Padre 'ajilipua' kwa askofu Mwamakula kuhusu "Matembezi ya hiari"

Kazi ya kiongozi wa kikristo ni moja tu kuwaambia watu tubuni na kuiamini injili...
Yesu alipokuwa anatangaza amani alikuwa anatangaza kuheshimiwa kwa Katiba kwa nchi ambazo zitakuwa na Katiba kwa kuwa Katiba ndio makubaliano ya namna ya uendeshaji wa taasisi au nchi. Kiongozi wa dini anayetaka kuandikwa kwa Katiba inayobeba matakwa ya jamii, huyo anakuwa anafanya kile kile ambacho kimefanywa na Yesu zaidi ya miaka 2000 iliyopita.

Huyo "mtaalamu mmoja" atakuwa ni zwazwa kwa sababu hajui kwamba wakati kila mmoja anatakiwa asimame katika nafasi yake, wengine wakiwemo maaskofu nafasi yao ni pamoja na kufanya "checks & balance", na wanapohamasisha kuandikwa Katiba mpya na au kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi wanakuwa wanatekeleza hilo!
 
Ninachokiona kwa wafuasi wa watawala na serikali za ki Africa ni kutokupenda kitu kinachoitwa HAKI kwa kila mwananchi, hata wale walio nje ya system. Wanajisikia kichefuchefu pale KATIBA ya nchi na TUME ZA UCHAGUZI zinapotoa haki kwa wananchi wote bila kubagua.

Tambo zenu za kuwa babkubwa zingelikuwa na mashiko, kama tu wananchi wangekuwa sawa katika vyombo vya dola na vya maamuzi. Lakini hii ya kuwa na watu special ni kujidanganya nafsi na kuwaumiza wengine wenye mawazo tofauti. Mfano wa Mtikila na hata Kolimba si ushujaa zaidi ni uoga.

Odhis *
 
Kazi ya kiongozi wa kikristo ni moja tu kuwaambia watu tubuni na kuiamini injili..
Hivi kuna sehemu kwenye Biblia au Quran inasema watawala wa viongozi waapishwe kwa hivyo vitabu vitakatifu?
Unaweza kuitenganisha Siasa na Dini?

Viongozi wa dini wanashiriki Siasa kwa kuwaasa waumini kulinda amani,kutenda haki,kupiga kura,kuandaa viongozi nk Hivi kuna sehemu vimeandikwa kua viongozi watapewa tuzo na viongozi wa dini?

JPM amepewa tuzo na dhehebu flani ambalo linajijua lenyewe..vipi ulikosoa na kupinga ilo au kwakua tukio ilo lilikua la kumfuriaisha kipenzi basi ukaona ni sawa!

Leo Askofu Bandekile akianza kusifia mtawala au kumuita kua ni yesu utaweza kupinga?
 
Ninachokiona kwa wafuasi wa watawala na serikali za ki Africa ni kutokupenda kitu kinachoitwa HAKI kwa kila mwananchi, hata wale walio nje ya system. Wanajisikia kichefuchefu pale KATIBA ya nchi na TUME ZA UCHAGUZI zinapotoa haki kwa wananchi wote bila kubagua...

Sumu ni nzuri sana pale inapotumika kufanya kazi iliyokusudiwa na ni mbaya sana inapotumika kufanya isichokusudiwa

Haki na wajibu vinaenda pamoja, kutumia neno haki kuvunja taratibu na kuhujumu nchi haviwezi kubalika na wastaarabu wa nchi yoyote duniani.

Watu wanaweza kuua watu lakini serikali ya Tanzania haiwezi na haijawahi tumia vyombo vyake kuua watu uliowataja.

Mheshimiwa Mwakyembe aliwahi nusurika kifo, je serikali ndio ilitaka kumuua? Mheshimiwa rais aliwahi ongelea kupewa sumu, je serikali ndio ilitaka kumuua?

