kali linux
JF-Expert Member
- May 21, 2017
- 2,301
- 6,114
PART 1:
Hello bosses and roses....
Leo nimejaribu kuingia jamiiforum bila VPN na ikakubali, hongera sana kwa boss kubwa Maxence Melo na team yote ya JF, nina muda sana sijaandika makala humu, naomba niandike makala hii labda itawasaidia baadhi ya watu
Daah, maisha haya ni fumbo sana.
Ni zaidi ya miaka mitano imepita sasa toka nipitie hali ya kuumwa ambayo haikua ya kawaida.
Hali ambayo kila niliokuwa namsimulia hanielewi na anasema nimerogwa wengine wakasema naigiza
Hali ambayo hadi baadhi ya madaktari waligiveup.
Nililelewa na mzee wangu ambae alinifundisha kutoonesha weakness hasa kipindi naumwa, nakumbuka niliwahi kaa na malaria hadi siku kdg nizimie ndipo nikasema, nadhan ndio hali ilionifanya watu kutoamini kipindi naumwa sabb kwa nje nilionekana mkakamavu ila kwa ndani nilikua nimeisha.
Mishipa yangu ya fahamu ilikua inazidi kudhoofika kila siku...
usikivu ukaisha kabisa, nikawa sisikii....
nikashindwa kushika vitu, misuli ya tumboni na kiunoni nikaacha kusikia kabisa, miguu ikawa kama sio yangu na ilifikia hatua sikuweza kutembea bila support.
Nilifikia hali ya kukata tamaa, niliona ndoto zangu zimeishia pale. Nilianza kuogopa hadi kulala sababu nikilala na kuamka mwili wote unakua umekufa ganzi hadi misuli ya kichwani, kuanzia hapo nikaanza kuogopa kulala, nikihofia siku moja naweza kutoamka sabb ya hali ile ambayo hakuna mtu aliekuwa anaielewa.
Sikuwah kutegemea siku ningepelekwa Kawe kwa mwamposa, ila kudadeki nilipelekwa tena kwa lazima bila utashi wangu sababu waliokua wananiuguza hawakuona matumaini.
Siku moja nikapata nguvu nikaenda kwa pastor mmoja hivi wa kilokole ambae kdg anahubiri bila maslahi ya dini husika, nilivutiwa na pastor huyo sababu siku za nyuma niliwahi kumsikia akiongelea kuhusu meditation, na alitoa funzo kubwa sana kuhusu meditation kwa kusema "Wengi tuna-meditate bila kujua"
Baada ya kumwelezea hali yangu pastor alinambia kwamba "Kali Linux, uhai wako ni jukumu lako, upiganie, mwambie Mungu sitaki kufa sasa hivi"
Siku chache baadae nikakutana na daktari alieweza ku-decipher vipimo na kujua ugonjwa uliokuwa unanisumbua, CIDP.
CIDP naweza sema sio ugonjwa ni ile hali ya mwili wako kuwa na kinga yenye nguvu kupitiliza kiasi kwamba kinga hio inaanza kuzipiga seli zinazounda mishipa ya fahamu.
Seli hizo huwa zinazunguka neva na kuwa sehemu ya myelin sheath ambazo ndio cover ya nje ya neva, chukulia kama neva ni waya basi myelin sheath ni ile cover ya nylon au plastic nje ya waya ambayo ikitoboka basi inaweza sababisha shoti, na kwa mwili wa binadam hio ikitoboka basi taarifa zinazosafirishwa na neva zinakua zinapoteza signal na ndio chanzo cha kutosikia, kutoona vizuri na ganzi kwenye viungo vingi mwilini. Hali hii haiambukiziki bali mtu anazaliwa nayo, hivyo ni vema kwa wazazi kuwapima watoto wao mwanzo kabisa kujua kama wana hio hali endapo mtoto ataonesha dalili za kuwa na ganzi za mara kwa mara, usikivu au uonaji dhaifu, na hali nyinginezo zinazohusishwa na usafirishaji wa taarifa mwilini.
ITAENDELEA...
~ kali linux