Pamoja na kuitafuta miaka yangu hii ya 60 bado nikipanda Dala Dala nawapisha Wazee, ila Vijana 'mnauchuna' tu Vitini

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,738
109,175
Ndiyo maana mnaishia tu Kuvuta Bangi, Kupewa hovyo Mimba, mnafeli hovyo Mashuleni, Akili hamna huku wengine mkipenda kuwa kama Dada zenu wakati ni Watoto wa Kiume.

Nidhamu ni Ufunguo wa kila Jambo na chanzo cha Baraka Maishani hasa ikionyeshwa na Mtoto / Kijana mbele ya Wakubwa zake hata kama siyo Wazazi wake.

Haiwezekani GENTAMYCINE nimepanda DalaDala ambalo lina Vijana wa Kiume na Like wengi ( tena Wanafunzi ) tena nimekaa Siti ya Nyuma halafu anapanda Bibi na Wanamchunia kabisa hadi Mimi wa nyuma nikampisha akakaa na nikasimama hadi mwisho wa Safari.

Halafu kila Ijumaa, Jumamosi na Jumapili mnaenda Kuswali / Kusali kwa Mungu. Hivi mnadhani Mwenyezi Mungu ni Mwendawazimu na Juha kama mlivyo kwa Nidhamu zenu hii mbaya na Unafiki kabisa awapeni Baraka zake na mfanikiwe?

Hovyo kabisa......!!!!!!
 
Mimi niko 20+ ila sikupishi kwa daladala hata iweje mkuu, yaani wewe unaona daladala imejaa unajipandisha huko kwenda kutegemea Huruma? Aisee hapana utasimama hadi ujute kwenye gari sote ni abiria hakuna kijana wala mzee ndio maana nauli tunalipia sawa, ila mwanafunzi sawa apishe wazee maana yeye analipa nusu nauli.
 
Kuna comments ukisoma badala uhuzunike unabaki kucheka tu,Kama hii.

Kijana Kama mzee mwenyewe ndiyo Mimi na hutaki kunipisha nikae,hakika nakushusha busha/mshipa kimo Cha ndoo ndogo ya sadolin ili usinyanyuke kabisa hapo kwenye kiti wallahi.

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu punguza hasira, wazee mim nimepambania hadi nimepata siti wewe uje uninyanyue tu kirahisi hapana aisee, tena kama nimekaa ya dirishan ndio kabisa nafunga macho kujifanya nimelala kabisa
 
yani unatoka masaki unaitafuta Gongo la Mboto.. Kutokana na uchovu wa kazi nzito na kupigika kazini unaona hapa nijisogeze kidogo kituo cha nyuma nizunguke na gari, unatulia zako kweny siti unanyosha kiuno unawaza ya kwako. Mbele kidgo baada ya gari kugeuka anakuja mzee mweny kanguvu zake anakusimamia kwenye siti yako kihuruma.. Dah wazee embu mtusamehe muda mwingine maana mtatupa laana za bure.

Binafsi huwa nawapisha watu wazima ila napima na utu uzima wao na namna ya upatikanaji wa gari haiwezekan gari zipo za siti haupandi uje upande lile limejaa kwa advantage ya uzee nitakupisha siti, aisee sifumbi macho wala sivai earphone ndo kwanza nakukodolea macho unavoteseka kwa kusimama.
 
Back
Top Bottom