Padre 'ajilipua' kwa askofu Mwamakula kuhusu "Matembezi ya hiari"

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,792
287,994
Nathan Peter (pichani) au Padre Haule ambaye ni Kasisi wa Kanisa Anglikana Tanzania ameamua kujilipua kwa kuandika yafuatayo katika kuchangia andiko langu katika ukurasa wangu:

"Kama unatumwa na wenye mihimili hiyo sawa usintamaze kwani nawe ni wao, lakini Kama unajituma, Anza kutafiti alipo mzee mtikila na anachokifanya kwa Sasa."

Maneno ya Padre huyo siyo ya kupuuza. Anagusia wenye mihimili na anaongea kuhusu Mtikila pasipo kumtaja Mtikila yupi! Inawezekana Padre anajua kilichompata Mtikila anayemtaja na sababu za kumpata hayo yaliyompata. Kuna uhusiano gani kati ya yaliyompata Mtikila na yanayoweza kumpata Askofu Mwamakula, hatujui. Labda Baba Padre anajua! Askofu anajua kuwa huyo Padre ni kada wa chama kimoja cha siasa nchini ingawa hajui uhusiano wake na hao wenye mihimili au Mtikila

Nilipokuwa mdogo, jirani kulikuwa na Kambi ya Jeshi kule Ipyana na Kibugujo (Kyela)! Tulifundishwa kutokuwapuuzia watu tukikutana nao maporini! Kuna mmoja alikuwa anajifanya kichaa na kuishi mwituni kumbe kule msituni alikuwa ameweka ofisi yake shimoni! Bila shaka ujumbe wa Padre kwa Askofu Mwamakula umefika!

Ni vizuri Padre na wengine wakatambua kuwa Askofu ataongoza hayo "Matembezi ya Hiyari" nchi nzima na wala hahitaji kufanya utafiti wa kazi anayoifanya huyo Mtikila aliyetajwa! Askofu alizaliwa siku moja na atakufa siku moja iwe kwa ugonjwa, risasi, sumu, ajali, uzee, au kuliwa na wanyama wakali, nk haijalishi!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula

24FC5C5F-F588-45EC-8378-C7FED43BB517.jpeg
 
"Kama unatumwa na wenye mihimili hiyo sawa usintamaze kwani nawe ni wao, lakini Kama unajituma , Anza kutafiti alipo mzee mtikila na anachokifanya kwa Sasa."
Sijaelewa kidogo.... usintamaze lina maana gani.

Ila nadhani anamtahadhalisha kuwa Mtikila, Mchungaji marehemu alikufa/aliuawa kwa vile alikuwa anaipinga serikali... mihimili ilimshughulikai (ndivyo nilivyoelewa) I stand to be corrected
 
Hiyo usintamaze hata mimi sielewi inamaanisha nini. Zipo tetesi kwamba Mtikila katika ile ajali yake ya gari ilikuwa ni mauaji yaliyofanywa na wasiojulikana. Bahati mbaya kama tujuavyo nchi yetu sasa hivi hata uchunguzi hakuna. Lissu walitaka azikwe haraka haraka, Ben Saanane, Azory na wengine hakuna hata uchunguzi wa kuzuga.

Sijaelewa kidogo.... usintamaze lina maana gani

Ila nadhani anamtahadhalisha kuwa Mtikila, Mchungaji marehemu alikufa/aliuawa kwa vile alikuwa anaipinga serikali... mihimili ilimshughulikai (ndivyo nilivyoelewa) I stand to be corrected
 
Hiyo usintamaze hata mimi sielewi inamaanisha nini. Zipo tetesi kwamba Mtikila katika ile ajali yake ya gari ilikuwa ni mauaji yaliyofanywa na wasiojulikana. Bahati mbaya kama tujuavyo nchi yetu sasa hivi hata uchunguzi hakuna. Lissu walitaka azikwe haraka haraka, Ben Saanane, Azory na wengine hakuna hata uchunguzi wa kuzuga.

RIP Mtikila
RIP Chacha Wangwe
 
Kazi ya kiongozi wa kikristo ni moja tu kuwaambia watu tubuni na kuiamini injili, kinyume cha hapo hamna kiongozi wa kikristo hapo ni mbwa mwitu tu aliye ndani ya uongozi wa kanisa

Hakuna kiongozi wa kikristo anayetumwa na Mungu kuhubiri kuhusu katiba au tume za uchaguzi sababu katiba duniani kila nchi ina zake na zinatofautiana kati ya nchi na nchi na tume zinatofautiana kati ya nchi na nchi na nchi zingine hazina kabisa sababu hazifanyi chaguzi hutawaliwa kifalme nk lakini injili ni ile ile kwa mataifa yote dunia nzima ndio maana Yesu akaagiza viongozi wake waende duniani pote wahubirie watu watubu na kuiamini injili ambayo ni ile ile jana leo na hata milel haibadiliki.Katiba zitabadilika injili haibadiliki.TUME ZA UCHAGUZI ZITABADILIKA INJILI HAIBADILIKI

Mtaalamu mmoja alisema ili nchi iendelee inatakiwa kila mmoja asimame kwenye nafasi yake afanye kile alichopewa mkulima alime sana kwa nguvu zake zote nk na akili zake zote na kiongozi wa dini asimame nafasi yake aliyopewa na Mungu
 
Mstake kutuumizia vijana wetu kwa starehe za wengine.

Akina Maalim, Kabwe, Mbowe, Mdee, Mbatia,washachukua luzuku na wanakula nchi kwa mrija.

Badala ya kuwahamasisha vijana wapigane ili kujiondoa katika lindi la umaskini mnawahamasisha matembezi ili wazidi baki katika ufukara wao, na hao waongezewe ruzuku.

Mpinzani wa Kweli alikuwa Mtikila tu hao wengine ni Wachumia tumbo tu.
Vijana Chapeni kazi.
 
Padre Nathan Peter Haule wa Anglican amenikumbusha neno hili kutoka katika kitabu cha 1Yohana4: 1-6 ambapo biblia inatukumbusha waumini Kuzipima Roho.

1Yohana4: 1-6
"1 Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zipimeni hizo roho, kama zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.
2 Katika hili mnamjua Roho wa Mungu; kila roho ikiriyo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatokana na Mungu.
3 Na kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani.
4 Ninyi, watoto wadogo, mnatokana na Mungu nanyi mmewashinda, kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia.
5 Hao ni wa dunia; kwa hiyo wanena ya dunia na dunia huwasikia.
6 Sisi tunatokana na Mungu. Yeye amjuaye Mungu atusikia; yeye asiyetokana na Mungu hatusikii. Katika hili tunamjua Roho wa kweli, na roho ya upotevu."


Unapokua muumini wa imani, iwe imani ya siasa au dini ni muhimu ujue kuzipima roho ili ufanye maamuzi sahihi

Mungu ibariki Tanzania
 
Hiyo usintamaze hata mimi sielewi inamaanisha nini. Zipo tetesi kwamba Mtikila katika ile ajali yake ya gari ilikuwa ni mauaji yaliyofanywa na wasiojulikana...
Hatujui hata kesho yetu
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom