Hapa tunaongelea hali kiujumla, wewe unaongelea isolated cases za watu wachache wanaoporomosha mijengo na kuweka swimming pool ambao huenda ni walewale walamba asali ambao wana kamba za kujipimia. Tunapoongelea hali ya kiuchumi au hali ya maisha tunakuwa tunalenga nchi kwa ujumla wake, Je ni asilimia ngapi ya wananchi wanamudu angalau zile gharama muhimu za kujikimu kimaisha?Kuna wakati ukiona maisha magumu usifikiri na wenzio wanalia kilio hichohicho unaweza kujikuta uko peke yako na unapolalamika wenzio wanajifanya mnalalamika wote kumbe wanakuchora.
Kuna wakati tujikite kutafuta mbinu za kutukwamua na kuendana na kasi ya ulimwengu, vinginevyo hii dunia itakutesa peke yako.
Wakati unalalamika maisha magumu kuna wenzio kule Mbweni, Goba, Madale nk wanashusha maghorofa na kuweka mpaka swimming pools.