BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,376
- 8,119
Gasaya alishtakiwa kwa makosa ya kujipatia fedha hizo kutoka katika Saccos ya JATU kwa madai kuwa fedha hizo ataziweka (Kuzipanda) kwenye Kilimo cha Mazao ili kuzalisha faida zaidi, wakati akijua kuwa ni uongo.
Kupitia wakili wake, Nafikile Mwamboma amedai Gasaya amedai kuwa ameandika barua kwa DPP, tangu Aprili 20, 2023 akiomba kukiri mashtaka yake ili aweze kuimaliza kesi hiyo.
============
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya JATU PLC, Peter Gasaya (33) anayekabiliwa na mashtaka mawili likiwemo la kujipatia Sh5.1 bilioni kwa njia ya udanganyifu, amemwandika barua ya kukiri na kuomba apunguziwe adhabu, Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP).
Gasaya anadaiwa kujipatia fedha hizo kutoka katika Saccos ya JATU kwa madai kuwa fedha hizo atazipanda kwenye kilimo cha mazao ili kuzalisha faida zaidi, wakati akijua kuwa ni uongo.
Mshtakiwa huyo ameileza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo, Aprili 24, 2023 mbele ya hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo Richard Kabate, wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutajwa.
Gasaya, kupitia wakili wake, Nafikile Mwamboma amedai kuwa ameandika barua kwa DPP, tangu Aprili 20, 2023 akiomba kukiri mashtaka yake ili aweze kuimaliza kesi hiyo.
MWANANCHI