Nimesoma andiko la ZITTO refu sana akieleza historia mwanzoni lakini jana nikasoma maoni ya Mwandishi wa CITIZEN aliyekuwa karibu sana akishirikiana na Mwasisi mwenyewe Richard Mgamba,ambaye alikuwa Mhariri wa Citizen na sasa yupo Guardian, nikathibitisha kwamba ZITTO ni mwanasiasa kijana mpenda sifa zoote kupata kutokea taifa hili;
1.Anasema yeye ndiye aliyemtuma KAFULILA hoja hiyo bungeni na kwamba nyaraka hizo ndiye aliyempa pia Mhariri wa CITIZEN Bw Richard Mgamba mwaka2014. Lakini kwa Mwandishi huyu wa CITIZEN anaonesha wazi kwamba CITIZEN walipata nyaraka hizo tangu Nov 2013, kutoka Singapore, Malaysia na South Africa.
2.Mwandishi huyo anasisitiza walimpa nyaraka hizo awali KAFULILA April2014 baada ya wao kuchapa mfululizo na KAFULILA kuwaomba Nyaraka hizo.
3.Mwandishi anasema baada ya KAFULILA kulipua bungeni wakati wa mjadala wa Bajeti ya waziri Mkuu April 2014, na kutaja vigogo kwa majina, ndipo joto likapanda, na wao walipoonekana kama ndio source, wakatishwa zaidi na kampuni ya Singasinga PAP.
4.Ndipo Tido Muhando akiwa Mkurugenzi wa Mwananchi Communication inayomiliki gazeti la CITIZEN akawataka wandishi waliokuwa na AGENDA hiyo wakiongozwa na Mhariri Mgamba kutoa maelezo ya kina juu ya swala hilo kisha wakakubaliana ushahidi huo aongezewe KAFULILA kwasababu tayari ameshawasha moto huo ili ukweli uzidi kujulikana.
5.Ndipo KAFULILA alipochangia tena kwenye mjadala wa Bajeti ya wizara ya Nishati akaingia na Mkoba mkubwa umejaa docs hizo na akatakiwa na Spika kuwasilisha akawasilisha, ni siku hiyo Prof Muhongo alisema yeye anaoushahidi wakujaa pickup, na kwamba karatasi za KAFULILA ni zakufungia vitumbua.
6.BAADA ya hapo ndipo ZITTO alipata ushahidi wa ziada akampa Mgamba na Kafulila ikiwa ni mwezi June,moto umeshawaka na Waziri Mkuu ameshatangaza bungeni kwamba uchunguzi maalumu ameagiza utafanywa na CAG&PCCB na taarifa zake zitawasilishwa na kuamua.
7.Mwandishi anasisitiza kwamba Dr Hosea alifanya kazi kubwa sana katika vita hii hasa ikizingatiwa kuwa jambo hilo lilihusu mpaka Ofisi ya mwajiri wake, ambaye ni Rais. Kumbuka kupambana vita ya escrow ilikuwa kupambana na JK.
8.Mwandishi anasisitiza kwamba kila mtu alifanya jukumu lake ,kwa nafasi yake na hata pamoja na Kafulila kupewa tuzo April 2015 haikumanisha alifanya kazi peke yake lakini ni kama ilivyo kwenye mpira kwamba anapewa TUZO mfungaji bora bila kujali ilikuwa juhudi za team nzima, kila mmoja kwa nafasi yake. Hakuna sababu ya mchezaji mwingine kulalamika kwanini sio yeye.
9.USHAURI wangu kwa ZITTO kwamba tuzo imeshatolewa tangu April 2015, aliyeonekana kuwa ni mchezaji bora kashapewa Tunzo yake na mchango wa yeyote aliyeshiriki katika pambano hili utabaki kwenye kumbukumbu, huna sababu ya kutaka uonekane wakati watu wa wameshakuona katika mapambano mengine,kaka umefanya kazi nyingi ikiwemo Buzwagi na Mabilioni ya uswiss, hakuna asiyekujua
Ni ushauri tu usijisikie vibaya ,ongeza juhudi kulipigania Taifa badala ya kutafuta nani ni bora .....
Msem kweli ni mpenzi wa Mungu
[HASHTAG]#TeamNyalila2020[/HASHTAG]