Kyela: Polisi wavamia nyumbani kwa Askofu Mwamakula usiku wa manane

RWANDES

JF-Expert Member
Jun 12, 2019
1,615
3,909
Polisi Kyela walifika Itunge, Kyela katika Mkoa wa Mbeya nyumbani kwa Askofu Mwamakula, usiku huu majira ya saa 6:40 usiku. Walipofika waligonga mlango, walipofunguliwa wakaulizia Askofu. Ndugu walishangaa kwani hawakuwa na taarifa kama Askofu angekuwa kule leo au hata wiki hii.

Polisi hawakuridhika hadi ndugu walipompigia simu Askofu na kuongea nao huku Polisi wale wakisikia na ndipo wakajiridhisha kuwa Askofu hakuwa pale na pia hakuwepo Itunge leo. Polisi wa Kyela walitumwa na wakuu wao ili wafike katika Makazi ya Askofu yaliyoko Itunge, Kyela katika Isyeto (Makaburi ya Chifu Bandekile) ili kuona kama Askofu yupo pale. Haijulikani pia kama Polisi wale walifika katika mji mwingine wa Askofu ulioko Itunge. Tutajua baadaye.

Askofu aliongea na Mkuu wa Polisi (OCD) wa Kyela kwa namba ya ndugu aliyekuwepo. Lakini Askofu alipouliza walifuata nini usiku na kuwa walishindwa nini kumtafuta yeye mchana hata kumpigia simu, hakukuwa na maelezo yaliyo na mashiko. Ni wazi Polisi wa Kyela walitumwa tu na kwamba wao walikuwa wanatekeleza amri za wakubwa na hivyo Polisi wa Kyela hawawezi kulaumiwa. Itoshe kusema Askofu hana shida ye yote na Polisi wa Kyela na anawataka wawe na amani katika kutimiza majukumu yao.

Sisi Askofu hatujajua lengo la Polisi hao kufika nyumbani kwetu Itunge usiku huu wa manane. Kama sisi tungekuwepo kijijini kwetu, kamwe tusingekwenda kwa kujificha kwa kuwa hiyo si tabia yetu, hatujawahi kujificha na hatutajificha kwa kuwa sisi sio wahalifu.

Jeshi Polisi lina njia nyingi za kutaka kujua ni wapi alipo Askofu kuliko kwenda usiku kijijini kusumbua ndugu wa Askofu. Kama ni suala la Maandamano, hayo hayajaitishwa na Askofu, na kama Askofu angeitisha wala asingejificha. Yeye angetangaza hadharani kama alivyofanya mwezi Februari 2021 alipoitisha 'Matembezi ya Hiari' kuhamasisha umma kudai Katiba mpya na Tume Huru ya Uchaguzi wakati wa utawala wa Rais John Pombe magufuli.

Taarifa hiyo imetolewa na askofu mwamakula mwenyewe kwenye ukurasa wake wa Facebook.
 
askofu aachane na siasa, ajikite kwenye dini yake
Siasa haitengani na maisha ndiomana hata pamoja na sheria kutowataka askali kujihusisha na siasa akiwa na baada ya kustaafu bado tunaona kiongozi wa CCM amekufa na jeneza lake likafunikwa bendela ya jeshi la polisi hapo sio kuchanganya jeshi na siasa?
 
Polisi Kyela walifika Itunge, Kyela katika Mkoa wa Mbeya nyumbani kwa Askofu Mwamakula, usiku huu majira ya saa 6:40 usiku. Walipofika waligonga mlango, walipofunguliwa wakaulizia Askofu. Ndugu walishangaa kwani hawakuwa na taarifa kama Askofu angekuwa kule leo au hata wiki hii.

Polisi hawakuridhika hadi ndugu walipompigia simu Askofu na kuongea nao huku Polisi wale wakisikia na ndipo wakajiridhisha kuwa Askofu hakuwa pale na pia hakuwepo Itunge leo. Polisi wa Kyela walitumwa na wakuu wao ili wafike katika Makazi ya Askofu yaliyoko Itunge, Kyela katika Isyeto (Makaburi ya Chifu Bandekile) ili kuona kama Askofu yupo pale. Haijulikani pia kama Polisi wale walifika katika mji mwingine wa Askofu ulioko Itunge. Tutajua baadaye.

Askofu aliongea na Mkuu wa Polisi (OCD) wa Kyela kwa namba ya ndugu aliyekuwepo. Lakini Askofu alipouliza walifuata nini usiku na kuwa walishindwa nini kumtafuta yeye mchana hata kumpigia simu, hakukuwa na maelezo yaliyo na mashiko. Ni wazi Polisi wa Kyela walitumwa tu na kwamba wao walikuwa wanatekeleza amri za wakubwa na hivyo Polisi wa Kyela hawawezi kulaumiwa. Itoshe kusema Askofu hana shida ye yote na Polisi wa Kyela na anawataka wawe na amani katika kutimiza majukumu yao.

Sisi Askofu hatujajua lengo la Polisi hao kufika nyumbani kwetu Itunge usiku huu wa manane. Kama sisi tungekuwepo kijijini kwetu, kamwe tusingekwenda kwa kujificha kwa kuwa hiyo si tabia yetu, hatujawahi kujificha na hatutajificha kwa kuwa sisi sio wahalifu.

Jeshi Polisi lina njia nyingi za kutaka kujua ni wapi alipo Askofu kuliko kwenda usiku kijijini kusumbua ndugu wa Askofu. Kama ni suala la Maandamano, hayo hayajaitishwa na Askofu, na kama Askofu angeitisha wala asingejificha. Yeye angetangaza hadharani kama alivyofanya mwezi Februari 2021 alipoitisha 'Matembezi ya Hiari' kuhamasisha umma kudai Katiba mpya na Tume Huru ya Uchaguzi wakati wa utawala wa Rais John Pombe magufuli.

Taarifa hiyo imetolewa na askofu mwamakula mwenyewe kwenye ukurasa wake wa Facebook.
Duh...!. Hili la kuchanganya dini na siasa nilimuuliza huyu Askofu siku nilipokutana nae

View: https://youtu.be/L1VfloknySk?si=E4s9MfAP_VpVUR0a
P
 
Mtoto wangu akikua sitaki ajiunge na Polisi bora awe hata bodaboda, akijiunga atatafuta ukoo wake na baba ake mwingine.
Tema mate chini, siku ukipata mwanao au ndugu yako akiwa polisi na akafanikiwa kuwa na ka cheo utaishi maisha mazuri sana, yaani hata kama polisi akija kwako kuomba maji ya kunywa ukimwambia hebu ongea kwanza na afande x, lazima aage japo ana kiu.
 
Askofu Mwamakula alidiriki kuandamana kudai tume HURU ya UCHAGUZI na Katiba mpya utawala wa Magufuli.

Jambo sitalisahau.

Mungu ambariki sana.
 
Tema mate chini, siku ukipata mwanao au ndugu yako akiwa polisi na akafanikiwa kuwa na ka cheo utaishi maisha mazuri sana, yaani hata kama polisi akija kwako kuomba maji ya kunywa ukimwambia hebu ongea kwanza na afande x, lazima aage japo ana kiu.
Hayo ni mambo ya kizamani, nina ndugu tena ACP lakini simshobokei
 
Polisi wenyewe wanaishi maisha magumu hatari lkn kuchat kutwa wako na virungu kukandamiza wapigania haki.

Polisi wana vipele mwili mzima kwa kulalia magodoro yaliyochqkaa. Watoto wao wanasoma kayumba.

Na wanaishi kwa mikopo ya kausha damu. Nyambafu!!
 
Back
Top Bottom