Tujifunze kuwajibika kwa matendo yetu zaidi ya kulaumu serikili kwa kila kitu
 
Yesu alipokuwa anatangaza amani alikuwa anatangaza kuheshimiwa kwa Katiba kwa nchi ambazo zitakuwa na Katiba kwa kuwa Katiba ndio makubaliano ya namna ya uendeshaji wa taasisi au nchi. Kiongozi wa dini anayetaka kuandikwa kwa Katiba inayobeba matakwa ya jamii, huyo anakuwa anafanya kile kile ambacho kimefanywa na Yesu zaidi ya miaka 2000 iliyopita. Huyo "mtaalamu mmoja" atakuwa ni zwazwa kwa sababu hajui kwamba wakati kila mmoja anatakiwa asimame katika nafasi yake, wengine wakiwemo maaskofu nafasi yao ni pamoja na kufanya "checks & balance", na wanapohamasisha kuandikwa Katiba mpya na au kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi wanakuwa wanatekeleza hilo!
kazi ya askofu si kusimama kwa niaba ya watu anasima kwa niaba ya Mungu.Kazi za kusimama kwa niaba ya watu ni za wanasiasa wakiwemo wabunge ,wanaharakati nk

Yesu aliona wazi katiba ilikuwa mbaya lakini msikilize hapa alichoongea akasema ya Mungu yabakie ya Mungu na kaisari yabakie huko kwa Kaisari

Ulaya makanisa yamekufa yalipojiingiza kwenye siasa hamna watu wanasali makanisani tena waklijitia ohh kanisa linatakiwa kushiriki siasa vikaanzishwa hadi vyama vya kidini mfano ujerumani chama tawala kwa sasa kinaitwa CHRISTIAN DEMOCRATIC UNION cha ANGELA MERKEL .WAtu wakahamasika kweli kuihoji serikali lakini mwamko huo ukaenda mbele zaidi watu wakaanza kuhoji mambo ya kanisani ikiwemo doctorins kwa kisingizio kile kile kuwa kama maaskofu wanahammisaji watu kuhoji serikali bunge na mahakama kwa nini kanisa lisihojiwe?

Maaskofu wakaanza kuwekwa kitimoto!!! La kwanza lilihojiwa ni kuwa kulikuwa na kodi mbili kodi ya kwanza unakatwa kwenye mshahara inaenda serikalini na kod ya pili unakatwa kwenye mshahara inaenda kanisani .Wakaenda bungeni kupinga kuwa si kila mtu anasali hiyo kodi ikatwe tu kwa wanaosali.

Ikapita watu walipoona wasiosali hawakatwi kodi wengi wakaacha kusali ili wasikatwe kodi ya kanisa!!! Sasa hivi mikanisa mingi ulaya haina waumini na yanauzwa kwa minada hata ukiingia goole iko kibao ,Michungaji na miaskofu kibao ikaachishwa kazi sababu mikanisa haina hela za kuwalipa!!!

Sasa hivi chama cha siasa cha CHristian Democratic UNION ndio kimenawiri kanisa limesinyaa!!!

Huyo ASkofu mwamakula ona watu wanavyofurika mikutano yake ya siasa !!! Ajaribu kuitisha mkutano wa injili uone hapati mtu!!! Mchungaji Mtikila pia alikuwa na hilo tatizo watu wanajaa mikutano yake ya siasa ukienda kanisani kwake Ilala boma anasali yeye mke wake na nduguze hawafiki wanne!!! HAYO NDIO YA askofu Mwamakula uliza kanisa lake hata liko wapi hakuna humu anayeweza hata kukuonyesha !!! unaishia kuona tu kavaa minguo ya kiaskofu aliyojishonea mwenyewe kwa fundi cherehani

Hii trend ya maaskofu kujitosa kwenye siasa sio nzuri kwa afya ya kanisa in the short run and in the Long run time
Kiongozi wa dini abaki kanisani
 
kazi ya askofu si kusimama kwa niaba ya watu anasima kwa niaba ya Mungu.Kazi za kusimama kwa niaba ya watu ni za wanasiasa wakiwemo wabunge ,wanaharakati nk.....
Kwani mikutano ya injili au kanisa niya Askofu?

Gwajima yupo Bungeni nani Askofu wa Kanisa ingawa aliwai kukashfu Ukatoliki kua ni dini ya Uongo na Uislam kua ni dini ya mashetani. Nini msimamo wako?

Alafu kutoa mifano ya nchi za kibeberu na huku Tanzania sio sawa.

Vipi Bishop Desmund Tutu alikua anakosea kupinga uonevu na ubaguzi wa rangi?

Vipi marehem Papa Paul ii alikua anakosea kuwatetea wapalestina dhidi ya dhuluma ya Israel?
 
