Vijana mnaooa na kufunga ndoa miaka hii, mnakera sana

Fall Army Worm

JF-Expert Member
Jan 8, 2015
19,331
14,259
Wapendwa hbr za jioni?,Poleni kwa majukumu ya siku nzima.Bila kupoteza Muda nianze kwanza kwa ku declare interest kuwa mimi ni Muumini wa dini ya Kikristo,Kanisa Katoliki.Hivyo ninapenda sana Vijana wanaooana kwa kufunga kwanza Ndoa Kanisani au Msikitini,Maana wanatimiza kile Mungu anataka,hivyo ni Jambo la Baraka.

Lakini Kuna Jambo huwa sipendezwi nalo;Unakuta Kijana hajajipanga,Badala yake anategemea watu Wengine ndio wampige jeki, hii si sawa.

Mimi Wakati nafunga Ndoa sikuwasumbua watu,Watu wa Karibu yangu nilipokuwa naishi na kufanyia Kazi walijikusanya wenyewe wakaunda Kamati nami nikaweka Kiasi cha pesa mezani nao wakachangia kuongezea, kimsingi niliwashirikisha tu wale wa Karibu yangu mahali nilipo,wale wa mbali sikutaka kuwasumbua Kwasababu niliona sio fair.

Sasa siku hizi unakuta mtu yupo Mwanza anaomba mchango wa harusi kwa mtu yupo Mtwara,huu ni usumbufu Kwasababu yule wa Mtwara ataombwa Mchango pia na watu wa pale anapoishi.

Jambo la pili linalonikera,unakuta Kijana huyo hakuwahi kukutafuta siku za nyuma ili kujuliana hali,lkn Harusi yake ikishakaribia anakutafuta kukuomba Mchango wa Harusi yake,Hapa na pale utachangia,Sherehe zikiisha,anakata tena mawasiliano unakuta hana muda na wewe Kabisa,hata akisikia unaumwa hawezi kukumbuka angalau hata salamu za pole tu.Kiufupi unakuwa wa Muhimu tu wakati anataka kufanikisha sherehe yake.Huu ni Uchuro mnakatisha sana tamaa.

Tatu ni ishu ya Viwango vya Mchango, Mtu yupo Dar anakutumia Mchango mtu upo Songea kuwa ni Tshs.100,000/=,ili hali anajua fika kuwa hutashiriki na ukijitahidi ukalipa hata nusu yake ataendelea kudai utadhani ni deni, huu ni upuuzi, nikikuchangia Kiasi chochote kwa vile sitashiriki Kwenye sherehe yako,basi tosheka nacho.

Jambo la mwisho linalonikera,utakuta mtu anakuunga Kwenye kamati ilihali upo mikoa ya mbali Kabisa,sasa hivyo vikao vya Kamati utahudhuriaje?,Siku ya sherehe watakupanga Kwenye sekta ipi Wakati hautakuwa eneo husika? Halafu kwanini unipange Kwenye Kamati pasipo ridhaa yangu?.Huu ni ujeuri.

Rai yangu kwa Vijana; Ndoa ni Jambo Takatifu,Sherehe za Ndoa zisigeuzwe kitega Uchumi.Pili Waheshimuni sana wanaowachangia kufanikisha Sherehe zenu za Harusi,msigeuze watu tissue paper Kwamba ikishatumika unaitupa Kwenye dustbin, hii inavunja sana moyo.

Yangu ni hayo tu kwa leo, kama kuna Mwingine amewahi kukerwa km mimi Fall Army Worm Karibu,tuwaonye Vijana.
 
Ni point ya msingi sana!

Mtu anataka kuowa anataka sherehe ya Tsh 18mill akiulizwa mezani unaweka bei gani anasema 500,000/= hizo 17.5mill zitatoka wapi anasema kwa ndugu na jamaa utafikiri aliwapa wamshikie,baada ya muda anaanza kuwakimbiza watu mchaka mchaka.

Nadhani ilikuwa jambo la busara kama mtu anataka watu washiriki ktk sherehe yake yeye awape card yenye maelezo yote tarehe ya sherehe ukumbi wapi etc kisha awaache waamue kuchanga au kutochanga siyo kuzidisha kuwasumbua kila mara simu au sms,nimelala usiku naamka asubuhi nakutana na msg ya ada ya mtoto na ya mchango wa harusi naapa sitaacha kukutukana.
 
Jamani natarajia kufunga ndoa muda si mrefu! Nimekuwa na marafiki wengi humu janvini kwa IDs za kuficha uhalisia kama ilivyokawaisa ya JF. Nikiwapitishia ombi la michango nitawakwaza?
 
Hujalazimishwa changia
Una uhuru wa kukubali au kukataa
Once ukishapewa card ukaipokea hapo hapo unapokwa uhuru wako,kila saa simu au text kukukumbusha mchango.

Nipe kadi halafu kaa kimya kama kunikumbusha nikumbushe mara moja tu nisipo-respond kausha subiri siku ya ndoa yako kafurahi na waliokuchangia maana wao walitaka kushiriki unajuaje kama sipendi sherehe ndiyo maana sitaki kukuchangia?
 
Once ukishapewa card ukaipokea hapo hapo unapokwa uhuru wako,kila saa simu au text kukukumbusha mchango.

Nipe kadi halafu kaa kimya kama kunikumbusha nikumbushe mara moja tu nisipo-respond kausha subiri siku ya ndoa yako kafurahi na waliokuchangia maana walitaka unajuaje kama sipendi sherehe ndiyo maana sitaki kukuchangia?
Ndio maana nimesema si lazima
 
Back
Top Bottom