Bubu Msemaovyo
Platinum Member
- May 9, 2007
- 4,189
- 3,552
Kitendo cha kumtimua Mwanasheria wa Tanesco kwa kisingizio cha kusafiri nje ya nchi bila ruhusa ya mwajiri wake kinazua maswali mengi hasa baada ya ukweli kubainika kwamba alipata ruhusa kama taratibu zinavyotaka. Godwin Ngwilimi alienda nchini Malaysia kuchunguza uuhalali wa Kampuni ya PAP kumiliki hisa za IPTL.
Fununu zilizozagaa mitaani zinadai kwamba alichokiona huko Malaysia na kuja kukitoa kama report yake ndivyo vilivyo sababisha awajibishwe, inasemekana aliona wamiliki wa PAP ni wakurugenzi wane wawili kati yao Watanzania ambao ni Mama Mkubwa na Bintiye wenye majina yanayofanana fanana.
Jambo la pili ni kauli ya Prof Muhongo aliposema ikiwa atalazimishwa kujiuzulu nchi itatikisika.
Jambo la tatu ni kukataa kwa benki ya Stanbic kutoa majina ya waliopata mgao wa fedha za escrow account.
Kwa sababu hii kuondolewa madarakani Prof Muhongo hakupo, kiporo alichosema Mh Rais ni usanii tu.