Hivi kuna sehemu kwenye Biblia au Quran inasema watawala wa viongozi waapishwe kwa hivyo vitabu vitakatifu?
Unaweza kuitenganisha Siasa na Dini?....
Nianze hilo la kuapishwa kwa vitabu vya dini.HUYO MWAPISHAJI MWENYEWE HUWA SIO KIONGOZI WA DINI!!!!! au hujaliona hilo? Kinachofanyika wanakijua wenyewe acha kuhusisha viongozi wa dini kwenye hilo.mTU SI KIONGOZI wa dini anasimama mbele ya mtu asiye kiongozi wa dini kuapa utasemaje hapo kuwa viongozi wa dini wanaapisha?

Pili kuhusu kanisa kumpa TUzo Raisi MAgufuli ,Lilikuwa kanisa la ASSEMBILIES OF GOD.Lile kanisa wanajielewa sana.Wanaamini sana kwenye kumuomba Mungu kwenye utatuzi wa changamoto za maisha.Ni waombaji sana.Sasa ugonjwa wa Corona ulivyokuja nchini Raisi aliitisha maombi ya siku tatu ya kufunga na kuomba Mungu aondoe Corona Tanzania.

Na wao wakashiriki yale maombi.Sasa sababu imani yao ya kidini inaamini kwenye maombi na raisi aliomba pamoja nao ndio wakampa tuzo kama mwanamaombi mwenzao aliyetoa wito wa maombi nchi nzima.Hapo haikuwa tuzo ya kisiasa bali ya kimaombi ilikuwa njia ya kusema asante kwa kuomba pammoja nasi na kutambua Mungu kuwa ni jibu la changamoto ya Corona wakati wengine hawaamini kuwa Mungu ni jibu wanaamini tu sayansi!!!
 
Nianze hilo la kuapishwa kwa vitabu vya dini.HUYO MWAPISHAJI MWENYEWE HUWA SIO KIONGOZI WA DINI!!!!! au hujaliona hilo? Kinachofanyika wanakijua wenyewe acha kuhusisha viongozi wa dini kwenye hilo.mTU SI KIONGOZI wa dini anasimama mbele ya mtu asiye kiongozi wa dini kuapa utasemaje hapo kuwa viongozi wa dini wanaapisha?....
Umejibu post/maswali yangu au nini hiki? Vipi ,uliwai kuhoji au kuwakataza kua kwanini wanatumia vitabu vya Dini wakati hao si viongozi wa Dini?

Sasa kuna tofauti gani kati yao na Askofu Mwamakula maana na yeye anataka Taifa liwe na Katiba Mpya ili watu waishi kwa haki na Taifa lipige hatua kwenye Demokrasia. Anataka Tume Huru ili tuondokane na lawama kwenye Uchaguzi.

Hivi mchungaji Martin Luther alikua anakosea kama kiongozi wa dhehebu/ dini kupinga ubaguzi Na kudai usawa?
 
Vipi Bishop Desmund Tutu alikua anakosea kupinga uonevu na ubaguzi wa rangi?
Vipi marehem Papa Paul ii alikua anakosea kuwatetea wapalestina dhidi ya dhuluma ya Israel?
Niseme wazi ASkofu Tutu alipoteza muda na nguvu bure aliokuwa akiwatetea mbona ndio wabaguzi wakubwa wa waafrika wenzao.Afrika kusini sasa hivi waafrika toka mataifa mengine wanabaguliwa kuuawa na maduka kuchomwa moto na waaftrika weusi wenzao.Ulishasikia wazungu waafrika kusini wamepiga waafrika weusi wahamiaji toka mataifa mengine Afrika ya kusini?

Waafrika kusini weusi ni wabaguzi hatari sasa hivi acha tu watanzania tuliwasaidia kuanzia vita hadi kujitolea damu hadi kuwahifadhi kama wakimbizi mazimbu morogoro nk lakini wakuone sura yako mtanzania kule utakoma.Uonevu upi alipinga mbona wao wanatufanyia uovu sasa na unajua Desmund Tutu ni mzima hajafa mbona hatoi tamko? Yeye kama kiongozi wa dini alitakiwa tu kukomaa kuhubiria makaburu na wesi kuwa Tubuni na kuiamini injili wakitubu na kuiamini ubaguzi ungekoma automatically bila kelele wala risasi kurushwa wala maandamano

Pili kushinda kwake kwenye siasa kulifanya kanisa lake la Anglikani Afrika kusini liharibike wameruhusu ndoa za jinsia moja!! na yeye mwenyewe aliishia kashfa ya kuzaa nje ya ndoa akakubali wakamvua uaskofu aliharibikia huko kwenye siasa akakutana na vimwana vikamvua joho !!!

