Wafikishwa Mahakamani kujibu mashtaka 11 likiwemo utakatishaji Tsh. Milioni 658

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,119
1686222970132.png

Watu wawili wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka 11 likiwemo la utakatishaji wa fedha zaidi ya Sh658 milioni.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Grace Mwanga amewataja washtakiwa hao ni mfanyabiashara Ridhiwani Shaban na Moses Nassoro.

Akisoma hati ya mashtaka Wakili, Mwanga amedai kati ya Agosti 28 hadi Septemba 9, 2022, katika maeneo tofauti nchini washtakiwa hao walikula njama na kutenda kosa la kujipatia Sh658.8 milioni kwa njia ya udanganyifu.

Mwanga amedai washtakiwa hao walijipatia fedha hizo kutoka kwa Reymond Mavika kwa madai kwamba wataziwekeza katika biashara ya mazao ya kilimo badala yake walitakatisha fedha hizo Kwa kujinunulia vitu mbalimbali.

"Washtakiwa hao walitakatisha fedha hizo kwa kujinunulia vitu mbalimbali huku wakijua fedha hizo ni mazalia ya kosa la kujipatia fedha kwa udànganyifu," amedai Mwanga.

Inadaiwa Shabani alizitumia kwa kununua gari aina ya Toyota IST, Music System, gari aina ya Toyota Rush, seti ya Luninga aina ya Goodvision, genereta, taa za disko, trekta na Sh21.4 milioni aliziweka katika akaunti yake ya CRDB.

Mwanga alidai kuwa mshtakiwa Nassoro alizitumia kwa kununua gari aina ya Toyota Harrier, Town Hiace, spea za gari na Sh96 milioni alikutwa amezihifadhi nyumbani kwake Mang'ula, Kilombelo huku akijua ni kosa.

Upelelezi bado haujakamilka na washtakiwa hao walikana makosa yanayowakabili.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Mkuu, Rhoda Ngimilanga aliahirisha shauri hilo hadi Juni 21, 2023.

MWANANCHI
 
Walikosa elimu kuhusu Pesa !! Ila kibongo bongo kutakatisha pesa inawezekana kabisa na usikamatwe !! Tatizo kuna Wenge la hela.
Madogo wanauza cocaine halafu mradi wa kuzugia eti mtu anaenda kufungua kiflame cha kuuza cover za simu tu anaweka vitaa taa ! Wahuni watakushtukia tu ! Bata unalokula lisipoendana na miradi yako full kujiachia watakusarandia tu , wakutie korokoroni !
 
Dah! Kuna watu hapa duniani hawana bahati hata kidogo. Yaani sisi wengine tunahangaika na mikopo ya mabenki, huku tukidhikabidhi hizo benki hati zetu za nyumba!

Halafu anatokea mtu ambaye hana mambo mengi, anawapa hela zote hizo kwa ajili ya kwenda kumnunulia mazao! Badala yake wanaenda kununlia magari na vitu vingine vya kipuuzi!! Ujinga gani huu! Ndiyo kusema hela inaleta vishawishi kiasi hiki!!

Huyo jamaa angenipa hizo hela mtu kama mimi, aisee ningemnunulia mzigo wake! Na kwa uaminifu mkubwa! Na faida kidogo ambayo ningepata, ningeitumia kwa uhuru kabisa.
 
View attachment 2650077
Watu wawili wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka 11 likiwemo la utakatishaji wa fedha zaidi ya Sh658 milioni.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Grace Mwanga amewataja washtakiwa hao ni mfanyabiashara Ridhiwani Shaban na Moses Nassoro.

Akisoma hati ya mashtaka Wakili, Mwanga amedai kati ya Agosti 28 hadi Septemba 9, 2022, katika maeneo tofauti nchini washtakiwa hao walikula njama na kutenda kosa la kujipatia Sh658.8 milioni kwa njia ya udanganyifu.

Mwanga amedai washtakiwa hao walijipatia fedha hizo kutoka kwa Reymond Mavika kwa madai kwamba wataziwekeza katika biashara ya mazao ya kilimo badala yake walitakatisha fedha hizo Kwa kujinunulia vitu mbalimbali.

"Washtakiwa hao walitakatisha fedha hizo kwa kujinunulia vitu mbalimbali huku wakijua fedha hizo ni mazalia ya kosa la kujipatia fedha kwa udànganyifu," amedai Mwanga.

Inadaiwa Shabani alizitumia kwa kununua gari aina ya Toyota IST, Music System, gari aina ya Toyota Rush, seti ya Luninga aina ya Goodvision, genereta, taa za disko, trekta na Sh21.4 milioni aliziweka katika akaunti yake ya CRDB.

Mwanga alidai kuwa mshtakiwa Nassoro alizitumia kwa kununua gari aina ya Toyota Harrier, Town Hiace, spea za gari na Sh96 milioni alikutwa amezihifadhi nyumbani kwake Mang'ula, Kilombelo huku akijua ni kosa.

Upelelezi bado haujakamilka na washtakiwa hao walikana makosa yanayowakabili.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Mkuu, Rhoda Ngimilanga aliahirisha shauri hilo hadi Juni 21, 2023.

MWANANCHI
Wamejua hadi matumizi na bakaa ila "upelelezi haujakamilika" wakipewa mgao wao upelelezi hautakaa ukamilike 😎😎
 
Hakuna kesi hapo. Labda wasingekutwa na huo mpunga. Huohuo mpunga ndo hakimu.
 
Back
Top Bottom