Mbona humzungumzii Gwajima & the like? Hii hoja uliyokuja nayo sasa nimeshughulika nayo sana tu. Binafsi siungi mkonop watumishi wa Mungu wakati huo huo wanakuwa wanasiasa wa moja kwa moja huku wakisimaam madhabahuni kama wachunga kondoo, najua wanafanya usanii tu. Na mfano ni Gwajima. Nimetofautiana na wewe unapotaka kuonyesha kwamba viongozi wa dini wanapaswa kubaki kimya na kuachia wanasiasa wafanye upuuzi, na ukatoa mfano wa huyo "mtaalamu mmoja". Hilo nalipinga! Kufanya checks & balance kwa viongozi wa dini ni sehemu ya injili kama utapenda kuelewa leo.kazi ya askofu si kusimama kwa niaba ya watu anasima kwa niaba ya Mungu.Kazi za kusimama kwa niaba ya watu ni za wanasiasa wakiwemo wabunge ,wanaharakati nk
Yesu aliona wazi katiba ilikuwa mbaya lakini msikilize hapa alichoongea akasema ya Mungu yabakie ya Mungu na kaisari yabakie huko kwa Kaisari
Ulaya makanisa yamekufa yalipojiingiza kwenye siasa hamna watu wanasali makanisani tena waklijitia ohh kanisa linatakiwa kushiriki siasa vikaanzishwa hadi vyama vya kidini mfano ujerumani chama tawala kwa sasa kinaitwa CHRISTIAN DEMOCRATIC UNION cha ANGELA MERKEL .WAtu wakahamasika kweli kuihoji serikali lakini mwamko huo ukaenda mbele zaidi watu wakaanza kuhoji mambo ya kanisani ikiwemo doctorins kwa kisingizio kile kile kuwa kama maaskofu wanahammisaji watu kuhoji serikali bunge na mahakama kwa nini kanisa lisihojiwe? Maaskofu wakaanza kuwekwa kitimoto!!! La kwanza lilihojiwa ni kuwa kulikuwa na kodi mbili kodi ya kwanza unakatwa kwenye mshahara inaenda serikalini na kod ya pili unakatwa kwenye mshahara inaenda kanisani .Wakaenda bungeni kupinga kuwa si kila mtu anasali hiyo kodi ikatwe tu kwa wanaosali .Ikapita watu walipoona wasiosali hawakatwi kodi wengi wakaacha kusali ili wasikatwe kodi ya kanisa!!! Sasa hivi mikanisa mingi ulaya haina waumini na yanauzwa kwa minada hata ukiingia goole iko kibao ,Michungaji na miaskofu kibao ikaachishwa kazi sababu mikanisa haina hela za kuwalipa!!!
Sasa hivi chama cha siasa cha CHristian Democratic UNION ndio kimenawiri kanisa limesinyaa!!!
Huyo ASkofu mwamakula ona watu wanavyofurika mikutano yake ya siasa !!! Ajaribu kuitisha mkutano wa injili uone hapati mtu!!! Mchungaji Mtikila pia alikuwa na hilo tatizo watu wanajaa mikutano yake ya siasa ukienda kanisani kwake Ilala boma anasali yeye mke wake na nduguze hawafiki wanne!!! HAYO NDIO YA askofu Mwamakula uliza kanisa lake hata liko wapi hakuna humu anayeweza hata kukuonyesha !!! unaishia kuona tu kavaa minguo ya kiaskofu aliyojishonea mwenyewe kwa fundi cherehani
Hii trend ya maaskofu kujitosa kwenye siasa sio nzuri kwa afya ya kanisa in the short run and in the Long run time
Kiongozi wa dini abaki kanisani