Kuhusu papa kutetea wapalestina jibu liko pale pale alitakiwa asimame ahubiri kuwa wapalestina na waisraeli tubuni na kuiamini injili.Wakitubu na kuiamini tatizo la wapalestina na waisrael litaisha automatically, hata yeye papa kama ninavyompinga Mwamakula na yeye nampinga msimamo wake wa kuwa na upande kwenye mgogoro wa Israel na wapalestina.Hatakiwi kuwa na upande!!
 
Kwahiyo marehem Mzee Mkapa alitudanganya aliposema anajuta watu wazanzibar waliouwawa na polisi wakati wa Utawala wake?
Moja ya wajibu wa raia na kulinda HAKI yake au na ili ulijui?
Kiongozi sahihi, imara na makini ni yule anayeweza kuyaona makosa yaliyo ndani ya mfumo, asiyekubali na akayafanyia kazi makosa hayo hata kwa gharama ya kuwajibika yeye na kuwajibisha watendaji wake. Na hicho ndicho aluchofanya Mkapa.

Raia wanalinda haki bila kuvunja sheria
 
Umejibu post/maswali yangu au nini hiki?Vipi ,uliwai kuhoji au kuwakataza kua kwanini wanatumia vitabu vya Dini wakati hao si viongozi wa Dini?
Sasa kuna tofauti gani kati yao na Askofu Mwamakula ...maana na yeye anataka Taifa liwe na Katiba Mpya ili watu waishi kwa haki na Taifa lipige hatua kwenye Demokrasia. Anataka Tume Huru ili tuondokane na lawama kwenye Uchaguzi.
Hivi mchungaji Martin Luther alikua anakosea kama kiongozi wa dhehebu/ dini kupinga ubaguzi Na kudai usawa?
Vitabu vya dini sio miliki ya mtu au dini fulani ni vya Mungu na vinauzwa madukani ndio maana waweza kuta mkristo ana kurani nyumbani na mwislamu ana biblia nyumbami na hata vyuo vya kipagani hutumia Biblia kufundishia English Literature!!! HUwezi kuzuia mtu asinunue!!!

Pili sio kazi ya kanisa kuiiga dunia inachofanya!!! Wao ndio wanatakiwa kuiga kanisa!! HUwezi sababu wao wanatumia kitabu cha dini hivyo ruksa kiongozi wa dini na yeye kufanya siasa!!! kisa kaona dunia inatumia kurani au Biblia kuapa!!! Ni upotofu !!! Ndio maana zamani maakofu na mapadre walikaa mbali na dunia .Misheni unazikuta ziko porini kwenye ukimya ambako hapati nafasi ya kusikiliza radio,TV, magazeti mitandao na ku interract na watu nk abaki na Mungu tu
Lakini toka hayo yameachwa ndio haya matatizo yameanza kuibuka ya kiongozi wa dini kuwa sehemu ya dunia aki interract na watu!!! NDio unaona tunapata wanasiasa,wazaa nje ya viapo vyao,wabaka watoto wadogo nk wanaiga dunia inachofanya!! Haitakiwi kuiga dunia!! Kuapa kwa Biblia au Kurani hakumpi uhalali kiongozi wa dini kujitosa kwenye siasa!!

Kuhusu Martin Luther mwanzilishi wa kanisa la kilutheri anachokumbukwa ni kuigania mambo ya kidini sio siasa!! Kanisa la kilutheri msingi wake ni wa kidini tu .JINA kanisa la kilutheri ni kama sisi siku hizi tunasema kanisa la Gwajima au kanisa la kakobe sasa hilo lilitwa kanisa la LUTHER la mtu anaitwa Luther NDIO WAFUASI WAKE wanaitwa LUTHERAN kama leo tunavyosema wafuasi wa KAkobe AU WAFUASI WA GWAJIMA NK
 
PADRE 'AJILIPUA' KWA ASKOFU MWAMAKULA KUHUSU "MATEMBEZI YA HIARI"

Nathan Peter (pichani) au Padre Haule ambaye ni Kasisi wa Kanisa Anglikana Tanzania ameamua kujilipua kwa kuandika yafuatayo katika kuchangia andiko langu katika ukurasa wangu:

"Kama unatumwa na wenye mihimili hiyo sawa usintamaze kwani nawe ni wao, lakini Kama unajituma , Anza kutafiti alipo mzee mtikila na anachokifanya kwa Sasa."

