Safari Yangu Kutoka Lilongwe Hadi Dar es Salaam: Je, Umewahi Kuwa na Imani Kali Kiasi Hiki? 😂 Noma sana
Mwaka fulani nilikuwa Malawi, mjini Lilongwe Wakati huo nilikuwa na miaka 14, naelekea kutimiza 15
Nilikuwa nimeenda likizo, ikafika muda wa kurudi Tanzania
Mama akanipa nauli na kuniambia:
Shika hii pesa vizuri, nenda ukate tiketi.
Kwa nini hakunisindikiza sitasema leo. 😅
Basi nikachukua begi langu lenye nguo chache na mkoba mdogo uliokuwa na pesa za nauli, pesa ya kula, pamoja na kibari changu cha kusafiria Malawi
Nikafika stand ya Lilongwe ambapo magari ya Dar es Salaam yalikuwa yanapatikana
Kipindi hicho kulikuwa na kampuni moja maarufu sana, Taqwa
Sasa sijui ilikuwa bahati mbaya, uzembe sielewi mpka leo nilipochunguza mkoba wangu nikakuta umepotea 😭
Pesa zote zimeenda
Kibari kimeenda
Nauli imeenda
Kila kitu kimepotea
Aisee nilichanganyikiwa vibaya sana. Nikalia mpaka macho yakachoka
Lakini jambo moja nililokuwa na uhakika nalo ni hili
Sirudi nyumbani
Na hii ni hata leo nikisema hapana ni hapana
Kwa sababu mama yangu alikuwa mkali sana
Nilijiona nikirudi kumwambia nimepoteza nauli basi hakuna rangi ningeacha kuona
Nikajiwaza🤔
Kati ya kukutana na mama au kuvuka mipaka bila pesa, bora nijaribu bahati yangu
Nikajikaza nikamfuata dereva
Nikamsalimia kwa heshima zote za dunia
Shikamoo
Akanijibu
Marahaba binti, unasemaje?
Hapo ndipo nilipoanzisha filamu yangu ya kwanza ya maisha Uongooo pro 🤣
Nikaanza
Mimi nilikuja Malawi kufanya kazi za ndani : Astghafirullah 🙌
Dereva aliposikia hivyo akasema
Hebu njoo huku kidogo
Tukakaa pembeni
Sasa hapo nikaanza kusuka hadithi ya uongo kwa kasi ambayo hata nikikumbuka nachoka maana uongo sio tabia yangu mtu muongo na mnafiki hawajaachana mbali
Nikamuambia bosi wangu ananitesa sana, nimeamua kukimbia na kurudi Tanzania lakini sina hata senti
Dereva akaniangalia, akaangalia sura yangu ya mtoto mtulivu, akasikitika
Akamwita konda
Wakakubaliana kunibeba bure.
Mimi ndani ya moyo nikasema:
Asante Mungu, operation usirudi kwa mama imeanza rasmi🤣
Safari ikaanza
Usiku ulivyoingia, konda naye akaingia kwenye shughuli zake akanisahau kabisa kuhusu chakula
😭
Lakini Mungu alikuwa mbele
Nilikaa karibu na kaka mmoja ambaye kila alichonunua alikuwa ananipa sehemu bila kuniuliza hata MashaAllah 😍
Nilikuwa nakula kama nimepewa huduma ya full board😂
Tulipofika Karonga polisi wa Malawi walikuwa wanakagua
Konda akaniambia
Shuka ujifiche kwanza he kasheshe
Nikashuka
Ukaguzi ukaisha
Yaani simple tu ikawa imeisha hiyoo
Nikapanda tena
Mpaka leo nikiikumbuka najiona kama nilikuwa kwenye mission ya siri 🤣
Lakini ni kasheshe la kweli lilikuwa
Linaendela nahisi ningefaa kwa ujasusi🤪
Konda akasema shuka
Sisi tutapita hapa rasmi, wewe shuka upande ule vuka kwa mtumbwi 🙄
Nikabaki namtazama
Mtumbwi? Mimi ambaye hata kuangalia maji kwa muda mrefu naogopa? 😭
Akanipa hela kidogo ya kuvukia
Nikakuta mzee wa mtumbwi yupo tayari kazini Inaonekana ni michongo yake
Nikapanda
Tukiwa katikati ya mto nikaanza kuona mbele polisi kama anatusubiri kabisa 😂😂😂 heh
Moyo ukaanza kwenda mbio kuliko mtumbwi
Nilipofika upande wa pili, kweli polisi akaniita
Umetoka wapi?
Malawi
Ulikuwa unafanya nini?
Hapo nikarudia script ile ile akili mtu wangu 🤭
Nilikuwa nafanya kazi za ndani, bosi ananitesa, nimekimbia 🤣
Akauliza kitambulisho
Hakuna
Kibari
Hakuna
Simu
Hakuna
Kila kitu kilikuwa hakuna😂
Yule polisi akaniangalia halafu akasema
Wewe mtoto una ujanja sana
Akaandika namba yake kwenye karatasi na kuniambia
Ukifika Dar nitafute🤣😒
Mimi nikasema sawa, lakini kichwani nilikuwa nawaza basi lisiniondokee tu
🤣
Nikakimbia mpaka sehemu niliyoelekezwa
Baada ya muda gari likafika
Nikapanda
Safari ikaendelea mpaka Dar es Salaam
Leo nikikumbuka hii safari, najiuliza nilikuwa na ujasiri au nilikuwa na hofu ya mama yangu? 😂😂😂
Mom S 🥹🙌
Kwa sababu uongo wote huo, mipango yote hiyo, kuvuka mipaka, mtumbwi, polisi na hatari zote hizo tena mtoto wakike mdogo baso sijakomaa sura katika ya majangili (wanaume jokes)
chanzo chake kilikuwa kimoja tu
Mama yangu alikuwa mkali mno! 😭😭
Lakini pamoja na yote
Mama, nakupenda sana ❤️ ila ukweli ni kwamba ulikuwa mkali mnoooo!