Papa Msoffe na wenzake wafutiwa mashtaka na DPP

Papa Msoffe na wenzake wafutiwa mashtaka na DPP

Marijani Abdubakari Msoffe aka Papa Msoffe ameachiliwa huru baada ya MKurugenzi wa Mashitaka (DPP) kusema hana mpango wa kuendelea na kesi dhidi yake. Walikuwa wakikabiliwa na mashtaka matano likiwemo la kujipatia fedha kiasi cha Sh943 milioni kwa njia ya udanganyifu

Mbali na Msofe, washtakiwa wengine walikuwa wakili wa kujitegemea, Mwesigwa Mhingo, Wenceslau Mtui, Josephine Haule na Fadhil Mganga

Miongoni mwa mashtaka yaliyokuwa yakiwakabili ni kuratibu genge la uhalifu, utakatishaji fedha na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu

Zaidi, soma:
1). Papaa Msofe naye yamkuta. Afikishwa Mahakamani akituhumiwa na makosa matano likiwemo ya Utakatishaji fedha

2). Papaa Msoffe apata dhamana baada ya kubadilishiwa mashtaka

3). Papaa Msofe akabiliwa na kesi ya mauaji

4). Papa Msofe ni mfanyabiashara au tapeli Maarufu?
Kweli tulikabidhi nchi kwa mshamba .Anyway,angalau taratibu biashara na mishe mitaani zitaanza kuimarika ivyo mzunguko wa fedha kuonekana, whether legally or illegally the money must flow across the streets!
 
Legally or illegally? Haya ni maajabu? Uchumi ukiendeshwa kwa illegal money huko street unaposema basi hiyo nchi inakaribia kuanguka
 
Watu wapo ndani miaka upelelezi haujakamilika, jinai haifi ikithibitika wana makosa watawakamata tena
Serikali makini hawa walistahili kupotezwa moja kwa moja. sasa huyu ambaye hana ajenda ya kisiasa kumpa sifa, ameona kuachia waharifu ndo sifa yake kuu. Tunaumizwa Tanganyika wakati kwao Zanzibar wamejifungia.
 
Kweli tulikabidhi nchi kwa mshamba .Anyway,angalau taratibu biashara na mishe mitaani zitaanza kuimarika ivyo mzunguko wa fedha kuonekana, whether legally or illegally the money must flow across the streets!
Unamzungumzia nani? JPM? Kama jibu lako ni ndiyo basi nawe ni bwege kama huyo anayetoa msamaha. Hujui hata Msofe alikamatwa lini, wewe unaropoka tu. Au we ni wale wa kanda ile?
 
Huyu Dpp anafungulia watu kama hana akili nzuri! Ubaya anayafanya haya ili kufurahisha watu... tungoje mìezi kadhaa hapo mbele ndio atajua hajui
Kama Serikali imeshindwa kuthibitisha mashtaka yao kwanini wabaki jela
 
Kwanini wasitoe watu masikini waliofungwa kwa wizi wa kuku ambao kesi zao hazina miguu wala kichwa badala yake wanaachiwa hao mafisadi pekee?
Wewe MJINGA ikiwa kwa Miaka yote mliopeleka kesi Mahakamani mkashindwa kuthibitisha mashtaka yenu manake mliBambikia watu
 
Wewe MJINGA ikiwa kwa Miaka yote mliopeleka kesi Mahakamani mkashindwa kuthibitisha mashtaka yenu manake mliBambikia watu
Kwa kuwa sheria ndo inatafarisi makosa, ina maana amebambikiwa japokuwa watakuwapo walioathirika na hizi njemba. Kama kweli wako clean wadai fidia au siyo???
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemfutia mashtaka na kumwachia huru Mfanyabiashara Marijan Msofe (53) maarufu Papa Msofe na wenzake wanne.

Hii ni baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania( DPP) kuieleza Mahakama hiyo kuwa hana nia ya kuendelea na shauri dhidi ya Washtakiwa hao.

Papaa Musofe na wenzake walikuwa wanakabiliwa na mashitaka matano likiwemo la kujipatia fedha kiasi cha Sh.Mil 943 kwa njia ya udanganyifu ambapo wengine ni Mwesigwa Mhigo, Wenceslau Mtui, Josephine Haule na Fadhil Mganga.
 
Back
Top Bottom