ukijumlisha yote haya hutapata wasi wasi juu ya utendaji wao?
 
Mkuu si kwamba nakudharau ila mbona kama uwezo wako wa kujenga na kuchambua hoja umeshuka sana? nini tatizo? siasa nyingi? ushabiki wa ccm au nini?

Kwa uwezo wako sikutarajia uwe na mawazo madogo kama haya. No offence intended but you need to change for good!!

Kila la heri.
Huna hoja pumbafu wewe your IQ is below the sea level
 
Idara ya usalama wa taifa, ndo idara nyeti, nzito na muhimu kuliko idara zote za serikali.

Kwa hiyo panatakiwa pawe na wafanyakazi ma genius hasa ktk idara hiyo, na wasiwe na mapenzi ya chama chochote cha siasa, bali wawe na mapenzi na nchi yao tu.

Wawe wabunifu kwa ajili ya usalama wa taifa lao, usaili wa ajira ufanyike bila kuangalia kiwango cha Elimu ya mtu (kwa baadhi ya vitengo) bali uwezo, weledi, uzalendo wa nchi na akili za mtu.

Neno “Usalama wa Taifa” ni neno pana sana, naipenda sana nchi yangu Tanzania ndo maana naamini ushauri wangu kuna siku utafanyiwa kazi vilivyo.

Usalama wa taifa ni lazima wahakikishe nchi ina uchumi mzuri, kwa sababu watu wakilala njaa na kukosa mahitaji muhimu matokeo yake nchi inaweza kuingia kwenye vurugu kubwa mno na hivyo kufanya usalama kutoweka.

Ndo maana nasema hii ni idara nyeti mno, taifa lolote lenye uchumi mbovu na maisha magumu kwa watu wake ina maana pia usalama wa taifa ni dhaifu hauwezi kulinda usalama wa nchi kwa uhakika.

Kutisha watu,na kuua wapinzani ni kuzidi kupanda mbegu za chuki na bomu ambalo mwisho wa siku ni lazima lilipuke.

Kama idara ya Usalama wa Taifa haina kitengo cha kufanya hujuma za kiuchumi kwa mataifa ya nje kwa faida ya nchi ina maana bado kitengo ni dhaifu na kina watu ambao hawajapikwa na kuiva hasa.

Kila napokuja nyumbani Tanzania na kuangalia mazingira ya nchi yapo duni mno, vijana wengi wakishinda vijiweni hawana kazi za kufanya, huwa najiuliza nini hatima ya nchi Kama hii? Lowassa aliwahi kusema, ukosefu wa ajira ni bomu linalosubiria kulipuka siku moja.

Basi idara ya Usalama wa Taifa inatakiwa ihakikishe hilo bomu halilipuki kwa gharama yoyote, ikibidi kufanya ujambazi (ujasusi) wa kiuchumi kwa mataifa ya nje na kuleta nyumbani ili watoto wale.

Urusi ilikuwa taifa la kwanza Duniani kupeleka chombo na wanaanga kwenye mwezi.

Marekani ilipoona hivyo, ikajaa wivu na ilipojaribu kwenda, chombo chao kililipuka kwa sababu ya hitilafu kwenye engine, wakajiuliza kwa nini warusi waliweza na sisi kushindwa?

Walichofanya ni kuiba teknolojia ya Urusi ya engine hadi wakafanikiwa kwenda.

Sisi tuna wivu wa kichawi, tunapigana vita ndugu kwa ndugu, hatutaki wapinzani waingie ikulu, badala ya kupigana Vita ya kumaliza umaskini, tunamalizana sisi kwa sisi.

Halafu anasimama mtu na kusema eti tutafanikiwa, tutafanikiwa kwa lipi wakati mikono yetu ina Damu za watu zinazolia kwa Mungu zikidai kisasi?

Yaani idara ya Usalama wa Taifa ilishuhudia kabisa viwanda zaidi ya 400 alivyoacha Mwl Nyerere vikiuliwa, lakini idara hiyo haiko tayari kushuhudia mkosoaji wa serikali akisimama hadharani na kuikosoa serikali ,labda awe nyuma ya keyboard Kama mimi hapa

INAENDELEA
Hao wapinzani unaotaka waingie ikulu wako wapi kamanda?
Hawa akina Sumaye na Nyalandu?
 
Ukiweka siasa pembeni, Kitabu cha Yericko Nyerere kimeyaandika hayo kwa undani sana tena kwa mifano

Kiongozi pitia kitabu hicho

Mambo yote ya ujasusi wa kiuchumi, mbinu na fitina za ulimwengu wa kisasa ameviandika
Halafu wenye mamlaka hawawezi fanyia kazi ushauri wa Yeriko tu kwasababu Yeriko ni mwana Chadema; nchi hi ina matatizo 2 makubwa, ccm pamoja na Uyanga na Usimba; yaani mtu hata mwenye akili nyingi nae hua anatoa comment akiangalia maslahi either ya uccm au kwenye michezo huko basi ni usimba na Uyanga. Sorry kwa kutoka kidogo nje ya topic, juzi bwana Haji Manara kafanya press yake vizuri tu, kuna mengi kakosea but mengi ya yale maneno alikua anajaribu kujibu hoja zilizotolewa na waliokua wakubwa wake, facts tupu katema kule, nilishangaa sana mtu kama kigogo2014 kumponda vile, nilishangaa sana, yaani kwamba hata mtu niliyekua nadhani ni mtu makini kama kigogo2014 nae akajikuta anajadiri hoja Kisimba zaidi kuliko facts? Nilishangaa sana, but hali ndio hiyo hiyo, mwana ccm akisikia kitu kutoka kwa mwana chadema hata kama kina mantiki but hatakubali, atajitahidi kubishana hata kwa UJINGA tu ili chama chake kiwe salama na sio nchi, stupid. Wote tunakua kama kina Msukuma, kibajaji/Lusinde, very sad indeed
 
Back
Top Bottom