Papa Msoffe na wenzake wafutiwa mashtaka na DPP

Papa Msoffe na wenzake wafutiwa mashtaka na DPP

Waachie jamani na wezi wa kuku, tena hao ni wengi tu na ndio wamejaza magereza, maana hata kama ni makubaliano na DPP inakuwa rahisi.....
 
Huyu papaa Msofe alikuwa mhuni, muonevu sana, DPP asilifunge jalada la huyu jamaa, Watu wanasema huyu mtu siyo mzuri.
Kwa huyu jamaa DPP kachemsha
Kama aliachiwa babu Seya wala sioni ajabu kwa Papaa Msofe! Kazi iendelee...
 
Hicho si kigezo cha kuhalalisha wahalifu warudi uraiani
Kama ulikua na ushahidi usiotia shaka ungeupeleka.Sio watu wote wanaoshikiliwa magerezani ni wahslifu na pia ata kama ni wahalifu walifanya ualifu kwa akili kiasi cha kuficha ushahidi ndo maana inakua vigumu kumtia hatihani moja kwa moja.sasa kesi za aina hiyo kuna haja gani kuendelea kua nazo.kwahiyo usikariri sana maana ata wewe kesho waweza jikuta behind bar.
 
Marijani Abdubakari Msoffe aka Papa Msoffe ameachiliwa huru baada ya MKurugenzi wa Mashitaka (DPP) kusema hana mpango wa kuendelea na kesi dhidi yake. Walikuwa wakikabiliwa na mashtaka matano likiwemo la kujipatia fedha kiasi cha Sh943 milioni kwa njia ya udanganyifu

Mbali na Msofe, washtakiwa wengine walikuwa wakili wa kujitegemea, Mwesigwa Mhingo, Wenceslau Mtui, Josephine Haule na Fadhil Mganga

Miongoni mwa mashtaka yaliyokuwa yakiwakabili ni kuratibu genge la uhalifu, utakatishaji fedha na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu

Zaidi, soma:
1). Papaa Msofe naye yamkuta. Afikishwa Mahakamani akituhumiwa na makosa matano likiwemo ya Utakatishaji fedha

2). Papaa Msoffe apata dhamana baada ya kubadilishiwa mashtaka

3). Papaa Msofe akabiliwa na kesi ya mauaji

4). Papa Msofe ni mfanyabiashara au tapeli Maarufu?
Ifike Mahali huyu Papaa Msofe aache Wizi na Utapeli Umri umekuwa Mkubwa anataka Aibe mpaka Kaburini
 
Back
Top Bottom