Papa Leo aahidi kuiombea Tanzania amani na Utulivu
Papa akutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania

Ni katika nchi ya Tanzania ambayo Tume ya uchunguzi iko inafanya kazi ili kubaini wahusika wa vurugu zilizoibuka mwezi Oktoba 2025 iliyopita katika tukio la uchaguzi.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Papa Leo XIV, kabla ya Katekesi yake Jumatano tarehe 28 Januari 2026, alikutana na Balozi Mahmoud Thabiti Kombo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania. Waziri yuko anatimiza ziara ya Kimataifa na alikuwa Mwakilishi wa Ujumbe wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, aliyethibitishwa kuongoza tena Tanzania katika uchaguzi wa Mwezi Oktoba iliyopita.

Kama itakumbukwa katika siku za upigaji kura, mwishoni mwa mwezi Oktoba 2025, kulitokea mapigano na vurugu ambazo kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Kimataifa, zilisababisha mamia ya vifo.

Rais wa Tanzania aliunda Tume ya Uchunguzi ambayo tayari inafanya kazi kwa ajili ya ujenzi mpya wa kile kilichotokea na ambacho kinawakilisha mshtuko mkubwa kwa Nchi, ambayo hadi wakati huo ilikuwa tulivu na mahali ambapo hapakurekodiwa mvutano maalum wa kijamii. Vurugu hizo zilikuwa zimelaaniwa na viongozi wakuu wa Makanisa na kidini nchini Tanzania, Maaskofu na Maimamu, kwa kuomba kufanyika uchunguzi wa kujitegemea ili kubaini hali hiyo na wahusika.

Papa Leo XIV alikuwa amezungumza wazi kwa umma kuhusu hali hiyo ya nchi wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana, tarehe 2 Novemba 2025 akisema kuwa:“ Tusali hata kwa ajili ya Tanzania, mahali ambapo baada ya uchaguzi uliopita wa kisiasa, iliibuka mivutano na kusasabisha waathirika. Ninawaalika wote kuepuka kila aina ya vurugu na kuchuchumalia njia ya amani.”
 
Attachments

  • _TOM6859.JPG
    _TOM6859.JPG
    793.4 KB · Views: 2
  • _TOM6892.JPG
    _TOM6892.JPG
    753 KB · Views: 3
  • _TOM6841.JPG
    _TOM6841.JPG
    665.3 KB · Views: 9
  • _TOM6832.JPG
    _TOM6832.JPG
    672.9 KB · Views: 6
  • 138997727_F138997727.mp3
    138997727_F138997727.mp3
    1.9 MB
  • _TOM6850.JPG
    _TOM6850.JPG
    641.4 KB · Views: 6
Kitu alichokifanya kabudi aibu naona mimi sijui alienda kuongea nini maskini na papa kwamba unashtaki wanaopinga mauwaji.

Heti huyu ndio mnamuita genius sijui professor? ameenda kufanya kazi kipumbavu sana yani kiufupi hajui anachokifanya ni nini na papa alimuona hana akili sana sio tu papa bali wakatoriki duniani wakisikia wata mshangaa sana.

Aibu naona mimi kweli washauri wa samia ni akina kingwendu kwahiyo papa akuunge mkono kwa mauwaji ya halaiki ya watanzania uliyofanya na kujigamba kuwa ilikuwa sio tatizo ?

Sasa niwazi ile project ya wakotoriki feki na hii ya kabudi ni ya samia na genge lake na zote ni za kimbumbumbu na matumizi mabaya ya madaraka na fedha za umma.
 
Mzee wa kuwaponda mabeberu ndo huyo ametumwa kwenda kuwapigia magoti
 
Back
Top Bottom