Msipotoshe kuhusu Papa


Papa Francis amewaruhusu mapadre kuwabariki wapenzi wa jinsi moja, yakiwa ni maendeleo makubwa kwa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsi moja na mahusiano mengine ya kijinsia wanaofahamika kama LGBT katika Kanisa Katoliki la Roma.
Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki la Roma amesema makasisi wanapaswa kuruhusiwa kuwabariki wapenzi wa jinsi moja na wanandoa "isiyo ya kawaida", kwa misingi ya hali fulani.
Lakini Vatikani ilisema baraka hazipaswi kuwa sehemu ya taratibu za kawaida za Kanisa au zinazohusiana na miungano ya kiraia au harusi.
Iliongeza kuwa inaendelea kuiona ndoa kuwa kati ya mwanamume na mwanamke.

Papa Francis aliidhinisha waraka uliotolewa na Vatican kutangaza mabadiliko hayo siku ya Jumatatu.
Vaticani ilisema inapaswa kuwa ishara kwamba "Mungu anawakaribisha wote", lakini hati hiyo inasema makuhani lazima waamue kwa msingi wa kesi baada ya kesi.
Akitambulisha andiko hilo, Kardinali Víctor Manuel Fernández, ambaye ni msimamizi wa Kanisa, alisema kwamba tamko jipya limebakia kuwa "imara kwenye fundisho la kimapokeo la Kanisa kuhusu ndoa".
Lakini aliongeza kuwa kwa kuzingatia "maono ya kichungaji" ya Papa" ya "kupanua" ombi la Kanisa Katoliki, miongozo mipya inawaruhusu mapadre kubariki uhusiano ambao bado unachukuliwa kuwa wa dhambi.
Watu wanaopokea baraka "haifai kuhitajika kuwa na ukamilifu wa kimaadili wa awali", kulingana na tamko hilo.
Katika Kanisa Katoliki, baraka ni maombi au ombi, ambalo kwa kawaida hutolewa na mhudumu, akimwomba Mungu ambariki mtu au watu wanaobarikiwa.
Kardinali Fernández alisisitiza kwamba msimamo huo mpya hauhalalishi hadhi ya wapenzi wa jinsia moja mbele ya Kanisa Katoliki.

Hii ni taarifa ya BBC
Haya maelezo yana tofauti gani na maelezo ya Kiharage aliyekuwa MD wa TANESCO kwamba hakuna mgao wa umeme isipokuwa kuna upungufu wa umeme?
 
Sidhani kama bado tuko Kwenye nyakati za Manabii wa Ukweli' kwa Sababu dalili zote zinaonyesha Ule Mwisho wa Ulimwengu huu umekaribia

Tunaishi katika Nyakati ngumu sana Joshua Mollel kachinjwa kama ngamia

Kana Kwamba hiyo haitoshi Papa Francisco anayeketi kitini pake mtume Petro anahalalisha Ndoa za Jinsia Moja, Watoto wetu wamekwisha

Ghadhabu ya Mungu wa mbinguni itakuwa Zaidi ya Sodoma na Gomola

Na Nchi zinazoishi kwa Mikopo Ndoa za Jinsia Moja zaweza Kuwa Sharti la kukopesheka

Mungu wa mbinguni Uturehemu Sisi!
Hukuisoma taarifa ya Papa vizuri, ndiyo maana umeamua kupotosha bila sababu
 
Back
Top Bottom