Maneno ya Padre huyo siyo ya kupuuza. Anagusia wenye mihimili na anaongea kuhusu Mtikila pasipo kumtaja Mtikila yupi! Inawezekana Padre anajua kilichompata Mtikila anayemtaja na sababu za kumpata hayo yaliyompata. Kuna uhusiano gani kati ya yaliyompata Mtikila na yanayoweza kumpata Askofu Mwamakula, hatujui. Labda Baba Padre anajua! Askofu anajua kuwa huyo Padre ni kada wa chama kimoja cha siasa nchini ingawa hajui uhusiano wake na hao wenye mihimili au Mtikila

Nilipokuwa mdogo, jirani kulikuwa na Kambi ya Jeshi kule Ipyana na Kibugujo (Kyela)! Tulifundishwa kutokuwapuuzia watu tukikutana nao maporini! Kuna mmoja alikuwa anajifanya kichaa na kuishi mwituni kumbe kule msituni alikuwa ameweka ofisi yake shimoni! Bila shaka ujumbe wa Padre kwa Askofu Mwamakula umefika!

Ni vizuri Padre na wengine wakatambua kuwa Askofu ataongoza hayo "Matembezi ya Hiyari" nchi nzima na wala hahitaji kufanya utafiti wa kazi anayoifanya huyo Mtikila aliyetajwa! Askofu alizaliwa siku moja na atakufa siku moja iwe kwa ugonjwa, risasi, sumu, ajali, uzee, au kuliwa na wanyama wakali, nk haijalishi!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula

View attachment 1680849
Mleta mada,

Umepata ridhaa ya huyo padri kuweka picha yake halisi kwenye jukwaa la watu waliojificha sura na majina yao?

Unavyoonesha kila ukilala, ukiamka, ukitembea, ukiongea, ukiwaza, ukisoma, ukiandika chochote unatamani kukutana na ujumbe unaosema vibaya serikali yenye mtizamo ulio kinume na wa kwako. Inavyoonesha wewe ni mhanga wa moja kwa moja au kuambukizwa kutokana na matendo ya viongozi wa serikali.

Unapenda sana kuwanukuu viongozi wa kidini (sio wa kiroho) wenye mtizamo kama wa kwako kisha unawakilisha kwenye jukwaa hili kwa taswira chonganishi ya kisiasa.

Kwa mada yako hii unaithibitishia jukwaa kwamba Mchungaji Christopher Mtikila aliuwawa na watu kwa sababu za kisiasa na sio ajali aliyopata huko Msolwa, Chalinze wakati akitokea Morogoro kwa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2015.

Kwa mantiki hiyo unaushahidi wa kutosha kwamba aliuwawa na sio ajali kama ilivyothibitishwa na hospitali teule ya Tumbi, Pwani pamoja na taarifa ya kamanda wa mkowa wa Pwani Jafari Mohamed.

Ingependeza zaidi ushahidi huu uupeleke polisi ili watu waliohusika kudhulumu nafsi ya mchungaji Mtikila ichukuliwe kwa haki.

Kumbuka: kwenye ajali hiyo mchungaji mtikila aliambatana na watu wengine wanne ambao walijeruhiwa. Gari lipinduka na watu waliokuwemo ndani baadhi walichomoka hadi nje na wengine kukandamizwa. Eneo ambapo ajali ilitokea inasadikika kuna mtu alikuwa anaonekana chini ya mti nyakati za usiku akioka moto kwa ajili ya kupika au kupata joto.

Uzoefu unaonesha kwamba eneo hilo ajali nyingi hutokea hasa wakati wa jioni au alfajiri asubuhi; kuna lori aina ya fuso lililokuwa limepakia wanyama aina ya nguruwe iliwahi kupinduka hapo lakini cha ajabu nguruwe walimwagika chini kisha wakawa wanazunguka zunguka gari lilipo mpaka ulipopatikana msadaa. Ukipita eneo hilo utaona upande wa magharibi kuna miti imewekewa vitambaa au chupa tupu za maji kana kwamba aliyefanya hivyo ni kichaa lakini huwezi kumwona mtu yeyote hata kama ukikaa hapo kusubiri kumwona.

Mjadala usipotoshe ukweli kwamba kilichotokea ni ajali; tizama picha ya gari husika hapa chini kisha ujitenge na chuki binafsi

1611037990723.png
 

Attachments

  • Mtikila.jpg
    Mtikila.jpg
    24.9 KB · Views: 1
Back
Top Bottom